Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 21 Rabi' II 1447 | Na: Afg. 1447 H / 06 |
M. Jumatatu, 13 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mapigano ya Hivi Karibuni Kati ya Afghanistan na Pakistan Yanatumikia Maslahi ya Sera za Kieneo za Marekani na India
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumamosi usiku, vikosi vya jeshi la Afghanistan na Pakistan vilishiriki katika mapigano ya mpakani, wakishambuliana nafasi za kila mmoja kwenye Mstari wa Durand; matokeo yake, pande zote mbili za Waislamu zilipata hasara. Siku mbili kabla ya hapo, jeshi la Pakistan lilikuwa limeshambulia kwa mabomu maeneo fulani katika miji ya Kabul na Paktika, na kusababisha hasara zake zenyewe.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan imelaani vita vinavyoendelea kati ya ardhi hizi mbili za Kiislamu na kuviona kuwa vinatumikia sera za kieneo za Marekani na India na kuwadhuru Waislamu. Mzozo huo kwa mara nyingine unaonyesha jinsi mipaka bandia na siasa zisizo za Kiislamu zilivyowaweka Waislamu dhidi ya wao kwa wao, huku maadui halisi wa Umma wakitazama hali hiyo wakiwa katika sehemu ya usalama kamili.
Inasikitisha sana kwamba jeshi la Pakistan – ambalo linajihesabu kuwa jeshi lenye silaha lenye nguvu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu – linatumia nguvu na silaha zake sio dhidi ya maadui wa Uislamu lakini dhidi ya Waislamu wenzao. Jeshi hilo hilo, lisilo na aibu liliacha kadhia ya Kashmir kwenda India na limekaa kimya mbele ya sera za chuki dhidi ya Uislamu na hatua za ukandamizaji za serikali ya Modi ya utaifa wa kibaniani, sasa inashambulia miji na vijiji vya Afghanistan na katika maeneo ya kikabila kwa ujasiri mkubwa huo, lau ujasiri huo na azma hiyo vingeonyeshwa dhidi ya India na dola ya Mayahudi, Kashmir haingelala katika udhalilifu, Gaza hangevumilia miaka miwili ya mzingiro na mauwaji makubwa, na leo hii suluhisho la aibu la amani lisingelazimishwa juu ya watu wa Gaza chini ya shinikizo na usaliti wa baadhi ya watawala wa Kiarabu na Pakistan.
Tunajua kwamba mtindo huu wa uadui dhidi ya Waislamu na kunyamaza mbele ya ukafiri ni kazi ya duara maalum, ya mamluki ndani ya jeshi la Pakistan, na kwamba ujasiri huu unatokana na ukaribu wa muda wa uongozi wa Pakistan kwa bwana wao, Donald Trump. Ukaribu huo umelipa jeshi la Pakistan udanganyifu na ujasiri wa kufanya mashambulizi nchini Afghanistan, na Marekani imefafanua dori kwa jeshi la Pakistan kuwafanya Waislamu wake wenyewe katika maeneo ya kikabila na kando ya Mstari wa Durand kukabiliana na kujishughulisha na mujahidina wa Afghanistan.
Kama ilivyotokea hivi karibuni, na kama adhabu ya muda kwa India, Marekani kwa mara nyingine tena inajifanya kuwa Pakistan ni mshirika muhimu; Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan unajishughulisha na usafiri, kupiga picha na ishara za kuwafurahisha maafisa wa Marekani. Ilhali upepo unapobadilika, Pakistan inatupwa tena kwenye kona ya usahaulifu. Kama vile Khawaja Muhammad Asif, waziri wa ulinzi wa Pakistan, alivyokiri wakati mmoja: “Tumekuwa tukifanya kazi hii chafu kwa ajili ya Marekani kwa takriban miongo mitatu ... na Magharibi, ikiwemo Uingereza. Hilo lilikuwa kosa na tumeteseka kwa hilo.”
Kukiri huku kunaonyesha kwamba miongo kadhaa ya sera ya Pakistan ilitumikia maslahi ya Marekani na kuwebebesha gharama kubwa Waislamu wa eneo hili. Matukio ya hivi majuzi pia yanaonyesha kuwa Pakistan haijajifunza kutoka kwa historia na kwa mara nyingine inafadhilisha kuregeshwa kwa Marekani katika eneo hili. Uhalisia ni kwamba Marekani huikumbuka Pakistan isipokuwa pale tu inapofikia mkwamo katika sera zake kuelekea Afghanistan, India, au China. Wakati huo Pakistan ghafla inakuwa “mshirika wa kimkakati” na dori yake ya muda inaamshwa. Lakini mara baada ya misheni kumalizika na sera ya Marekani katika eneo hilo kuregea katika hali yake ya kawaida, Pakistan inawekwa kando tena; Ahadi hizo zote na tabasamu za kidiplomasia – kama ilivyokuwa dhahiri wakati wa Biden – si chochote ila barakoa za muda tu.
Ujumbe wetu kwa mujahidina wa Afghanistan na kwa wanaume wenye ikhlasi ndani ya jeshi la Pakistan ni huu: badala ya kuwachinja Waislamu na kupigana wenyewe kwa wenyewe, tazameni picha kubwa zaidi. Kwa sasa matumaini ya Waislamu duniani kote – hasa katika Asia ya Kusini – yako juu ya uwezo wa kijeshi wa mujahidina wa Afghanistan na wale maafisa wanyoofu katika jeshi la Pakistan ambao wanauweka Uislamu na ahadi ya Pepo juu ya wadhifa na cheo cha kidunia. Majeshi haya yana uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa: kwa kuondoa mipaka bandia, ya kikoloni na kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili, yanaweza kuunganisha uwezo wa Ummah katika eneo zima na kuibuka kama nguzo huru ya kisiasa na kijeshi kwenye jukwaa la dunia. Kwa kweli, Khilafah kama hiyo ingezima miundo ya kikoloni ya Marekani, India, na China katika eneo hili na ingekusanya jeshi kukomboa ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu kama vile Kashmir, Turkestan Mashariki na Palestina.
[وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلاَ تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَاصْبِرُواْ إِنَّ اللّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ]
“Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” [Al-Anfal:46]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |