Jumatano, 23 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  20 Rabi' II 1447 Na: 1447/04
M.  Jumapili, 12 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Janga la Gabes, Mhasiriwa wa Machaguo ya Dola ya Kisasa
(Imetafsiriwa)

[وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ]

“Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” [Al-Baqara:205]

Maandamano ya watu wa Gabes kusini mwa Tunisia yanaendelea kwa sababu ya sumu inayotolewa kutoka kwa tata ya kemikali, ambayo imegeuza jiji hilo kuwa eneo lililoathirika kimazingira na kiafya, na kuathiri moja kwa moja afya ya wakaazi wa Gabes na mali asili yake. Saratani na magonjwa ya kupumua yameenea, na suala hilo limefikia hata visa vya kukosa hewa miongoni mwa wanafunzi. Miongo kadhaa ya ahadi za uongo na kupuuzwa kwa makusudi kumeifanya Gabes kuwa ishara ya kutengwa na uchafuzi wa mazingira, kwani utajiri wa phosphate umegeuka kutoka kuwa baraka hadi laana kwa sababu ya sera za serikali ya kisasa, ambayo ilichagua faida ya haraka na maslahi ya makampuni makubwa kwa gharama ya afya ya watu na haki yao ya maisha bora.

Enyi Watu wa mji mzuri wa Gabes: Mji wenu, chini ya utawala wa Uislamu, wakati wa Khilafah ya Kiislamu, ulikuwa ni chemchemi nzuri ambapo maisha yalikuwa ya kupendeza na yenye uchangamfu. Umegeuka chini ya mfumo mchafu wa kibepari kuwa mji ulioshambuliwa na mandhari ya kukosa hewa na kifo cha polepole. Basi msingojee ufumbuzi wa matatizo yenu kutoka kwa walioyasababisha, na chukueni hatua ya kuyatatua wenyewe, kwa kuregea katika njia ya Mola wenu Mlezi, na kufanya kazi ya kuubomoa mfumo wa kibepari aliolazimishwa na adui yenu juu yenu, na kuusimamisha mfumo wa Uislamu, unaoziunganisha ardhi za Waislamu katika dola moja yenye nguvu inayowachunga kwa sheria ya Mola wao Mlezi, ambaye amafafanua kwa kina yale ambayo ni milki ya dola na wajibu wake kwake, na yale ambayo ni ya raia na wajibu wao kwake, kwani ameufanya ufisadi katika ardhi kuwa ni uhalifu unaochukiza. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ]

“Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” [Al-Baqara:205]. Na Mtume Wake (saw) amekaharamisha mtu kujidhuru nafsi yake au kuwadhuru wengine. Yeye (saw) amesema: «لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ» Pasiwe na kudhuru wala kudhuriwa.” Na akasema (saw):

«لا يَبولَنَّ أحَدُكُمْ في الْمَاءِ الدَّائِمِ الذي لا يَجْرِي، ثُمَّ يَغْتَسِلُ فِيه»

“Asikojoe mmoja wenu katika maji yaliyotuama yasiyotiririka, kisha akaoga humo.” Na kanuni ya kisheria ya Kiislamu ni kwamba “njia ya inayopelekea kwenye haramu ni haramu.” Kwa hiyo, kuchafua mazingira kwa njia ya madhara, au kwa njia inayopelekea madhara, au kupelekea haramu wakati wa mchakato wa utengenezaji, maendeleo ya kiuchumi, na utumizi mbaya wa maliasili, ni haramu kiSharia, bila kujali gharama zinazotokana na kuepuka kufanya hiyo.

Enyi Watu wa mji mzuri wa Gabes: Tatizo la kimazingira haliwezi kutatuliwa kupitia masuluhisho ya kibepari ambayo yanapima mambo yote kwa manufaa na faida. Hakuna kitakachozuia ubadhirifu wa makampuni ya kibepari ambayo yameharibu mazao na wanyama isipokuwa utawala wa Uislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«فَالإِمَامُ رَاعٍ وهو مَسْؤُولٌ عن رَعِيَّتِهِ»

Imam ni mchungaji na atahisabiwa kwa raia wake.” Tiba ya tatizo hili katika Dola ya Kiislamu itakuwa ni kutenga maeneo ya viwanda yaliyo mbali na maeneo ya makaazi kwa viwanda vya uchafuzi wa mazingira, kufuatilia vituo vya viwanda na kilimo na vyanzo vyengine vyote vya uchafuzi wa mazingira, na kuvilazimu vituo na vyanzo hivi kufuata mbinu na mifumo safi ya uzalishaji, kama vile vitengo vya kutibu taka za viwandani, na kutoruhusu uchafuzi kuvuja kwenye mazingira yanayozunguka.

Dola ya Khilafah pia inatilia maanani kuanzisha viwanda vya kuchakata tena taka zinazoruhusiwa za viwandani na kuzitumia tena kama aina mpya za mada na nishati, ambayo inaitwa kuregesha tena matumizi, ili kupunguza kiasi cha taka za viwandani. Kinachobaki cha taka hizi ambacho hakiwezi kutumiwa au kuchakatwa tena kinatupwa kwa kuzikwa katika maeneo ya mbali.

Maandamano ya watu mashujaa wa Gabes lazima yawe nukta kianzilishi kuuangusha mfumo katili wa kibepari na kusimamisha utawala wa muongofu kwa msingi wa Uislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu