- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na Mashababu (wa Hizb ut Tahrir) Hasa katika Sikukuu ya Idd Al-Adha 1446 H sawia na 2025 M
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na wanaomfuata, nk…
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd
Kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla... Umma bora uliowahi kuletwa kwa ajili ya wanadamu, unaoamrisha mema na kukataza maovu na unaomuamini Mwenyezi Mungu Al Aziz Al Hakim.
Kwa wabebaji Da’wah hasa... Mwenyezi Mungu awape ushindi mikononi mwao na awanusuru kwa nusra yake wasimamishe dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.
Kwa wageni waheshimiwa wanaozuru tovuti wanaokuja kuona kheri inayoleta... wanaojitahidi kadiri wawezavyo kutetea haki na kuwanusuru watu wake.
Kwa wote hao, Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,
Nakupongezeni kwa Idd Al-Adha iliyobarikiwa 1446 H ... na namuomba Mwenyezi Mungu Al Qawi Al Aziz iwe ni bishara ya kheri na baraka kwa Waislamu wote.
Kina kaka na dada waheshimiwa,
Idd hii inawasili na uvamizi wa Kiyahudi, unaoungwa mkono na Marekani na silaha zake, bado unaendelea dhidi ya Gaza Hashim na Palestina yote. Na watawala katika nchi za Waislamu wanatazama yanayotokea, mbora wao ni yule anayepatanisha kana kwamba yuko kundi lisilofungamana na upande wowote, bali yuko karibu zaidi na Mayahudi. Si ajabu kwamba Marekani, makafiri wakoloni na umbile lao, dola ya Kiyahudi, wanatushambulia. Ni maadui wa Uislamu na Waislamu, sio kuanzia leo bali wa miaka iliyopita. Wala si ajabu kwamba makafiri wakoloni kwa kuegemea sheria za kimataifa wanaweza kuzishambulia nchi za Waislamu kwa sababu sheria hii ilianza kwa mara ya kwanza dhidi ya Waislamu na dola yao (Dola ya Uthmani) kwenye Kongamano la Westphalia mwaka 1648, ambalo baadaye likawa Ligi ya Mataifa na kisha Umoja wa Mataifa. Hayo yote si maajabu, lakini cha ajabu ni kwamba watawala wa nchi za Waislamu zinazopakana na Palestina wanatazama jinai na mauaji yanayoendelea huko huku wakiwa wamenyamaza kimya na kuyazuia majeshi kunusuru (nusrah) Gaza, na kwa hakika Palestina yote. Bali wamehakikisha utekelezaji wa maazimio ya kimataifa ambayo yalikuwa ni mauti kwa Waislamu, Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali, jinsi wanavyodanganyika!
Kwa kumalizia, fanyeni haraka, enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu, kuwanusuru ndugu zenu wa Gaza, na ikiwa tawala za kidhalimu katika nchi za Waislamu zitasimama katika njia yenu, basi ziondoeni kwa njia zote... na msimamishe utawala wa Mwenyezi Mungu mahali pao, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, katika kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha kutakuwepo na utawala wa kidhalimu (ملكًا جبرية), na utadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza.” [Musnad Imam Ahmad] Na kisha hapo, wasaidizi wake, na askari wa Uislamu, kutoka ngazi ya juu kabisa hadi ya chini kabisa, watakwenda kutoka ushindi mmoja hadi mwingine, wakipiga Takbira na Ummah wakipiga pamoja nao, watakuwa na nguvu kwa Mola wao na Dini yao, hivyo hakuna adui atakayesubutu kuwa na umbile katika ardhi ya Uislamu.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi. * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.aa” [Ar-Rum: 4-5]
Kwa kumalizia, namuomba Yeye (swt) kwamba Idd hii iwe ndio mwanzo wa kheri, baraka, na izza kwa Uislamu na Waislamu.
[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُون]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd
Wassalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
10 Dhul Hijjah 1446 H Ndugu Yenu
06 Juni 2025 M Ata Bin Khalil Abu Al Rashtah