- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuweka Matumaini juu ya Kuvunjika kwa Safu za “Israel” ni Usaliti Mpya wa Gaza
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kura moja ya maoni ilifichua kuwa 56% ya “Waisraeli” wanaogopa kusafiri nje ya nchi, 67% wanaamini kuwa serikali haiwawakilishi na 62% wanaunga mkono makubaliano ya kina ya kusitisha mapigano kati ya umbile la Kiyahudi na Hamas, ikiwemo kuachiliwa huru kwa mateka. Tovuti ya “Zman Yisrael,” ambayo ilichapisha maelezo ya kura hiyo ya maoni mnamo tarehe 5 Septemba 2025, ilifafanua kuwa wengi wa “Waisraeli” walionyesha kutokuwa na uwezo wao wa kusafiri nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa ukosoaji wa kimataifa wa umbile lao pamoja na kutengwa kunakoendelea kwa kimataifa kwa dola yao na kuendelea kwa vita mjini Gaza. (AlJazeera)
Maoni:
Sambamba na umbile la Kiyahudi kuendelea kuongeza kampeni yake ya kihalifu ya mauaji ya halaiki, mauaji, na kuhamisha watu katika Ukingo wa Magharibi na Gaza, vyombo vya habari vya Kiarabu na rasmi katika ulimwengu wa Kiislamu vinaangazia habari kama hizi za kura ya maoni. Ambayo inaonyesha kana kwamba umbile la Kiyahudi linaporomoka kutoka ndani. Pia kile uvujaji wa hivi majuzi ulifichua kutoka kwa mkutano wa Waziri wa Elimu wa umbile la Kiyahudi, Yoav Kisch, na familia za mateka, ambao ulifichua kina cha kuvunjika na kuporomoka kindani kwa umbile la uvamizi, kwani waziri huyo alikiri wazi wazi kwamba serikali “imetengwa, na vita vinaendelea kwa njia hii kwa sababu “haina uwezo,” huku familia hizo zikimtuhumu kwa ujinga, utelekezaji, na kuhatarisha wapendwa wao kupitia sera zilizofeli. Channel 12 ya Kiebrania ilitangaza maungamo huu, ikifichua serikali iliyopooza, maamuzi yake yakifungika kwa kipote cha wachache, na kutengwa na jamii ya Kiyahudi na mazingira yake ya kimataifa.
Hakuna shaka kwamba migawanyiko na maandamano haya ndani ya umbile vamizi la Kiyahudi yanawakilisha udhaifu wa kweli katika muundo wake, ambao unaakisi mmomonyoko uliopatikana kwa jamii yao mchanganyiko, chini ya shinikizo la vita vya muda mrefu. Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba vyombo vya habari vya Kiarabu na visivyo vya Kiarabu na wanasiasa ambao wameiangusha Gaza, badala ya kubeba jukumu la kuwanusuru wanaodhulumiwa ndani yake, na kuyakusanya majeshi ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa na Al-Masjid Al-Aqsa al-Sharif kutokana na kunajisiwa na Mayahudi, waliichukulia migawanyiko hii kama karatasi ambayo waliweka juu yake matumaini yao ya kukomesha mashini hiyo ya mauaji. Wanaonyesha kuanguka kwa Netanyahu, au mtafaruku wa jeshi, au maandamano ya ndani kana kwamba ndio njia ya wokovu wa watu wa Gaza.
Kuegemea kama huko sio tu ni kukwepa faradhi ya Shariah, na kuhalalisha kufeli na khiyana, bali pia ni upotofu na kuzilaza ardhi za Kiislamu, ambazo zinawaka kwa hasira kwa zinazoshuhudia katika mateso wanayopata ndugu zake na dada zake, na ambazo zinaweza kuwanusuru, kama si kwa ajili ya khiyana ya watawala wa Waarabu na Waislamu, na kuwa kwao upande wa Mayahudi. Ummah unafahamu kwamba kadhia la Ardhi Iliyobarikiwa haijaamuliwa, na kamwe haitaamuliwa na migogoro ya siasa za Mayahudi, au mustakabali wa Netanyahu. Badala yake, dhati yake ni mapambano kati ya Umma na Magharibi, inayowakilishwa na uvamizi wake wa kikoloni katika moyo wa ardhi za Kiislamu: Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Watu wa Gaza na Palestina, kwa damu na uthabiti wao, ndio vinara wanaotengeneza mlingano wa kweli wa mzozo kati ya Umma na Mayahudi, na ulimwengu wa Kikruseda unaounga mkono umbile la Kiyahudi, na watu wa Gaza sio watazamaji tu wa mizozo ya ndani ya adui.
Kuweka matumaini juu ya kuvunjika kwa safu ndani ya umbile la Kiyahudi kunaonyesha, kiuhalisia, usaliti mwingine wa Gaza. Faradhi ya Shariah wa kuinusuru Gaza kwa uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu inabadilishwa na udanganyifu wa kuangamia kwa adui yeye mwenyewe. Wakati uhalisia uliothibitishwa ni kwamba uvamizi huo hautaanguka isipokuwa chini ya mashambulizi ya majeshi ya Waislamu, na sio kwa maandamano tu au migogoro ya kisiasa ya muda mfupi ndani ya umbile la Kiyahudi.
[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ * وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ وَيَتُوبُ اللَّهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ]
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini, Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba ya amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.” [At-Tawba:14]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan