Jumatano, 29 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  24 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 1446 / 13
M.  Ijumaa, 20 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umbile la Kiyahudi ni Panya Anayejifanya Kumiliki Nguvu ya Simba, Ubabe na Ujasiri wake unatokana na Watawala Wasaliti wa Waislamu

(Imetafsiriwa)

Alfajiri ya Ijumaa, 13/6/2025, umbile la Kiyahudi lilifanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Iran, yakilenga maeneo ya nyuklia na makao makuu ya kijeshi, na kusababisha vifo vya viongozi kadhaa wa kijeshi na usalama, pamoja na wanasayansi wa nyuklia.

Shambulizi hili linajiri wakati Iran imekuwa ikifanya mazungumzo na Marekani kwa muda wa miezi miwili kuhusu mpango wake wa nyuklia, na katika kivuli cha tishio linaloendelea kutoka kwa umbile la Kiyahudi. Ijapokuwa Iran haijachukua hatua zozote za tahadhari kulizuia umbile la Kiyahudi kufikia malengo yake na kutekeleza vitisho vyake!!

Iran ilipaswa kuchukua tahadhari baada ya udhalilifu na matusi iliyotendewa na umbile la Kiyahudi katika Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa. Ililenga chama chake nchini Lebanon, na kuharibu ngome zake na kuwaua viongozi wake mmoja baada ya mwengine. Walakini, Iran haikufanya chochote. Operesheni hii ilifuatiwa na kuilenga nchini Syria, na kuilazimisha, kwa udhalilifu, kutoka nje ya nchi hiyo, hadi ilipovamiwa nyumbani kwake yenyewe na kupata hatima hiyo hiyo na chama chake nchini Iran.

Iran ina chaguzi nyingi na uwezo wa hali ya juu. Sio shabaha rahisi, baada ya kufanikiwa kutoa mapigo yenye ufanisi kwa umbile la Kiyahudi. Hata hivyo, tatizo lake liko kwenye uongozi wake. Iwapo ungekuwa uongozi mwaminifu, ungetumia uwezo huu na kuchukua hatua ya kulishambilia umbile hilo na kuling'oa kutoka kwenye mizizi yake tangu kuanzishwa kwa Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa. Lakini haikufanya hivyo. Badala yake, iliiacha Gaza, Lebanon, na baadaye Yemen kuwa mawindo ya uhalifu wa Kiyahudi hadi ilipochelewa kabisa, na hakukuwa na wakati wa kujuta. Ilitosheka kuwa kibaraka katika mipango ya kafiri ya kulipandikiza umbile la Kiyahudi kama uhalisia ulioko ndani ya kitovu cha ardhi za Waislamu.

Enyi Waislamu: Kinachoujaza moyo masikitiko na maumivu ni uhalisia huu mchungu ambao Umma wa Kiislamu unapitia. Umbile hili vamizi, ambalo Mwenyezi Mungu ametia udhalilifu na ufukara kwa watu wake, limepanuka, linatishia, linafanya vurugu, kuua na kuwafukuza Waislamu. Badala yake, hatujaona mtu yeyote anayefanya kazi ya kuling'oa, licha ya utambuzi wetu na utambuzi wake kwamba ni umbile dhaifu na ni simba wa karatasi. Mayahudi ndio waoga zaidi katika viumbe vya Mwenyezi Mungu. Yeyote anayewaona leo baada ya kufichuliwa na majibu ya Iran na mashambulizi ya makombora yaliyolenga Tel Aviv na maeneo mengine, anatambua kikamilifu kiwango cha udhaifu wake. Hapa wanaiomba Marekani, wakiisihi na kujaribu kuilaghai ili kuiburuza vitani kwa kuingilia kati moja kwa moja ili kuwatoa kwenye kinamasi kipya ambamo wamejitumbukiza wenyewe, baada ya kutambua kutokuwa na uwezo wa kutatua vita.

Enyi Waislamu: Ujasiri wa umbile la Kiyahudi ni wa kirongo, Kafiri Magharibi imelivisha pamoja nao na linahifadhiwa na watawala wasaliti wa Waislamu, watawala vibaraka ambao wamekubali udhalilifu kwa badali ya kusalia madarakani. Miongoni mwa watawala hao ni watawala wa Iran, watawala ambao hawajaacha juhudi zozote katika kuwatumikia maadui wa Ummah hususan Marekani. Wamekuwa wakijidhalilisha kwa kafiri na kulipiza kisasi kwa waumini.

Enyi Waislamu: Enyi watu wenye nguvu na ulinzi: Jueni kwa yakini kwamba nyinyi hamna heshima wala hadhi na ikiwa mumetawaliwa na utawala wa Ruwaibidha (watawala wajinga wasio na maana), maadui wa Mwenyezi Mungu, Dini yake na waumini. Hakuna kitakachomdhalilisha adui yenu wala kuliondoa umbile hili vamizi linalonyakua ardhi na kuuwa watoto isipokuwa Khilafah, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wake (saw). Kwa kazi nzito na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir inawalingania, kuweni maanswari wa Mwenyezi Mungu, ili mpate kuvibomoa viti hivi dhaifu vya utawala na serikali fisadi, msimamishe Sharia ya Mwenyezi Mungu, muwakomboe waja na nchi, na wasahaulisheni maadui minong'ono ya Shetani. Nyinyi ni Umma wa kheri na uongofu, na mnastahiki hayo.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu