Jumamosi, 28 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taharuki Kati ya Ethiopia na Eritrea Inazifanya Kuwa Shabaha Rahisi kwa Dola za Kikoloni
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah - Toleo 565 - 17/09/2025 M
Na: Ustaadh Shabani Mwalimu*

Inaonekana kwamba mahasimu hao wawili wa muda mrefu, Ethiopia na Eritrea, wanaelekea kwenye vita, huku vitisho kati yao vikiongezeka na vikosi vinahamasishwa kwenye mpaka wao wa pamoja. Taharuki kati ya Ethiopia na Eritrea inachochewa zaidi na masuala matano:

Kwanza: Serikali ya kifederali ya Ethiopia na vikosi vya kikanda, haswa huko Tigray na Amhara, vinaichukulia Asmara kama tishio linalowezekana.

Pili: Ushindani wa kikanda, kwani Eritrea inahofia kutengwa kisiasa za kijografia katika Pembe ya Afrika, hasa kwa Ethiopia kuimarisha uhusiano wake na Somalia, Djibouti, na washirika wa kimataifa.

Tatu: Kukosekana kwa utulivu wa ndani nchini Ethiopia, kwani Eritrea inahofia kwamba mgawanyiko wa ndani nchini Ethiopia (machafuko ya Oromia, Amhara, na Tigray) huenda yakaenea.

Nne: Suala la Bahari Nyekundu: Ethiopia, nchi isiyo na bahari tangu uhuru wa Eritrea, imefufua matakwa yake ya kufikia bandari kwenye Bahari Nyekundu, ambayo Eritrea inaona kuwa tishio kwa ubwana wake.

Tano: Suala la mpaka: Ethiopia haijawahi kutilia maanani kuweka mipaka na Eritrea, kwani inaiona kuwa ni sehemu ya eneo lake na mojawapo ya majimbo yake yenyewe. Wakati uhuru wa Eritrea ulipotangazwa mwaka wa 1993, mipaka ya nchi hiyo mpya haikufafanuliwa. Isaias Afwerki alihofia kwamba Ethiopia ingeiunganisha tena nchi hiyo kwa kuchukua hatua za kijeshi kuweka mipaka, kinyume na mpango wa Marekani, na suala hili bado halijatatuliwa hadi leo.

Kupamba moto kwa hali ya sasa kunawezekana kunatokana na hisia inayokua kwamba mzozo mkali, kama sio vita vya kikanda, uko karibu. Katika mahojiano na vyombo vya habari vya serikali ya Eritrea Julai 19, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki aliituhumu Ethiopia kujiandaa na vita. Alielezea nia ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kupata njia ya ufikiaji wa bandari kwenye Bahari Nyekundu kama “mpango wa kichaa.” Getachew Reda, kiongozi wa kundi linalounga mkono serikali ya Ethiopia huko Tigray, alisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii mnamo Julai 21 kwamba chama cha Tigray People's Liberation Front kinajaribu kunyakua mamlaka kwa nguvu. Siku hiyo hiyo, wakati wa sherehe za kijeshi huko Jimma, kamanda wa Kikosi cha Ulinzi cha Kitaifa cha Ethiopia, Birhanu Jula, alionya kwamba Tigray iliyogawanyika inaelekea kwenye njia ya vita. Aliutuhumu Muungano wa Ukombozi wa Watu wa Tigray kukataa kushiriki katika mchakato wa kupokonya silaha, uondoaji hamasa, na ukarabati ulioainishwa katika Mkataba wa Pretoria wa 2022, ambao ulimaliza mzozo wa Tigray.

Mzozo unaoongezeka kati ya Eritrea na Ethiopia, unaoendelea kwa miongo kadhaa, unaingiliana na mgawanyiko wa wasiwasi kati ya vikundi katika eneo la Tigray. Baada ya miaka miwili ya mzozo kati ya watu wa Tigray na watu wa Eritrea, ripoti zilionyesha kwamba baadhi ya wanachama wa Tigray People’s Liberation Front na maafisa wa Asmara waliunda muungano mpya dhidi ya serikali ya kifederali ya Ethiopia.

Mnamo Machi mwaka huu, viashiria vya kuhisika vilijitokeza vya utayari wa Addis Ababa pamoja na Asmara kwa vita. Ripoti za kuaminika na zilizo na wasiwasi ziliibuka kuhusu uhamasishaji wa kijeshi katika pande zote za mpaka. Ethiopia imetuma idadi kubwa sana ya silaha nzito mpya na vitengo vya kiufundi katika eneo la Afar, karibu na mpaka wa Eritrea na umbali mfupi kutoka Assab.

Mvutano huu haupo huru na mambo mengine, lakini unachangiwa sana na ushiriki wa wahusika wa kimataifa na wa kikanda, kila mmoja akiwa na maslahi ya kimkakati, usalama, au kiuchumi katika Pembe ya Afrika. Ni muhimu kufahamu kwamba Ethiopia na Eritrea ni dola zinazoitii Amerika, na watawala wao ni vibaraka wake. Hii ina maana kwamba mivutano inayoongezeka kati ya wapinzani wawili wa muda mrefu iko kati ya vibaraka au “marafiki,” lakini inabaki chini ya rada ya kigeni. Amerika hutumia mazungumzo kusuluhisha tofauti zao.

Uhasama wa mara kwa mara katika Pembe ya Afrika unaifanya kuwa shabaha rahisi kwa dola za kikoloni, yaani Marekani na Ulaya, hasa Uingereza katika suala la ushawishi wa kisiasa, na China katika suala la ushawishi wa kiuchumi. Kwa kuwa eneo hilo, hususan Ethiopia, lina hifadhi kubwa ya mafuta katika maeneo mengi, hii imesukuma sera ya Marekani kuelekea maslahi zaidi katika Pembe ya Afrika, hasa kwa kuwa makampuni ya China yanacheza dori kubwa katika kuvinjari kiuchumi na uchimbaji wa mafuta ya Ethiopia.

Uingereza, kupitia Imarati (UAE), imejaribu kuiunganisha Ethiopia na mhimili na sera yake, ikitumai kuzishawishi Ethiopia na Eritrea. Bahari Nyekundu na Mkondo wa Suez ni njia muhimu kwa biashara ya kimataifa. Makadirio yanaonyesha kuwa takriban 10% ya biashara ya kimataifa hupitia njia hii, na Uingereza inaitegemea kupata mafuta, gesi na bidhaa kutoka Asia.

Inasikitisha kwamba Ethiopia na Eritrea ziko chini ya udhibiti wa dola za kikoloni Marekani, China, na Ulaya, na Waislamu hawazitilii maanani. Hakuna hata mmoja wa watawala wanaoungwa mkono na Magharibi anayeweza kusimama dhidi ya matamanio ya Marekani au Ulaya ya kuugawanya Umma. Kiongozi pekee mwenye uwezo wa kusimama dhidi ya ukoloni mamboleo ni Khalifa, kwani ameidhinishwa kuunganisha Umma wa Kiislamu chini ya mwongozo wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw).

* Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu