Alhamisi, 27 Safar 1447 | 2025/08/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  24 Safar 1447 Na: H 1447 / 09
M.  Jumatatu, 18 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ufuatiliaji Mkubwa wa Mkoloni Amerika juu ya kile kinachoitwa “Mageuzi” sio Chengine ila ni Jaribio la kupanua Udhibiti wake nchini Bangladesh

(Imetafsiriwa)

Balozi Mdogo wa Marekani jijini Dhaka, Tracy Ann Jacobson, alifanya mkutano na Profesa Ali Riaz, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Maridhiano wiki iliyopita ili kuuliza kuhusu mipango ya mageuzi inayoendelea na maendeleo yake. Jacobson na manaibu wake wamekuwa wakifanya mfululizo wa mikutano na wawakilishi wa vyama vikuu vya kisiasa. Kama sehemu ya ushirikiano wa Marekani ‘kukuza demokrasia’ nchini Bangladesh, tunaona mikutano na taarifa za mara kwa mara kutoka kwa Ubalozi wa Marekani nchini Bangladesh na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani zinazohimiza marekebisho katika utawala. Kusiwe na shaka kwamba msukumo wa Marekani wa kuleta mageuzi na kile kinachoitwa ‘uwajibikaji wa kidemokrasia’ haukusudiwi kheri ya watu wetu. Katika historia, mbeberu mamboleo Marekani imekuwa ikiunga mkono madikteta kwa maslahi yake huku ikitetea ‘demokrasia’ na ‘haki za binadamu’. Imetanguliza maslahi yake ya kimkakati na ya kiushindani (kama vile ‘Mkakati wa Indo-Pasifiki’ - msingi wa sera ya kigeni ya Marekani) juu ya kukuuza maadili ya kidemokrasia au haki za binadamu katika kanda hii. Tulishuhudia hali hii ya unafiki katika sera ya Marekani wakati imedumisha uhusiano wa kidiplomasia na wa kimkakati na serikali ya kimabavu ya Hasina kwa maslahi yake ya kijiografia huku ikiweka vizuizi ‘wakilishi’ vya visa  kwa maafisa fulani wa usalama wa Bangladesh wanaohusika na haki za binadamu. Siasa za kidemokrasia za Magharibi zimekita mizizi katika aina hii ya mbinu ya kuhadaa. Nyuma ya barakoa ya demokrasia na haki za binadamu, Marekani daima huficha udanganyifu wake, na kuingilia kati siasa za nchi nyingine kupanua udhibiti wake. Kwa hivyo, ufuatiliaji wa mara kwa mara wa Marekani kwenye ‘onyesho la kijasusi’ la kisiasa lililofichwa kama ‘mageuzi’ si chochote ila kutia ushawishi wa kiuchumi, kisiasa na kithaqafa kudhibiti Bangladesh. Bangladesh ina thamani muhimu ya kimkakati kwa Marekani, na serikali yenye ushirikiano zaidi kuliko ya Hasina inaweza kuhudumia vyema maslahi ya kimkakati ya Marekani katika eneo hili. Kwa hiyo, kwa jina la ‘kuunga mkono’ mageuzi ya Bangladesh, Mbeberu Marekani inaishinikiza Bangladesh iwiane na mfumo wa usalama wa Marekani ili kukabiliana na China na kuzuia kuongezeka kwa muibuko wa Uislamu wa kisiasa yaani, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi Watu, sababu ya iliyokufaneni kusimama dhidi ya dhulma ya Hasina, kumwaga damu, na kutumainia mabadiliko ya kweli, yote haya yatakuwa bure kwa sababu serikali hii ya mpito, wanasiasa na wasomi wa nchi yetu wamefeli vibaya sana kukuongozeni kuelekea kwenye njia iliyo sawa. La kusikitisha, bado hawako tayari kukiri kwamba ‘sababu halisi’ ya ukandamizaji haikuwa dikteta Hasina. Haijalishi ni serikali gani inaingia na haijalishi ni 'masuluhisho gani mapya ya kisiasa' yataundwa, hatutakombolewa isipokuwa tuweze kujinasua kutoka katika mtego wa mfumo huu wa kilimwengu wa Kimagharibi, sababu halisi ya masaibu yetu. Kwa hivyo, hata baada ya kuondolewa madarakani Hasina, mabadiliko yenu munayoyataka hayaji isipokuwa utekelezaji mzuri wa ajenda ya Amerika. Enyi Watu, uasi wenu tayari umetekwa nyara na mfumo wa zamani unarudi polepole. Msifanye makosa kufikiria kuwa mfumo wa zamani unamaanisha mfumo wa Hasina. Badala yake, suluhisho la kisiasa la Kimagharibi linaloongozwa na Marekani ndiyo mfumo mkuu unaowalea wanasiasa, wawe wa kidikteta au wa kidemokrasia kwa ajili ya maslahi yao. Mfumo huu wa kilimwengu unadumishwa na mbeberu Amerika. Lakini hata hivyo, wanafikra wa kisiasa wa nchi hii wanakuambieni kuwa kupima mambo kiakili. Macho mwao, India ni tishio la moja kwa moja kwa ubwana wetu na suluhisho la kivitendo kwa hili ni kuwa ndani ya mzunguko wa Amerika. Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inakuombeni mukatae mitego hii na udanganyifu uliofichwa kama ‘marekebisho’. Pazeni sauti yenu kwa ajili ya Khilafah iliyoahidiwa kwa njia ya Utume ambayo inaweza kuhakikisha mabadiliko ya kweli na kutukomboa kutoka kwenye makucha ya Wabeberu makafiri.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele...” [Surah Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu