Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ghasia za Indonesia: Mabadiliko Ambayo (Bado) Yamefungwa?

(Imetafsiriwa)

Msiba wa Affan Kurniawan, dereva wa teksi ya pikipiki wa mtandaoni wa Indonesia aliyeuawa baada ya kugongwa na gari la polisi aina ya barracuda mnamo 28 Agosti 2025, uliishia katika msururu wa maandamano katika miji mingi kote Indonesia. Makala haya hayakusudii kujibu maswali, bali kuibua maswali kwa yeyote anayedai kuwa mwanaharakati wa Kiislamu.

Athari za Kutokuwa na Usawa katika Jiji la Jakarta

Kifo cha Affan Kurniawan kimeangazia tofauti za kimaisha jijini Jakarta, mojawapo ya miji mikubwa ya Kusini Mashariki mwa Asia. Affan aliyeacha shule ya upili, aliishi katika nyumba ya kukodi ya mita 3x11 na wanafamilia wake saba katika eneo linalojulikana kama eneo la “pesa za zamani”. Alikimu maisha kwa kutafuta riziki kama dereva wa teksi ya pikipiki mtandaoni, taaluma iliyo chini kabisa ya uchumi usio rasmi wa mijini, akiwakilisha tabaka la watu masikini wa mijini ambao wanaishi katika mtaa duni kati ya majengo makuu ya Jakarta na ya kupendeza.

Si hivyo tu, bali pia sura ya mama mwenye utaji wa waridi ambaye alipokea sifa kwa ujasiri wake wa kukabiliana na mamlaka katika maandamano mazito pia ilizingatiwa. Mama aliyevalia vazi la waridi alisimama kwa fahari mbele ya waandamanaji, akipiga kelele kwa laana za hasira kama kawaida za vitongoji vya Jakarta, huku akiwa amebeba mti wa bamboo wenye bendera nyekundu na nyeupe. Aliakisi kina mama maskini wa mijini ambao walitatizwa na maisha ya anasa ya maafisa wa DPR ambao walikuwa wakifurahia posho.

Uso usio wa kawaida wa Jakarta ni taswira ya jinsi maendeleo ya kibepari yalivyofanya kazi katika nchi hii kwa takriban miongo minane. Kinaya ni kwamba, katika miongo hiyo, Jakarta imekuwa kivutio cha ukuaji wa miji mara kwa mara, sababu kuu ya wanaotafuta kazi kutafuta riziki. Hata hivyo, tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mgawanyiko mkali zaidi wa kijamii hutokea katika Jakarta ya Kati na maeneo ya mijini yaliyostawi zaidi. Alama ya ubepari.

Moto hauwaki bila makaa. Kuna suala la kimfumo hapa, sio la sehemu tu. Mithili ya majani makavu yanayoweza kuwaka, mateso ya watu huwashwa kwa urahisi. Inahitaji tu msukumo kidogo tu kuwasha. Ongezeko la kodi ya majengo (PBB) kwa watu katika majimbo mbalimbali, kuachishwa kazi kwa wingi katika sekta ya viwanda, pamoja na utata wa ongezeko la posho kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (DPR), basi linachagizwa na maoni mbalimbali yasiyopata usikivu na ukosefu wa huruma kutoka kwa wajumbe wabinafsi wa Baraza la Wawakilishi, ambao wengi wao ni watu mashuhuri watepetevu. Boom!!! Inalipuka kama bomu la wakati.

Ufichuzi wa Ubinafsi wa Kipote cha Mabepari na Vuguvugu la Vijana

Dahlan Iskan, mwanahabari mkuu wa Indonesia, aliandika kwamba kulikuwa na kitu cha kipekee kuhusu muundo wa maandamano ya Agosti 25-28. Harakati ziliendelea bila amri, kwa miito mingi lakini hakuna taasisi, athari nyingi lakini hakuna waratibu. Makamanda walitolewa zaidi kutoka kwa mitandao ya kijamii. Mialiko ya maandamano ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii. Kupitia miito. Bila kutaja nani alitoa miito hiyo. Walimezwa tu. Waliosoma miito hawakuangalia ilitoka kwa nani. Labda walihisi inafaa tu—wakasukumwa kujiunga na maandamano. Walikusanyika katika mahali palipopangwa mapema. Kutoka hapo, walikwenda kwenye shabaha zao. Kutoka maandamano hadi hata uporaji wa nyumba za wabunge.

Kama mtafiti wa ANU Edward Aspinall alivyodai, maandamano ya hivi majuzi yanaweza kueleweka kama matokeo ya mgongano kati ya dunia mbili za siasa za Indonesia: uwakilishi rasmi wa ulimwengu wa kisiasa na utamaduni mdogo wa ubunifu wa vijana ambao wanapinga. Vuguvugu la maandamano ya vijana, lililochochewa na mitandao ya kijamii, linatokana na chuki kubwa dhidi ya kipote tawala cha Indonesia. Mitandao ya kijamii hupenya na kuunganisha mtandao unaokua wa mashirika legelege, pamoja na miunganisho kati ya taasisi zilizoimarika zaidi. Vuguvugu hili lina tofauti kifikra – lakini limeunganishwa na uzi wa pamoja wa upinzani dhidi ya kipote chenye udhibiti, hasira kwa ufisadi wa kipote cha watawala, na kupinga ongezeko linalokuwa la ukosefu wa usawa wa kiuchumi.

Harakati hii ya vijana ni hodari katika kusoma mchezo wa mamlaka wa kipote cha watawala, ambapo sio kila mtu ni mwerevu katika kugundua uchezaji wao wa kijanja. Kwa mtazamo wa kisiasa wa kipote hicho, ubaguzi wa vikundi upo bila shaka ndani ya utawala wa Prabowo. Misukosuko ya mpasuko na migogoro kati ya kambi za Prabowo na Jokowi (inayowakilishwa na Gibran kama makamu wa rais) imekuwa dhahiri katika miezi ya hivi karibuni. Dalili za kuongezeka kwa uhusiano kati ya Parcok na Parjo kwenye uwanja wa maandamano – zinaonyesha vita fiche vya misuli vinavyozidi, kipote cha watawala wakicheza pawn kwenye ubao wa chess, na Parcok na Parjo kama vitu vyao vya kucheza kwa ujanja, lakini watu huwa kando kila wakati na ni vitu tu vya kunyonywa. Mchezo wa kuweka masharti mashinani unazidi kupamba moto huku kambi moja ikijaribu kucheza na moto kwa kutumia hasira za wananchi, lakini inaanza kuteketea kwa moto ambao umewasha yenyewe.

Makundi ya mabepari na maslahi yao yanayoshindana yaligunduliwa kwa urahisi na vuguvugu la vijana, ambalo lilinusa uvundo wa kupeleka ishara ili kuunda mazingira ya uporaji wa ghasia, ambao kwa kweli haukutokana na matarajio ya watu wenyewe. Kwa hivyo, uharibifu wa sifa ya Baraza la Wawakilishi (DPR) na uaminifu wa Polisi wa Kitaifa wa Indonesia (Polri) uliacha kambi zote mbili zikiwa zimefungwa katika mzunguko mbaya, wakijaribu kila mara kufungiana nje. Wakati huo huo, vuguvugu la vijana, pamoja na madai yake ya 17 + 8, lilikosa suluhisho la kimfumo au mwelekeo wazi wa mabadiliko, likisalia kulenga mabadiliko ya kivipande na mageuzi ya kitaasisi ndani ya DPR, Polri, na TNI katika muundo wa kidemokrasia wa kisekula wa 'mazingira ya zamani'.

Swali ni je, hila zinazoingiliana za kipote cha mabepari, pamoja na msukumo wa ajenda ya 17+8 na vuguvugu la vijana, zinaweza kufungua milango ya mabadiliko kwa nchi hii? Au badala yake itarudi kwenye mzunguko ule ule wa mwaka 1998, yaani mabadiliko ya madaraka ya utawala bila ya mabadiliko ya mfumo wa maisha?

Kimsingi zaidi, kuna swali la kustaajabisha zaidi: katika nchi hii kubwa zaidi ya Kiislamu, ziko wapi sauti za wanaharakati wa Kiislamu? Ziko wapi sauti za vijana ambao kwa sauti kubwa walitetea Uislamu mpana kama suluhisho la kupinga? Wako wapi wahubiri waliosubutu kujadili kila nyanja ya mazungumzo ya umma, kama vile mageuzi ya polisi, siasa za uwakilishi, maendeleo ya kiuchumi, madini na hata siasa za mijini?

Ndio, wamenyamazishwa kwa muda mrefu na kipote kilichoko madarakani, lakini sasa ni wakati wa kujiuliza hivi kweli tumenyamazishwa au tumezoea kunyamazishwa?

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu