Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tanzia na Rambirambi za Amiri wa Hizb ut Tahrir kwa Kifo cha Mhandisi Ismail Al-Wahwah (Abu Anas)
(Imetafsiriwa)

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surah Al-Ahzab 33:23]

Amiri wa Hizb ut Tahrir anatoa salamu za rambirambi kwa Waislamu kwa jumla, na kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir haswa, juu ya ndugu mtukufu, ambaye tulimpoteza katika Alfajiri ya Alhamisi, Mei 18, 2023, nchini Australia.

Abu Anas, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu, alikuwa ni miongoni mwa nguzo za Hizb, kwani alikuwa mwanachama wa Afisi ya Amiri, mwenye historia ndefu ya kupinga dhulma, na kusimama imara juu ya haki, bila ya kuteteleshwa na dhiki na mitihani wala magereza na mateso ya wadhalimu. Badala yake, alizidi nguvu juu ya nguvu, akifanya kazi kwa ikhlasi na ukweli, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu...

Katika dunia hii, macho yake yaliitazama Rayah (bendera) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo inanyanyuka kutoka kituo kimoja cha juu hadi chengine ... na huko Akhera, kama alivyosema (swt),

[إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ * فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ]

“Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. (*) Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.” [Surah Al-Qamar 54:54-55].

Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu ndugu yetu na amuingize kwenye Jannah yake pana, na amkusanye pamoja na Manabii (as), wakweli, mashahidi na watu wema. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie sisi na jamaa zake na Waislamu tuwe kama Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu alivyosema,

[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ]

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Surah Al-Baqarah 2:156-157].

Mwenyezi Mungu (swt) akurehemu, ewe Abu Anas, kwa rehma pana... Hatusemi ila yale aliyoyasema (saw) pale alipompoteza kijana wake mboni ya jicho lake, Ibrahim,

«إِنَّ الْعَيْنَ تَدْمَعُ وَالْقَلْبَ يَحْزَنُ وَلَا نَقُولُ إِلَّا مَا يَرْضَى رَبُّنَا وَإِنَّا بِفِرَاقِكَ يَا إِبْرَاهِيمُ لَمَحْزُونُون»

“Hakika jicho linabubujika machozi na moyo unahuzunika, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu, na hakika sisi kwa kutengana nawe ewe Ibrahim ni wenye huzuni.” [Bukhari, Muslim]

Mwenyezi Mungu (swt) akurehemu, ewe Abu Anas, rafiki yetu mwandani wetu katika njia yetu. Inna lillah wa Inna Ilaihi Rajioun, Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutarejea.

Ndugu Yenu na mwandani wenu katika njia,                                                                    28 Shawwal 1444 H

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah                                                                                            18 Mei 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu