- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Khilafah pekee ndio inayojali Maslahi ya Watu na ndio Mlinzi wa Haki na Mahitaji yao
(Imetafsiriwa)
Hali mbaya ambayo Sudan imefikia kufuatia vita vya kikatili vilivyoanza miaka miwili iliyopita kati ya vikosi vya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka sio siri. La kusikitisha, watu wasio na hatia wa Sudan wamelipia, na wanaendelea kulipia, gharama ya mzozo huu mbaya wa kimataifa unaoendeshwa na silaha za ndani kwa lengo la kuichana nchi na kulinda maslahi ya Amerika, Ulaya, na wengineo!!
Kila mwenye ikhlasi katika Ummah huu anashangaa vipi makundi mawili yanayopigana yametosheka kuchafua mikono yao kwa damu ya ndugu zao, na vipi wamekubali kuongozwa na maslahi yao wenyewe na ya mabwana zao?! Lau wangemcha Mwenyezi Mungu, wasingalikubali yanayotokea! Lau Uislamu ungetabikishwa, nchi za Magharibi zisingeweza kuzurura nchi nzima kwa uhuru na kutekeleza ajenda zao kwa kuwachochea wapiganaji na kuwapa silaha na zana!
Utawala katika Uislamu kimsingi unategemea kuchunga mambo ya watu na kuhakikisha maslahi na mahitaji yao. Kimsingi unahakikisha amani na usalama kwa raia wake wote. Khalifa anafahamu kuwa ataulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu juu ya yale aliyokabidhiwa. Kwa hiyo, anafanya kila awezalo kuhakikisha usalama wa watu na usalama wa maisha yao, kwani anatambua kuwa kuua mtu mmoja ni mbaya zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuibomoa Al-Kaaba! Kwa hiyo, Imam ni ngao ya kulindwa kwaye, kwani yeye hulinda na kuepusha uvamizi na kulinda maisha, fedha na mali pia. Ndio maana Umar ibn al-Khattab (ra) alikuwa akiwapaka dawa ngamia wa sadaka mwenyewe kwa kuhofia wasije wakafa, na akasema: “Ikiwa ngamia mmoja atakufa kwa bahati mbaya kwenye kingo za mto Furat, mimi nahofia kwamba Mwenyezi Mungu ataiuliza familia ya al-Khattab.”
Na kwa Mwenyezi Mungu tunashtakia masaibu ya ndugu zetu wa Sudan, ambako uhai wao unachukuliwa pasi na haki, wanawake wanabakwa, na kuibiwa mali zao. Haya yote yanatokea mbele ya watu walioko madarakani na wale wanaopambana nao. Hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu katika kuamiliana nao, kwa sababu hamu yao sio mambo ya watu, maisha yao, na mali zao, bali hamu yao pekee ni kiti cha enzi (viti vya madaraka) na maslahi yao wenyewe!
Zaidi ya hayo, chini ya utawala wa Khilafah ya Kiislamu, wizi wa mali na rasilimali za Umma wa Kiislamu na uwasilishaji wake kwenye sahani ya dhahabu kwa Magharibi kafiri ni haramu kabisa. Kwa hiyo, Khalifa anazilinda na kuzitumia katika njia zilizowekwa na sheria ya Kiislamu, na humshambulia kwa mkono wa chuma yeyote anayesubutu kuwa na ulafi au kutaka kuzichukua!
Kadhalika, chini ya utawala wa Kiislamu, dola huhifadhi umoja wa nchi, huzuia kusambaratika na mgawanyiko wake, na hutangaza jihad inapobidi ili kuhifadhi umoja wa Waislamu na kuulinda kutokana na mifarakano yoyote. Khilafah pekee, katika zama zote, ndiyo iliyoweza kuwaunganisha Wafursi, Waarabu, Wabarbera, Waturuki, wasiokuwa Waarabu, na watu wengine bila ya utofauti huu wa kikabila na kidini kuwa na athari yoyote mbaya katika kuishi kwao pamoja. Bali, wote waliyeyushwa ndani ya kinu cha Uislamu mtukufu.
Khilafah ilimdhaminia kila mtu mahitaji yake ya kimsingi na hata ya ziada kwa kadri ya uwezo wake. Khalifa alitumia rasilimali katika kusimamia mambo ya Ummah na kuhudumia maslahi yake, ili watu waweze kuishi kwa neema, ustawi, baraka, na kutosheka. Ibn Khaldun alitaja katika utangulizi wake kwamba kiasi kilicholetwa kwenye hazina ya Waislamu jijini Baghdad wakati wa utawala wa Khalifa wa Abbasiya Al-Ma'mun ni sawa leo na dolari bilioni 70 na tani 1,700 za dhahabu!! Mwenyezi Mungu amrehemu Khalifa Muadilifu Omar ibn Abdul Aziz, ambaye hakupatikana masikini hata mmoja katika Khilafah yake anayestahiki Zaka!
Ni nani kati yetu anaweza kusahau kwamba Sudan, ambayo watu wake wanateseka kwa njaa hivi sasa, chini ya Uislamu, ilikuwa kapu la chakula cha Waislamu wote!!
Hukmu zote za Uislamu ni nzuri, na utabikishaji wake sahihi unahakikisha maisha yenye staha. Kwa mfano, kwa kutabikisha hukmu za mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, riba, ukiritimba, ukosefu wa ajira, upendeleo, na ulaghai vitatoweka, na kila mtu atapata haki yake katika kazi na nyadhifa.
Kwa kutabikisha mfumo wa elimu ya Kiislamu, elimu katika ngazi zote itapatikana tena kwa kila mtu, sio tu kwa matajiri na wenye nguvu. Dola itakuwa na ukuu wa kisayansi na kiteknolojia unaohitajika kwa viwanda vizito, zana za kisasa za vita, na juhudi zengine kama hizo. Hakika dola ya Kiislamu itaregesha tena uongozi katika teknolojia na sayansi, kama ilivyokuwa huko nyuma, pale wafalme wa Ulaya walipopeleka watoto wao kusoma katika vyuo vikuu vya Kiislamu ili kukuuza maendeleo na ustawi wao!
Kwa kutabikisha sheria za mfumo wa kijamii, utovu wa adabu na uasherati vitaharamishwa, na heshima ya wanawake wa Kiislamu italindwa, hata kama itahitajika kuhamasisha majeshi, kama alivyofanya al-Mu’tasim pale mwanamke mmoja wa Kiislamu alipopaza sauti: “Ewe Mu’tasim!!
Kwa kumalizia, Khilafah inaangalia kikweli maslahi ya watu na ni mlinzi wa haki na mahitaji yao. Kwa hiyo, Ibn al-Qayyim al-Jawziyya, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Msingi na shina la Shariah umeegemezwa juu ya utawala na maslahi ya waja katika maisha ya dunia na Akhera, yote ni adilifu, yenye rahma, yenye kutimiza maslahi, na hekima. Kila suala linalokengeuka kwenye uadilifu kwenda kwenye dhulma, kutoka kwenye rahma kwenda kinyume chake, kutoka kwenye maslahi kwenda kwenye ufisadi, na kutoka kwenye hekima kwenda kwenye upuzi, haitokamani na Shariah. Shariah ni uadilifu wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake, na rehema yake katika viumbe vyake, na kivuli chake katika ardhi yake.” (I’lam al-Muwaqqi’in ‘an Rabb al-’Alamin)
Inajulikana vyema kwamba wakati Waislamu wote walipoifuata njia ya Uislamu, kama dola na kama watu binafsi, walikuwa watu wa kwanza katika hadhara, ufanisi, maendeleo na maarifa. Waliishi maisha ya starehe na walikuwa mwenge wa nuru na haki kwa walimwengu. Kwa hiyo, Sudan na nchi zote za Kiislamu hazitasuluhishwa isipokuwa kwa yale zilizosuluhisha kwayo hali zao huko nyuma, na hali ya kusikitisha huko haitabadilika isipokuwa kwa kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu, ambayo inakomesha dhulma, inalipiza kisasi kwa waliodhulumiwa kutoka kwa madhalimu, kuzichukua haki kutoka kwa wale wanaokataa kuzitoa na kuwapa wale wanaostahiki.
أزمة_السودان# #SudanCrisis
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Minnatullah Tahir