Jumatano, 11 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  7 Rabi' I 1447 Na: H.T.L 1447 / 05
M.  Jumamosi, 30 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Msamaha Mbele ya Mola Wetu, na Pole kwa Waliojeruhiwa Gaza
Tripoli ash-Sham Yapaza Sauti Yake Dhidi ya Sherehe za Kucheza juu ya Majeraha ya Umma!
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon imetoa wito kwa Mashababu (wanachama) wake kushiriki katika kikao kilichopangwa kwa uratibu na wanaharakati na watu mashuhuri katika mji wa Tripoli, Jumamosi hii jioni saa sita kamili mbele ya Maonyesho ya Kimataifa ya Tripoli, kwa ajili ya kukemea tamasha la densi (Zambo) na kuimba katika mji wa Tripoli, mji wa elimu na wanazuoni, kama udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusiana na makosa yanayofanywa mjini Tripoli na ambayo hayaonyeshi kitambulisho chake, katika wakati ambapo umbile halifu la Kiyahudi linaendesha vita vikali dhidi ya Waislamu wa Palestina kwa jumla na hasa Gaza, na uvamizi na jinai zake zimeenea hadi Lebanon na Syria, kwa kukalia kimabavu sehemu ya ardhi ya Kusini na ardhi ya Syria, na ndege zake hazijaondoka anga zake, zikipiga mabomu na kuangamiza bila kuzuiwa au mwenye kuwazuia!

Waandamanaji walishangazwa na idadi kubwa ya vyombo tofauti tofauti vya usalama, jeshi, ujasusi, habari, usalama wa jumla, na usalama wa serikali vilivyowekwa kuzuia kikao hiki na kuzuia usemi wa maoni ya Kisharia, badala ya kuzuia sherehe za ufisadi katika kipindi cha vita! Na ili kusiwe na mgongano nao, tulisonga makumi ya mita mbali na mikusanyiko hii ya usalama na kijeshi! Kisha tukaendelea na kikao ambapo Sheikh Dkt. Muhammad Ibrahim, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, alitoa hotuba fupi ambapo alikemea uovu huu ambao baadhi ya vyama vya wanawake vilivyo na tashwishi vinavyoungwa mkono na wababe wa pesa vinafanya, na akakemea kitendo hiki kwa wakati huu mahususi. Pia alishutumu kusukuma kwa mamlaka vyombo vya usalama dhidi ya wana wa mji huu, na akathibitisha kwamba mahali pao ni mipakani na makabiliano na Mayahudi, sio katika barabara za jiji la Tripoli. Dori yao ni kuwalinda watu, na sio kuwanyima haki yao, na ni faradhi juu yao kutotekeleza amri za wezi miongoni mwa vigogo wa pesa katika viti vya mamlaka. Sasa ndio wakati wa makabiliano na maandalizi dhidi ya adui, sio wakati wa sherehe na ufisadi, haswa katika mji wa Tripoli.

Na katika maoni yake kuhusu kichwa cha tamasha hilo, “Usiku wa Hisia,” (Zambo) Dkt. Ibrahim alithibitisha kwamba wakati huu ni wakati wa kuhisi masaibu ya watoto na wanawake wa Gaza na kufanya kazi ya kukomesha kuangamizwa kwao, pamoja na kusimama pamoja na maskini wa Tripoli na walionyimwa haki katika nchi hii. Na mamlaka nchini Lebanon lazima ifanye kazi ya kushughulikia mambo ya watu na kuwasaidia maskini na wahitaji, na kutafuta njia ya kuyageuza Maonyesho ya Tripoli kuwa kituo cha kiuchumi kinachoajiri maelfu ya vijana wahitaji kutoka kwa watu wa Tripoli, badala ya kuyageuza kuwa kitovu cha densi, kuimba, kufuru, na ufuska! Kisha kikao hicho kikahitimishwa kwa dua.

[فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ * وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ]

“Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu. Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema.” [Surat Hūd 116-117]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu