Alhamisi, 02 Rajab 1446 | 2025/01/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  25 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 066
M.  Ijumaa, 27 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ]

“Mayahudi Hawawi Radhi Nawe, Wala Wakristo, Mpaka Ufuate Mila Yao” [Al-Baqarah: 120]
(Imetafsiriwa)

Utawala mpya nchini Syria umetoa taarifa mtawalia kuhusu mfumo wa serikali ambayo wananuia kutekeleza baada ya dhalimu kutoroka. Ni wazi kuwa si mfumo aliouweka Mwenyezi Mungu (swt) bali ni mfumo wa kisekula unaotenganisha dini na maisha kwa kisingizio cha kuwapa watu uhuru wa kuchagua mfumo wa utawala. Wanawaruhusu waandamanaji wa kike wanaodai uhuru na kuvua hijab, huku wakiwateka nyara waandamanaji wasafi wanaodai kuachiliwa kwa jamaa zao wanaotaka kutabikishwa kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt)!

Fauka ya hayo, wanatangaza waziwazi kwamba wataliacha suala la kuchagua mfumo wa serikali kwa watu wakati wa kipindi cha mpito, kwa mujibu wa mfumo wa kikafiri wa kidemokrasia.

Yaliyo sahihi tu ndiyo ya kweli, na yaliyo haki ni kweli tu: neno la ukweli tunalolitangaza kama nasaha kwa kila Muislamu, kwa msingi wa kanuni ya kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwa kuzingatia haki ya uwajibikaji, tunalielekeza kwa utawala mpya wa Syria na wale wanaousimamia, kwa majina na sifa zao, mmoja mmoja, kwa sababu hesabu ya Siku ya Kiyama ni ya watu binafsi binafsi.

Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْداً] “Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake.” [Maryam: 95].

Yeye (swt) asema:

[وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَى كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاء ظُهُورِكُمْ وَمَا نَرَى مَعَكُمْ شُفَعَاءكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاء لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ]

“Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.” [Al-An’am: 94]. Basi hebu kila mmoja wenu na ajue kwamba atasimama peke yake mbele ya Al-Jabbar (Mlazimishaji), na hebu na aitafakari Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ اللهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ...»

“Kila mmoja wenu atazungumza na Mola wake (Rabb) bila ya mkalimani baina yao. Atatazama upande wake wa kulia na ataona tu matendo aliyoyafanya hapo awali; atatazama kushotoni kwake na ataona yale aliyoyafanya hapo awali, na atatazama mbele yake na hataona ila Moto (wa Jahannam) mbele ya uso wake. Basi uogopeni Moto (wa Jahannam) ...” hebu kila mmoja wenu na akumbuke kisimamo hicho hatari, na ajihadhari na aibu na hasara ya milele iliyo dhahiri.

Ikiwa hajui, basi na ajue: kwamba Muislamu hana haki ya kuchagua mfumo wa utawala - awe ni mtawala au mtawaliwa - na dalili ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu (swt);

[وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالاً مُّبِيناً]

“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab: 36].

Mtawala lazima ahukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na watawaliwa lazima wahukumiwe kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’idah:49]. Hotuba kwa Mtume (saw) ni hotuba kwa Ummah wake, kama inavyojulikana katika kanuni za fiqh (al-usul).

Imeharamishwa kwa mtawala wa Kiislamu kuhukumu kinyume na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na mwenye kufanya hivyo kwa yakini amekufuru. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ] “Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [[Al-Ma’idah: 44]. Yeyote anayehukumu kwa yasiyokuwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, pasi na kuyaamini, yeye ni dhalimu na fasiki. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أنزَلَ اللهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ] “Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Ma’idah: 45]. Na Yeye (swt) asema:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ] “Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” [Al-Ma’idah: 47]. Mwenyezi Mungu (swt) amekanusha imani kutoka kwa wale wasioshikamana na Shariah yake akisema:

[فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجاً مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيماً]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” [An-Nisa:65]. Kutawala na kukimbilia sheria kinyume na Sheria ya Mwenyezi Mungu ni kukimbilia kwenye taghut (batili) ambayo tumeamrishwa kuikufurisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيداً]

“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali” [An-Nisa: 60].

Tunakuonyeni kwa dhati na kwa uaminifu dhidi ya matokeo ya kuifurahisha Marekani au wengine wasioheshimu ahadi wa udugu na nyinyi, Uislamu, au Waislamu. Jueni kwamba wao hawatokuwa radhi nanyi mpaka mufuate ukafiri wao, na kwa kuwaridhia munafuata matamanio yao, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu wa Mkweli (swt):

[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Al-Baqarah: 120]. Kuweni na yakini kwamba mkijaribu kuwaridhia kwa kuiacha hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na mkatawala kwa mifumo yao ya Kikafiri iliyotungwa na wanadamu, basi watakutumieni kwa maslahi yao, na kuupiga vita Uislamu, Waislamu, Khilafah, na wale wanaoifanyia kazi. Kisha watakukataeni kabisa kama walivyo wakataa walio kuwa kabla yenu. Na nyinyi mnalo funzo na onyo kutoka kwa waliokuja kabla yenu, kama vile Bashar, Mubarak, Gaddafi, Ali Saleh na Ben Ali. Hawakuwajali wao, watu wao hawakuwahurumia na pesa zao hazikuwanufaisha, wala kuwaridhia kwao mabwana zao. Hawakuzingatia Akhera yao kwa hivyo walidhalilishwa hapa duniani na kesho Akhera, basi zingatieni enyi wenye akili!

Kutoa visingizio kama vile haki za watu wachache wa makabila mbalimbali au haki za wanawake (kwa kutokutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu) haikubaliki, kwani hakuna aliyewapa haki kama zile ambazo Uislamu umewapa, na hakuna yeyote aliyehifadhi haki zao kwa ajili yao kama Waislamu walivyozihifadhi, na historia ya Khilafah ni shahidi bora wa hilo, kama ilivyotolewa ushuhuda na adui mbele ya rafiki. Wasiokuwa Waislamu waliishi chini ya utawala wa Uislamu kwa karne nyingi, na walifurahia haki chini ya utawala wa Uislamu ambazo hata hawakuziota usingizini; hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) aliteremsha Shariah yake kwa watu wote, si Waislamu tu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللهُ وَلاَ تَكُن لِّلْخَآئِنِينَ خَصِيماً]

“Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini.” [An-Nisa: 105].

Na hivi ndivyo Waislamu walivyoendelea katika historia yote ya utawala wa Kiislamu, kuanzia zama za Utume na kuishia na Uthmani Khilafah.

Utekelezaji huu uliakisiwa kwa wasiokuwa Waislamu kwa kuridhika na kuhakikishiwa. Hivyo musifuate maamrisho ya Magharibi, musije mukawa miongoni mwa waliokhasirika... katika watawala waliowafuata kuna funzo kwenu.

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37].

Ewe Mwenyezi Mungu, tumefikisha ujumbe, Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa shahidi wetu.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu