- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Trump na Putin: Kutoka Mapenzi hadi Chuki ni Hatua Moja tu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Putin amemtishia Trump kwa “kuvunja mahusiano” endapo Ukraine itapokea makombora ya Tomahawk kutoka Marekani. (nv.ua)
Maoni:
Katika wiki mbili zilizopita, tumeshuhudia msururu wa ripoti za habari zinazoonyesha mabadiliko katika sera ya sasa ya utawala wa Marekani kuelekea Urusi na uvamizi wake nchini Ukraine.
Mnamo Septemba 23, Trump alitangaza ghafla: “Ninaamini kwamba Ukraine, kwa msaada wa Muungano wa Ulaya, ina uwezo wa kupigana na kushinda, kuregesha Ukraine yote kwenye mipaka yake ya awali.”
Siku hiyo hiyo, alisema pia: “Ukraine haiwezi tu kuregesha maeneo yake yote bali hata kwenda mbali zaidi.” “Urusi haionekani kuwa ya kuvutia. Kwao, hili lilipaswa kuwa la haraka. Inaonekana kana kwamba vita bado havijakwisha.”
Mnamo Septemba 26, alisema: “Uchumi wa Urusi utaenda kuzimu. Wanalipua kila kitu kinachoonekana na kuteka maeneo machache sana, ikiwa yapo. Kwa kweli, wanayapoteza baadhi yake.”
Mnamo Septemba 29, Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Ukraine Keith Kellogg alitangaza kwamba Trump ameidhinisha Ukraine kufanya mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya Urusi.
Mnamo Oktoba 2, ripoti ziliibuka kuwa Trump alitia saini agizo la kuidhinisha Pentagon na asasi za kijasusi kuisaidia Ukraine kwa mashambulizi kama hiyo.
Kwa mara ya kwanza, utawala wa Trump utasaidia Ukraine na mashambulizi ya masafa marefu. Marekani imewataka washirika wa NATO kutoa usaidizi mithili ya huo kwa Ukraine. Uwezekano wa kuipatia Ukraine makombora ya Tomahawk na Barracuda unazingatiwa.
Kwa kuzingatia habari hii, inaweza kudhaniwa kuwa Urusi imekataa masharti yaliyopendekezwa na Marekani ya kutatua mgogoro wa Ukraine.
Kama inavyojulikana, kwa miezi mingi kabla ya mkutano kati ya marais wa Marekani na Urusi huko Alaska, Urusi ilikuwa imesisitiza kama hali mbaya kwamba Ukraine itambue Crimea na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukraine kama Urusi. Inaonekana kwamba Urusi, baada ya kujifunza kutokana na uzoefu wa uchungu wa makubaliano ya Minsk, inaelewa kikamilifu kwamba “mgogoro mwengine uliohifadhiwa” kwa badali ya makubaliano kwa Marekani itakuwa kama kung’atwa tena na nyoka yule yule.
Huko nyuma mwaka wa 2015, Urusi – ikiamini kwamba Marekani inaahidi kupuuza uvamizi wake dhidi ya Ukraine – iliingilia kati mzozo wa Syria kwa niaba ya kibaraka wa Marekani Bashar al-Assad. Hili lilipelekea kurefushwa kwa utawala wa Assad nchini Syria, kwani Marekani ilikuwa bado haijapata mtu anayefaa kuchukua nafasi yake.
Mnamo 2022, wakati Urusi ilipogundua kuwa hakuna mtu aliyekusudia kutambua udhibiti wake juu ya Crimea iliyochukuliwa na kuikalia Donbas, ilizindua uvamizi kamili wa Ukraine.
Kufikia mwishoni mwa 2024, utawala wa Assad ulikuwa umechoka na nafasi yake ikachukuliwa na Ahmad al-Sharaa anayeungwa mkono na Uturuki. Urusi, kwa kutambua kuwa imetumika, ilifukuzwa kutoka Syria.
Tangu wakati huo, Urusi inaelewa kuwa makubaliano yoyote au kugandisha mzozo wa Ukraine itakuwa ni kujiua. Ndiyo maana inasisitiza kwa uthabiti kwamba udhibiti wake juu ya Crimea na Donbas utambulike.
Ama kuhusu msimamo wa mazungumzo ya Amerika juu ya Ukraine, unapanuka zaidi ya mgogoro wa sasa. Kimsingi, Marekani inatumia mzozo wa Ukraine kulazimisha Urusi kushirikiana katika kuikabili China.
Leo, China imezungukwa pande tatu na washirika wa Marekani, muhimu zaidi kati yao ni Japan, Korea Kusini, India na Pakistan, pamoja na dola zengine za kikanda.
Muungano unaowezekana kati ya Urusi na China ungeruhusu China kujinasua kutoka katika mazingira haya na kupata mwanya wa ufikiaji wa maliasili nyingi za Urusi – kutoa msukumo mkubwa kwa nguvu za kijeshi na kiuchumi za China.
Ama kuhusu msimamo wa China, inabakia kuwa muangalifu – haiko tayari kuunga mkono kikamilifu Urusi kwa gharama ya mahusiano yake mkubwa ya kibiashara na Marekani na EU.
Ni muhimu kutaja kuwa Marekani inataka kuwacha mlango wazi kidogo – haitafuti azimio kamili la mzozo wa Ukraine, kwani Urusi iliyojiingiza katika uvamizi wake itakuwa wazi zaidi.
Utatuzi kamili wa mzozo wa Ukraine badala ya hatua za pamoja dhidi ya China ungeruhusu Urusi, wakati wowote, kuachana na Magharibi na kuikumbatia China.
Kwa upande mwingine, majeraha mapya ya Urusi baada ya kufukuzwa kwake kwa fedheha kutoka Syria yanaikumbusha kwamba kukubaliana na mpangilio mwingine wa “Mtindo wa Minsk” itakuwa kama kukanyaga reki moja mara mbili.
Kwa hivyo, haikushangaza wakati Trump, mara baada ya mazungumzo, alisema: “Sasa inategemea sana Rais Zelensky kumaliza kazi.”
Ni muhimu kutaja kuwa huyu ndiye Trump ambaye, mnamo 28 Februari 2025, alimkemea Rais Zelensky katika Afisi ya Oval, akidai kwamba hakuwa na hoja za kweli na alikuwa akitegemea kikamilifu mahitaji ya silaha za Amerika.
Ukraine, kwa upande wake, ilitabiri kukataa masharti ya Urusi kutambua Crimea na Donbas kama eneo la Urusi.
Mnamo 15 Septemba 2025, Waziri wa Fedha wa Ukraine Serhiy Marchenko alikiri kimsingi kwamba mazungumzo ya amani yamefeli, akisema: “Tunahitaji kuandaa jeshi na watu kwa mwaka mwingine wa vita – itahitaji pesa zaidi.”
Mnamo 19 Septemba Katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa la Ukraine Rustem Umerov, mpatanishi mkuu wa nchi hiyo, alisema: “Kwa sasa Ukraine haifanyi mazungumzo na Urusi kumaliza vita.”
Siku chache tu baadaye, kuanzia 23 Septemba, Rais Trump alibadilisha kwa kiasi kikubwa cha kauli yake kuhusu Urusi na uvamizi wake nchini Ukraine.
Kwa kumalizia, yapasa ieleweke kwamba mgogoro wa Ukraine kwa mara nyingine tena unathibitisha kwamba mataifa—ubwana wao, rasilimali, maisha, na damu—yanasalia mateka katika mapambano kati ya dola kubwa.
Hata zile dola kubwa zinazojionyesha kuwa marafiki na watetezi wa mataifa yanayodhulumiwa, kwa hakika, ndio wachochezi wakuu wa migogoro na walengwa wakuu wa migogoro hiyo. Mazungumzo yote kuhusu haki ya mataifa ya kujitawala na kujitegemea, haki za binadamu, na kujali wanawake, wazee, na watoto si chochote zaidi ya uongo kwa siasa zao ovu.
Hali hii itaendelea hadi pale utawala wa kweli wa Mwenyezi Mungu utakaporegeshwa duniani—kwa umbo la Khilafah Rashida ya Pili kwa kufuata njia ya Utume—ambayo makusudio yake ya kweli yatakuwa ni ustawi wa wanadamu wote, sio kauli mbiu tupu.
[فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُؤُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيبًا]
“Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!’” [Qur’an 17:51]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazyl Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine