Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 19 Rabi' II 1447 | Na: H 1447 / 016 |
M. Jumamosi, 11 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji na Njaa ya Watoto wa Gaza Havitakwisha Kupitia Mipango ya Wale Waliohusika na Mauaji ya Halaiki Bali Kupitia Uhamasishaji wa Majeshi ya Waislamu Pekee
(Imetafsiriwa)
Katika kipindi cha miaka 2 iliyopita, watu wa Gaza wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya mabomu, mzingiro wa kikatili na jinai za kutisha zaidi za umbile la mauaji la Kiyahudi, ambapo wanawake na watoto wamekuwa wahanga wakuu. 65,000 wameuwawa, wakiwemo zaidi ya watoto 20,000 – sawa na watoto 30 wanaouawa kila siku. Watoto wamepigwa risasi kimakusudi na wavamizi wa Kiyahudi au mashambulizi ya droni barabarani, au hata wanapotafuta chakula kwenye vituo vya misaada ambavyo vimekuwa ‘mitego ya kifo’ kwa wanaokabiliwa na njaa. Kulingana na ‘Save the Children’, watoto waliuawa au kujeruhiwa katika zaidi ya nusu ya mashambulizi mabaya katika maeneo ya usambazaji wa chakula mjini Gaza ndani ya wiki nne baada ya Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza kuanza shughuli zake. Mashambulizi yasiyokoma ya vikosi vya Kiyahudi pia yamesababisha zaidi ya watoto 21,000 walemavu – Gaza sasa imekuwa nyumbani kwa idadi kubwa zaidi ya watoto waliokatwa miguu kwa kila mtu kuliko mahali pengine popote duniani. Kwa mujibu wa UNICEF, mgogoro wa utapiamlo Gaza umefikia viwango vya janga, na ongezeko la 500% la watoto wenye utapiamlo tangu mwanzo wa mwaka, na idadi yote ya watoto chini ya miaka mitano – zaidi ya watoto 320,000 – wakiwa katika hatari ya utapiamlo mkali, na zaidi ya watoto 150 wameangamia kutokana na njaa.
Na bado, serikali hizo hizo za kikoloni za Magharibi ambazo zilihusika katika mauaji haya ya halaiki kupitia ufadhili wao, silaha na uungaji mkono wa umbile la Kiyahudi, zinawasilisha mipango yao kwa mustakabali wa Gaza, kana kwamba ni ‘waleta amani’, wakiwaamuru Wapalestina jinsi ya kutawala ardhi yao, kana kwamba ni ya dola hizi za kikoloni! Hakika Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـكِن لاَّ يَشْعُرُونَ]
“Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.” [Al-Baqarah: 11-12]. Iwe ni Mpango wa Trump unaotaka kuunda aina mpya ya ukaliaji kimabavu mjini Gaza, kuikabidhi kwa Amerika, au iwe ni utambuzi wa dola ya Palestina isiyo na maana, ya udanganyifu wa Uingereza, Ufaransa, na dola zengine za Magharibi ndani ya ‘suluhisho la dola mbili’ - mipango hii inalenga tu kutoa njia ya hai kwa umbile la Kiyahudi ili kulihifadhi, kulilinda na kuliimarisha, kutotoa chochote kwa Wapalestina! Je, ni kheri gani inayoweza kuja kutoka kwa wale waliosaidia kuasisi umbile la Kiyahudi, na kulilea, na kutumika kama muungaji mkono na ngao kwa uhalifu wake? Mipango yao inatoa nini isipokuwa hisia ya uongo ya afueni hadi umwagaji damu utakaporegea?!!
Zaidi ya hayo, ni wazi wazi kwamba umbile la Kiyahudi halitamaliza vita vyake vya kuwaangamiza Wapalestina hadi lifikie lengo lake kuu la kuasisi ‘Israeli Kubwa Zaidi.’ Kwa hiyo, hakutakuwa na mwisho wa mauaji haya ya halaiki na kurudiwa tena kwa Naqba hadi ukaliaji huo wa kimabavu utakapong’olewa kutoka katika kila shubiri ya Palestina. Hili litafikiwa tu kwa kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu (swt) amewajibisha kuwalinda Waislamu na kukomboa ardhi zetu.
Kwa hiyo, tunawaambia ndugu zetu katika majeshi ya Waislamu… ni nini mnachosubiri kabla ya kuitikia Amri ya Mola wenu Mlezi ya kuulinda Ummah wenu na kuuondolea saratani ya uvamizi huu milele? Mutampa udhuru gani kwa Mola wenu Mlezi kwa kushindwa kuwatetea Waislamu na utakatifu wa Al Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa? Ni juu yenu nyinyi pekee kukabiliana na umbile la Kiyahudi na kuikomboa ardhi ya al Isra wal Miraj. Kwa hivyo, chukueni hatua sasa kuwaondoa watawala hawa wasaliti ambao wanatumika kama ulinzi wa mstari wa mbele wa uvamizi huo, na ambao sasa wanafurahia mpango muovu wa Trump; simamisheni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume mara moja ambayo pekee ndiyo yenye uwezo wa kukomesha mauaji haya ya halaiki dhidi ya Ummah wenu kwa milele! Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa: 75].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-uttahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-uttahrir.info |