- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hotuba ya Amir wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Hijria ya Kuvunjwa Khilafah
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na Maswahaba zake, na waliomfuata.
Kwa Ummah wa Kiislamu, kwa jumla… na kwa wabeba Da’wah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida, hasa…
Katika siku hii, tarehe 28 Rajab mwaka 1342 H, sawia na tarehe 3 Machi mwaka 1924 M, yaani, miaka 102 ya Hijria iliyopita, makafiri wakoloni, wakiongozwa na Uingereza wakati huo, wakishirikiana na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, waliweza kuiondoa dola ya Khilafah. Mustafa Kemal alitekeleza jinai ya ukafiri wa wazi, kwa kuiondoa Khilafah huko Istanbul, huku akimzingira Khalifa, na kumpeleka uhamishoni katika majira ya mapema siku hiyo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Msiba huu mchungu ulitokea, kwa kuvunjwa Khilafah, ndani ya Ardhi za Kiislamu... Ilikuwa ni faradhi juu ya Ummah kupigana na yule anayetekeleza ukafiri wa wazi kwa upanga, kama ilivyosimuliwa katika Hadith iliyopokewa na Bukhari na Muslim ya Mtume (saw), kutoka kwa Ubada ibn al-Samit (ra), «وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ» “Na tusizozane na wenye mamlaka isipokuwa mukiuona ukafiri ulio wazi ambao mnao ushahidi wa wazi mbele ya Mwenyezi Mungu.” [Bukhari na Muslim] Hata hivyo, Ummah haukufanya chochote kumtingisha mhalifu huyo na wasaidizi wake, kiasi kwamba yeye na washirika wake wangegeuzwa kuwa wenye hasara. Badala yake, jibu lilikuwa dhaifu na halikuwa karibu na hilo!
Hapo ndipo historia ya Ummah ilipotiwa giza. Hapo awali, Khilafah ilikuwa ni dola ya Ummah, iliyosimama juu ya haki na uadilifu lakini sasa Ummah una zaidi ya vijidola hamsini, vyenye madhara makubwa kutoka kwa watawala wao. Hata tetemeko la ardhi la Syria na Uturuki, katikati ya mwezi huu wa Hijri wa Rajab, halikuweza kuondoa mgawanyiko wao, na kuregesha umoja wa dola moja. Badala yake, waliendelea kama vipande vilivyopasuka, kabla na baada ya tetemeko la ardhi, wala hawakujali! Amesema Mwenyezi Mungu (swt),﴾أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا ﴿يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُون “Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.” [Surah At-Tawba 9:126].
Hata hivyo, janga la tetemeko hili la ardhi lilidhihirisha kwamba Uislamu umekita kwa kina ndani ya Waislamu. Walipokuwa wakiwaokoa ndugu zao kutoka chini ya vifusi, Waislamu walipiga takbira. Takbira hazikukoma katika ndimi zao, hasa walipokuwa wakimuokoa mtoto mchanga ambaye mama yake alimzaa, kisha akafa chini ya kifusi... ama yule ambaye alifinikwa na kifusi, huku mkono wake ukionekana umeshika tasbihi, ambayo kwayo alikuwa akimtukuza Mwenyezi Mungu (swt)... au walipokuwa wakijaribu kumtoa mwanamke kutoka chini ya jengo lililobomoka, mwanamke huyo aliomba afinikwe kichwa chake, kabla ya kutolewa nje, ili nywele zake zisionekane au pale yule aliyeita kutoka chini ya kifusi ili atolewe, aliomba kwanza maji ya kutawadha kabla ya swala ili wakati wa kuswali usimpite... kisha yule waliyekuwa wakijaribu kumuokoa kutoka katikati ya vifusi, na wakamkuta anasoma Surat Al-Baqarah ndani ya Quran ... au msichana ambaye walikuwa wanajaribu kumtoa, ambaye anaelezea huzuni yake kwa sababu hakuweza kuswali siku hiyo ... wakati wote huo, takbira zilisikika, Allahu Akbar... Hawa ndio Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu kila Muislamu aliyefariki wakati wa tetemeko la ardhi. Wawe miongoni mwa mashahidi wa Akhera, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) awaponye waliojeruhiwa, kwa tiba isiyoacha maradhi nyuma… Mwenyezi Mungu (swt) amnusuru kila Muislamu aliyesalimika. Mwenyezi Mungu (swt) amjaalie maisha mema, ayatumie katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw)...
Hawa ndio Waislamu, ilhali hao ndio watawala katika Ardhi za Kiislamu. Kwa kweli wametofautiana mbingu na ardhi. Pengo hili la utofauti lilitokea katika kipindi hiki cha miaka 102 Hijria, tangu msiba mkubwa wa kuondolewa kwa Khilafah! Kisha, kwa kupatiliza kuanguka kwa Khilafah, makafiri wakoloni walileta msiba mwingine wa kuumiza. Wakawapa Mayahudi dola katika Ardhi Iliyobarikiwa, mahali pa Israa (safari ya usiku), na asili ya Miraaj (kupaa) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kisha wakawapa njia za kuishi. Kubwa zaidi katika njia hizo ni kulinda usalama wake kupitia watawala vibaraka wanaoizunguka. Kwa hivyo wakashindwa na Mayahudi katika kila vita vilivyotokea, mpaka wakaipa dola ya Kiyahudi sura nyengine isiyokuwa ile sifa ambayo Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu kwayo: ﴾وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَة﴿ “na wamepigwa na unyonge.” [Surah Aali Imran 3: 112]. Na watawala hawa hawakuridhika na hilo pekee. Badala yake, walifanya jitihada zote za kuibadilisha kadhia hiyo kutoka kuondolewa kwa umbile la Kiyahudi, hadi kujadiliana nayo, kwa ombi kwamba ingejiondoa kutoka kwa baadhi tu ya yale maeneo waliyoyakalia kimabavu mwaka wa 1967!
Zaidi ya hayo, dola ya Mayahudi ilikuwa, na bado ingali inatenda jinai mbaya sana nchini Palestina. Mauaji ya Jenin, mnamo tarehe 26 Januari 2023, yanashuhudia hilo. Jeshi la umbile la Kiyahudi, likiwa na vikosi vikubwa na vyenye silaha nzito, lilivamia kambi ya Jenin, na kutekeleza mauaji makubwa ambapo watu tisa waliuawa shahidi. Wakati huo, walitekeleza uhalifu mbaya zaidi kupitia kuua, kubomoa kuta juu ya waliojeruhiwa, na kukanyaga kwa matingatinga. Kisha likaendelea na uchokozi wake dhidi ya Nablus, kuivamia Kambi ya Aqabat Jaber, kuua na kujeruhi, na kusababisha mashahidi na majeruhi… na yote haya yalitokea bila ya watawala katika Ardhi za Kiislamu kuhamasishana kuwaokoa. Badala yake, mfano bora zaidi wao ni yule ambaye alitoa upatanishi wake kati ya mhalifu na mhasiriwa aliyetendewa uhalifu. Mwenyezi Mungu awaangamize; wanadanganyika vipi? Na wanafanyaje zaidi ya hayo huku wakikimbilia kufanya uhalifu wa kuhalalisha mahusiano na Mayahudi? Baada ya watawala wa Misri kuongoza maandamano haya ya udhalilishaji na fedheha, PLO na kisha watawala wa Jordan, Imarati, Bahrain na Morocco mtawalia, wote walifuata mkondo huo. Na hii hapa Sudan inawafuata katika uhalifu huo kwani Rais wa Sudan, Al-Burhan, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kiyahudi Eli Cohen jijini Khartoum mnamo tarehe 2 Februari 2023 kujadili uhalalishaji mahusiano! Hakuna hata mmoja wao anayejali udhalilifu unaowazunguka. ﴾سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ﴿ “Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Surah Al-Anaam 6:124].
Kwa hakika ni ajabu kwamba kwa kila ongezeko, au kila uhalifu unaotendwa, na umbile la Kiyahudi, viongozi wake, siku moja kabla au siku hiyo hiyo, wako mikononi mwa watawala wa Kiarabu, au kwenye ziara kwao. Kabla ya uhalifu dhidi ya Jenin, Netanyahu alikuwa mgeni katika kasri la utawala wa Jordan! Wakati wa uhalifu dhidi ya Jenin, Mamlaka ya Palestina ilikuwa ikiratibu usalama na Mayahudi, kwa kukubali kwake yenyewe kwa sababu ilidai kwamba ingesitisha uratibu wa usalama, baada ya uhalifu huo. Hivyo, ndivyo ilivykuwa! Hata hivyo, cha kustaajabisha na kushangaza zaidi ni kwamba, pindi mmoja wa mashujaa wa Palestina alipoilinda ardhi yake na watu wake, na kuwaua Mayahudi saba katika operesheni ya Al-Quds, baada ya mauaji ya Jenin, watawala katika nchi za Kiislamu walikimbilia kulaani! Wizara za mambo ya nje za Uturuki, Imarati, Jordan na Misri, zote zililaani operesheni ya Al-Quds katika taarifa kwa vyombo vya habari!
Sasa, sio Palestina pekee iliyochomwa kisu mgongoni na watawala hawa bali pia walikubali au kuyasalimisha, maeneo mengine matukufu ya ardhi ya Uislamu. Kashmir iliunganishwa kwa nguvu na washirikina wa Kibaniani, katika dola yao, huku watawala wa Pakistan wamekaa kimya ... Waislamu wa Rohingya wanachinjwa huko Myanmar (Burma), huku watawala wa Bangladesh ni kana kwamba wamelala, bila kuona ... kisha kuna Turkistan Mashariki, ambapo China inafanya mauaji makubwa, huku dola za sasa katika Ardhi za Kiislamu zikidumisha kimya kama kimya cha makaburi. Kila wanapozungumza kuhusu mauaji hayo hudai kuwa ni mambo ya ndani ya China! ﴾كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً﴿ “Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.” [Surah Al-Kahf 18:5].
Kisha makafiri wakoloni hawakuridhika na fedheha waliyoufanyia Ummah. Badala yake walikiuka imani yake. Hivyo yule mtu duni aliyepitiliza mipaka alichoma nakala ya Quran Tukufu mbele ya jengo la ubalozi wa Uturuki, jijini Stockholm, mnamo Jumamosi 21 Januari 2023, baada ya mamlaka ya Uswidi kuruhusu hilo... Kisha uhalifu wao ukaendelea hadi kuchomwa kwa Qur'an Tukufu huko The Hague na kisha Copenhagen mnamo Ijumaa, 27 Januari 2023. Baadaye, tuliitazama Al-Azhar, kupitia Mwangalizi wake wa Al-Azhar wa Kupambana na Misimamo mikali, ikitoa taarifa yenye maneno makali ya kulaani na kutaka kusimama kupinga majaribio ya kukiuka matukufu ya kidini. Hapana shaka kwamba Wanazuoni wa Al-Azhar wanajua kwamba jibu la kuchomwa moto kwa Qur'an Tukufu si laana ya maneno tu, bali ni lazima majeshi yakusanywe kunusuru Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Dini yake. Kuchoma moto Qur’an Tukufu ni tangazo la vita dhidi ya Umma wa Kiislamu na imani yake. Kwa hiyo, jibu ni vita vinavyotoa mfano kuogofya kwao, ili kuwazuia wengine. Amesema Mwenyezi Mungu (swt), ﴾فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُون﴿ “Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Surah Al-Anfaal 8: 57].
Enyi Waislamu: Uchokozi dhidi ya Waislamu haukabiliwi kwa maneno ya mapambo kwa ajili ya kuonekana, kauli tupu zisizonufaisha wala kukidhi haja. Badala yake uchokozi unajibiwa kwa makali ya upanga, kwa mapigo yanayomfanya adui asahau minong'ono ya Shetani. Hivi ndivyo walivyokuwa Waislamu walipokuwa na Khilafah, na mwenendo wa matukio katika utawala wao unazungumzia pakubwa hilo. Huu ni ukweli uliothibitishwa kwamba hakuna mtu mwenye macho na ufahamu anayeweza kukataa. Mifano yake ipo katika historia ya Waislamu ambayo imepokewa katika (kitabu cha) “Mwanzo na Mwisho” (Al-Bidaya wa Al-Nihaya) cha Ibn Katheer, “Ufunguzi wa Ardhi” cha Al-Baladhuri, “Historia” cha Ibn Khaldun na “Historia ya Uislamu” cha Al-Dhahabi, miongoni mwa vyanzo vyengine. Sasa nawanukulia kutoka kwao:
“Kisha ukaja mwaka wa 87 baada ya Hijrah... ndani yake Qutayba ibn Muslim akafungua Poykent, ambayo ni moja ya wilaya za Bukhara... na haikufika adhuhuri Mwenyezi Mungu (swt) aliwapa ushindi... Yule aliyewashambulia Waislamu alikuwa mtu mwenye jicho moja, kutoka miongoni mwao. Alipokamatwa, alisema, “Ninajikomboa kwa mavazi elfu tano ya Kichina, ambayo thamani yake ni maelfu kwa maelfu.” Hivyo makamanda wakamshauri Qutayba kukubali hilo kutoka kwake. Qutayba akasema, "Hapana, Wallahi, kamwe hutatia hofu kwa Muislamu tena." Kisha akaamrisha kuhusiana naye na shingo yake ikakatwa…”
“Kisha ukaja mwaka wa 90 baada ya Hijrah... ndani yake Raja Dahir, mtawala wa Sindh, aliishambulia meli iliyokuwa imebeba wanawake wa Kiislamu, na kuwachukua mateka. Hivyo Khalifa alituma risala kwa wali (gavana) wake ili kulipiza kisasi kwa dhalimu huyo. Hivyo Muhammad bin Al-Qasim aliongoza jeshi na kuwaokoa wanawake wa Kiislamu, akalipiza kisasi kwa mtawala huyo dhalimu na akaiteka ardhi ya Sindh.”
“Kisha ukaja mwaka wa 223 baada ya Hijrah, na Mfalme wa Byzantino akaenda kwenye Ardhi za Waislamu, akiwaua na kuwateka nyara watu wa Zabtara. Mwanamke mmoja akapaza sauti, “Ewe Mu’tasim, uko wapi.” Wito huu ulimfikia Khalifa al-Mu’tasim, ambaye alijibu, “Niko kwenye huduma yako.” Yeye binafsi aliongoza jeshi na kulipiza kisasi kwa mwanamke huyo. Aliuliza ni ipi kati ya ardhi za Byzantino ilikuwa kubwa zaidi. Aliambiwa kwamba ilikuwa Amuriyya, ambayo ilikuwa "karibu na Ankara." Kwa hiyo akaifungua.”
“Kisha ukaja mwaka wa 582 baada ya Hijrah... ndani yake Arnat (Raynald), mvamizi wa Al-Karak, kwa khiyana alifunga njia, kwa ajili ya msafara mkubwa wa Mahujaji, ambao ulitoka Misri ambaye aliwaua na kuwateka nyara. Hivyo Sultan Salah ud-Din alijiandaa kwa ajili ya vita. Aliomba askari kutoka nchini. Aliapa kwamba kama angemshinda Arnat, angemuua. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamjaalia kuwa mshindi katika mwaka wa 583 baada ya Hijrah, katika Vita vya Hattin, katikati ya Rabi’ Al-Akhir. Kisha Salah Al-Din akamuua Arnat, kwa mkono wake mwenyewe, kama adhabu kwa ajili ya khiyana yake na kuziba njia. Hapo ndipo ukombozi wa Al-Aqsa ulipotokea, mnamo tarehe 27 Rajab, 583 baada ya Hijrah.”
“Kisha mwaka 1307 baada ya Hijrah, mwaka 1890 M, mtunzi wa skripti iliyomkashifu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), akajaribu kuionyesha kama mchezo wa kuigiza, katika moja ya kumbi za sinema jijini Paris. Khalifa Abdul Hamid alipopata habari hii, alimwita balozi wa Ufaransa jijini Istanbul na akakutana naye kwa makusudi akiwa amevalia sare za kijeshi. Kisha akamtishia kwamba ikiwa itaonyeshwa, Dola la Kiuthmani itatangaza kukata uhusiano na Ufaransa, katika hali ya vita. Akamwambia kwa sauti ya ukali, akisema, "Mimi ni Khalifa wa Waislamu ... nitageuza ulimwengu juu ya vichwa vyenu, ikiwa humtausitisha mchezo huu." Ufaransa ilijibu kwa kuzuia mchezo huo kuonyeshwa…”
Makafiri wakoloni walikuwa wakijua, wakati huo, kwamba ukiukaji wowote wa matukufu ya Uislamu, na Waislamu, ungekabiliwa na kukatwa ndimi na kuvunjwa viungo... Leo hii Quran Tukufu, Mtume (saw) na Ardhi za Waislamu zinashambuliwa, wakati uchokozi haulipizwi kisasi!
Hii ni kwa sababu tu hakuna Imam, Khalifa Rashid (Khalifa Muongofu), anayeulinda Ummah kutokana na shari za maadui. Imepokewa katika Hadith iliyo sahihi iliyopokewa na Bukhari na Muslim, kwamba amesema (saw): «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ، يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ، وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake, na hujihami kwake.” [Bukhari na Muslim]
Kwa kutamatisha, narudia ombi langu kwenu, Enyi watu wenye nguvu na ulinzi... Nyinyi pekee ndio mnaoweza kuuponya moyo wa Ummah kutokana na maadui zake, maadui wa Dini yenu. Nyinyi pekee ndio mnaoweza kukomesha udhalilifu uliowafikia Waislamu katika ardhi zao... Basi inukeni kutekeleza wajibu wenu, Mwenyezi Mungu (swt) awabariki. Inukeni ili mutupe Nusrah yetu, Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida. Sio tu njia pekee ya ushindi katika hali halisi ya sasa. Badala yake, ni kwa sababu ni faradhi kubwa ya kwango cha kwanza. Kwanza, yeyote asiyefanya kazi na hali ana uwezo wa kusimamisha Khilafah, na kusimamisha Khalifah anayestahiki Bayah (ahadi ya utiifu), basi dhambi lake ni kubwa kana kwamba amekufa kifo cha kabla ya Uislamu (Jahilliyah), ikidhihirisha ukali wa madhambi kama alivyo sema, «وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Na atakaye kufa ilhali hana bay’ah (ahadi ya utiifu kwa Khalifa) shingoni mwake, amekufa kifo cha kijahiliya.” [Muslim]. Pili, Waislamu walichukua kiapo cha Bayah kwa Khalifa, kabla ya kuanza maandalizi mazishi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kutekeleza wajibu wa mazishi yake. Yote hayo yanatokana na umuhimu wa Khalifah. Tatu, Umar (ra) siku ya kifo chake, aliweka kikomo cha muda, cha siku tatu na si zaidi, kwa ajili ya kumchagua Khalifa miongoni mwa wale sita waliopewa bishara ya Pepo. Ikiwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuhusu Khalifa, ndani ya kipindi hicho, basi mpinzani alipaswa kuuawa. Hili lilikuwa ni katika ijmaa ya Maswahaba (ra) ambao hakuna uovu wowote ulioripotiwa kuwahusu. Hivyo, ilikuwa ni Itifaki ya pamoja ya Maswahaba (ra). Hata hivyo, kwetu sisi, “siku tatu nyingi” zimepita juu yetu! Hakika kusimamisha Khilafah ni jambo kubwa.
Enyi Wanajeshi wa Mwenyezi Mungu: Tunatambua kwamba Malaika hawatashuka kutoka mbinguni ili kutusimamishia Khilafah. Bali Mwenyezi Mungu (swt) atatuteremshia Malaika watusaidie tu ikiwa tutafanya kazi kwa bidii katika kusimamisha Khilafah. Ni ahadi iliyothubutu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ﴾ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ﴿ “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [Surah An-Nur 24:55]. Ni bishara njema ya izza, baada ya utawala huu wa kidhalimu, katika hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt), «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “…Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo katika muda upendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” Kisha yeye (saw) akanyamaza. [Imepokewa na Ahmad]. Pia tunatambua kwamba maadui wa Uislamu wanaona kusimamisha tena kwa Khilafah ni jambo lisilowezekana. Wanarudia kauli ya wafuasi wao kutoka miongoni mwa wanao kejeli, ﴾غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ﴿ “Watu hawa dini yao imewadanganya.” [Surah Al-Anfal 8:49]. Lakini kama vile msemo huo ulivyokuwa laana kwa wale waliotangulia kuusema, kwani Mwenyezi Mungu ameitukuza Dini yake na akawapa ushindi watu wake, ni laana kwa wale wanaousema leo, kwani Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, yuko pamoja na waja wake wenye ikhlasi wanaofanya kazi kwa bidii, bila ya kutoka katika nyoyo zao na viungo vyao, kauli ya Mwenyezi Mungu (swt), ﴾إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً﴿ “Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [Surah At-Talaq 65:3]. Kila uchao, wanakaribia kwenye Qadr “azma,” hii kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). ﴾وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيبًا﴿ “na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Surah Al-Israa 17:51].
Wa Alaikum Assalaam wa Rahmutallahi wa Barakaatahu
Ndugu Yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, 28 Rajab 1444 H
Amiri wa Hizb ut Tahrir 19 Februari 2023 M