Jumatano, 25 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Rabi' I 1447 Na: 08 / 1447
M.  Jumatatu, 15 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mayahudi Wanachimba Makaburi kwa Mikono Yao Wenyewe Huku Watawala wa Waarabu na Waislamu Wakiuzuia Ummah wa Kiislamu Usiwazike

(Imetafsiriwa)

Katikati ya milipuko ya mabomu na makombora ya umbile la Mayahudi, ikinyesha moto juu ya vichwa vya watu wetu mjini Gaza, ambapo wanalenga ghorofa za makaazi, vyuo vikuu, shule, hospitali na misikiti, hata kuangusha mahema chini, kiasi kwamba mifupa ya watoto na nyama zao inachanganyika na vifusi, “mkutano wa aibu na waovu” ulikusanyika na kufanywa. Ilikuwa ni mkutano wa kilele wa watawala Ruwaibidha duni, waovu kutoka miongoni mwa Waarabu na wasio Waarabu.

Mkutano huo, uliopewa jina Mkutano wa Dharura wa Kiarabu na Kiislamu na uliofanyika jijini Doha, Qatar, hauzalisha zaidi ya kile kilichotarajiwa kutoka kwa watawala hao Ruwaibidha, shutma tu na maneno ya masikitiko. Shutma hizo hazikuwa hata kwa ajili ya mashahidi waliokufa jijini Doha na Gaza, bali kwa madai ya shambulizi dhidi ya ubwana wa “Himaya ya Doha.” Baada ya idadi ya mashahidi katika Gaza kuzidi makumi ya maelfu, hawakuwapa hata pumzi ndogo, ya kushutumu na kulaani. Badala yake, wale Ruwaibidha walitoa tamko la kulaani “uvamizi wa Israel dhidi ya Doha,” na kulilaani kama “usaliti na uoga wa wazi.” Ama kuhusu tamko lao la kuhitimisha, halikukengeuka kutoka katika sera ya uoga waliyoitabanni tangu walipowekwa juu ya shingo za Umma bora ulioletwa kwa wanadamu, katika Ulimwengu wote wa Kiislamu.

Haikuwakwepa vibaraka wa Marekani walioshiriki katika fedheha hii kukutana pembeni yake ili kuthibitisha kile kinachowashughulisha, kupiga vita Uislamu na Waislamu. Kwa hivyo, Abdel Fattah el-Sisi wa Misri alikutana na Shehbaz Sharif wa Pakistan kando ya ushiriki wake katika mkutano huo. Balozi Mohamed el-Shennawy, msemaji rasmi wa afisi ya rais wa Misri, alisema kuwa El-Sisi alianza mkutano huo kwa kutoa rambirambi za dhati kwa serikali, na watu wa Pakistan, kuhusu wahanga wa mafuriko ya hivi karibuni na wahanga wa operesheni ya kigaidi iliyofanyika mnamo 13 Septemba, akithibitisha msimamo thabiti wa serikali ya Misri katika kulaani na kukemea aina zote za ugaidi na itikadi kali na kupinga kwake waziwazi wa matukio hayo ambayo yanatishia usalama na utulivu. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Pakistan alisifu dori changamfu ya Misri katika kutuliza mivutano ya kikanda, na kupongeza juhudi za upatanishi za Cairo za kuleta usitishaji vita huko Gaza, na majaribio yake ya kupunguza mateso ya raia, pamoja na dori yake ya kuwezesha makubaliano ya kuregesha ushirikiano kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.

Haya yote ni huku damu ya Umma ikichemka juu ya yale yanayotokea katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na nyoyo zao zikiwaka moto kwa ajili ya ndugu zao dhaifu mjini Gaza na katika Palestina nzima, wakati ambapo Umma wa Kiislamu unajikusanya kupigana na Mayahudi, na wakati huo huo wale waliojiletea Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) juu yao wenyewe, wanauchokoza Umma wa bilioni mbili. Ni kana kwamba fikra yao inatangaza, “Kwa nini hamji kutuzika katika makaburi tuliyochimba kwa mikono yetu wenyewe?” Ni katika wakati huu ambapo watawala hao Ruwaibidha wanakusanyika, huku wakiutawala Ummah ambao, lau ungetaka ungeweza kung'oa milima. Basi vipi Umma wa Kiislamu usilisage sage umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, ambalo haliwezi kubakia hata mbele ya nchi ndogo kabisa kati ya nchi zilizokusanyika?!

Ufafanuzi wa fumbo hili umekuwa wazi kwa kila mtu wa karibu na mbali. Hawa sio watawala wakweli na waaminifu wa Umma wa Kiislamu. Badala yake, wao ni vibaraka wa dola za kikoloni za Magharibi na walinzi waaminifu wa uvamizi wa Wazayuni, na wengi wao wanapaswa kuhisabiwa pamoja na Mayahudi. Kazi yao pekee ni kulinda maslahi ya Magharibi katika Ardhi za Kiislamu na kulinda umbile lenye saratani la Kiyahudi, ambalo ni kambi ya kijeshi ya Magharibi ndani ya moyo wa Ulimwengu wa Kiislamu. Pia wanafanya kazi ya kuzuia kuunganishwa kwa Umma wa Kiislamu na kusimamishwa dola ya Kiislamu, Khilafah kwa Njia ya Utume.

Imekuwa ni jambo la dharura na la lazima zaidi kuliko hapo awali kuwaondoa, na hivyo kufagilia mbali ushawishi wa Kimagharibi kutoka katika ardhi za Waislamu, hususan na watu wenye nguvu za kijeshi na wenye uwezo katika ardhi za Kiislamu, yaani majeshi ya Kiislamu, yanayoongoza miongoni mwao ni Jeshi la Waislamu, Mujahidina la Pakistan. Ni faradhi ya Shariah kwa maafisa wenye ikhlasi ndani ya jeshi la Pakistan kutoa Nusrah yao (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir. Hiki ndicho kitendo pekee kitakachowaondolea hatia dhamiri zao, kuwarudisha hadhi katika nyuso zao na kutekeleza faradhi yao ya Shariah, ambayo yote yamechafuliwa na viongozi hawa wa Ruwaibidha. Wasipofanya hivyo, watazama katika fedheha na aibu duniani kabla ya kuzama kesho Akhera.

Ni lini maafisa wanyoofu watamnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) kwa kutoa Nusrah (msaada wa kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir, ambayo itasimamisha Khilafah na kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt), kuandaa majeshi na kuyaongoza katika ukombozi (tahrir) wa Ardhi Iliyobarikiwa, kulipiza kisasi kwa niaba ya kina mama waliofiwa. Watoto na wazee, na kuzika uvamizi wa Wazayuni katika kaburi ambalo walichimba kwa mikono yao wenyewe? Heshima hii ni kwa wale tu wanaostahiki. Basi ni nani miongoni mwa watu wa msaada wa kijeshi (Nusrah) anastahiki heshima ya kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) ili apate kuokolewa na adhabu ya Akhera na kupata neema ya Pepo? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُمْ مِنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ]

“Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu.” [Surah At-Tawba: 123].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu