Mradi wa Reli wa China–Indonesia: Mkakati wa China Kuidhibiti Indonesia
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Indonesia inafikiria kujadili upya deni la mradi wa reli ya mwendo kasi wa Jakarta–Bandung, unaojulikana kama Whoosh, kutokana na mzigo mzito wa kifedha unaouweka kwa mwendeshaji wa reli ya serikali Kereta Api Indonesia (KAI). Waziri wa Biashara Zinazomilikiwa na Serikali Erick Thohir alisema mpango huo utaruhusu KAI kusimamia treni huku serikali ikisimamia miundombinu. Mradi huo wenye thamani ya dolari bilioni 7.3 ulifadhiliwa hasa kupitia mikopo kutoka Benki ya Maendeleo ya China, awali kwa riba ya asilimia 2. Hata hivyo, kukatizwa na maambukizi na masuala ya ardhi yalisukuma gharama zaidi, na kuhitaji ufadhili wa ziada kwa riba ya asilimia 3.4.