Jumatatu, 07 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Waislamu nchini Tunisia: Hakuna Wokovu bila ya Uislamu
(Imetafsiriwa)

Watu wetu waheshimiwa wa Tunisia:

Inatusikitisha kuona masaibu mnayoyapata na ugumu wa kuishi chini ya mfumo wa kishenzi wa kirasilimali ambao umekufanyeni muteseke kati ya kutimiza kwa uchache mahitaji yenu ya kila siku, baada ya bei kupanda sana, na kuhama na kupasua mawimbi ya bahari na ghaibu ya maisha katika kutafuta makombo ya Magharibi inayopora utajiri wenu. Haya yanatokea licha ya utajiri mkubwa wa kifiqhi tulionao na neema nyingi na hazina iliyofichika ambayo Mwenyezi Mungu ameijaalia ardhi yetu nzuri. Hata hivyo, tabaka la wanasiasa (watawala na wapinzani) limehakikisha wanawapa makafiri uwezo juu yetu kwa kujisalimisha kwa balozi za Magharibi, mashirika yao na makampuni ya uporaji, na wakautenga Uislamu katika utawala na sheria na wakatulazimishia sisi katiba zilizotungwa na mwanadamu ambazo zimetufanya kuyumba-yumba katika uchafu wa upotovu, kurudi nyuma, utegemezi wa kisiasa, na migogoro inayodhoofisha kiuchumi, kijamii na kimaadili. Hakuna tofauti kati ya katiba ya kwanza, ya pili, au ya tatu ya jamhuri, zote ni katiba zilizotungwa na mwanadamu zinazotawala kinyume na aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Inasisitiza utawala wa Magharibi na miradi ya kikoloni ambayo inalenga imani, thaqafa na kitambulisho chetu na kuiweka rehani nchi hii, watu, na rasilimali kwa kafiri mkoloni na taasisi zake za kifedha. Juu yake ikiwa ni Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao unakaribia kutukosesha pumzi.

Enyi Waislamu katika Ardhi ya O Muslims in the Land of Zaituni:

[إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]

“Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf: 87]. Licha ya ujanja huu mkubwa wa kikoloni na usaliti wa watawala wa maovu, wokovu wetu kutoka katika makucha yake na kuregea kwetu katika uongozi ambao Mwenyezi Mungu ametukubalia upo karibu sana, kwa sharti kwamba tutazifungue kamba za ukoloni na kushikamana thabiti na imara na kamba ya Mwenyezi Mungu na kujifunga na Shariah ya Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

[وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقاً]

“Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi.” [Al-Jinn:16].

Enyi Watu Wapendwa wa Tunisia: Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inawakumbusheni mambo yafuatayo:

1- Mfumo wa Uislamu sio tu dini ya kikuhani iliyojitenga na maisha. Bali ni imani ambayo kwayo mfumo unachipuza, imani iliyothibitisha uhalisia wa mwanadamu, na kubainisha kuwa yeye ni kiumbe wa Mwenyezi Mungu (swt) na kwamba atakufa na kupelekwa kwa Muumba wake kuhisabiwa, na kwamba Muhammad (saw) alitumwa na Mwenyezi Mungu kwa wahyi kama muongozi, mbashiri na muonyaji, na kwamba ina mfumo unaojumuisha mambo yote ya maisha, na kwa msingi wa imani hii, mifumo mipana ya maisha imechipuza inayodhibiti utawala, uchumi, adhabu, sera ya kigeni na mengineyo... Tunawajibika kushikamana nayo mpaka wakati wa Kiyama, Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ]

“Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.” [Ash-Shura: 10] na hukmu ya wengine ni haramu, Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Al-Maida: 44].

2- Mfumo wa serikali katika Uislamu umejengwa juu ya usimamizi, sio ujanja na udanganyifu ili kufikia nyadhifa. Mtume (saw) akasema:

«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ...»

“Nyote ni wachungaji na nyote mtaulizwa kuhusu mlivyovichunga; Imam juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake...” Na Mwenyezi Mungu (swt) ameufanya usimamizi huu kuwa wajibu wa khalifa, ambapo watu watoa kiapo cha utiifu kwake ili kutabikisha Sheria ya Mwenyezi Mungu na kuwachunga kwayo, na khalifa hana haki ya kutoa amri kwa ajili ya kutafuta maslahi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao.” [Al-Maida: 49]. Na Khalifa hana uhuru kutawala apendavyo au kwa mujibu wa matakwa ya wenye pesa na ushawishi, bali yeye pia ni mwenye kuhisabiwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya kumhisabu Khalifa kuwa ni faradhi kwa Waislamu, watu binafsi na makundi, ambao wanamhisabu kwa Uislamu, si kwa mujibu wa maslahi yao.

3- Uislamu umebainisha sera ya kiuchumi, kujua chanzo cha ugonjwa katika jamii na kuutibu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ]

“ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Al-Hashr: 7]. Aliweka vipengee vinavyozuia mrundiko wa mali mikononi mwa kikundi cha wacheche katika jamii, na kuhakikisha mahitaji ya msingi ya makaazi, chakula na mavazi kwa kila mwanajamii, pamoja na dawa, elimu na usalama. Mwenyezi Mungu (swt) alimelazimsha zakat juu ya mali na kuharamisha riba na kuficha mali ili kuwasukuma matajiri kuwekeza pesa zao katika miradi ya kiuchumi, kuchochea mzunguko wa mtaji katika mzunguko wake wa kimaumbile, kuunda pesa halisi na kuzuia kutokea kwa migogoro ya kiuchumi kama vile mfumko wa bei na ukosefu wa ajira. Uislamu pia umeifanya mali iliyo chini ardhi ya gesi, mafuta, fosfeti, madini na nyinginezo kuwa mali ya umma ya Waislamu wote, kwa mujibu wa yale yaliyosemwa katika hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «النَّاسُ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي الْمَاءِ، وَالْكَلَأِ، وَالنَّارِ» “Watu ni washirika katika mambo matatu: katika maji, malisho na moto” na maandiko mengine ya kisheria. Hakumpa Khalifa haki ya kukabidhi umiliki wa umma, alizuia mtu yeyote kupora pesa za watu, hata awe nani, jambo ambalo Mwenyezi Mungu (swt) amelifanya kwa ajili yao pekee na pia akaharamisha upendeleo unaopeanwa kwa makampuni ya uporaji ya kikoloni na kuwanyimwa watu wetu. Uislamu uliweka vipengee vya kuijenga upya ardhi na kuzifufua zilizokufa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu.

4- Ama kuhusu sera ya kigeni, Uislamu umefanya kubeba da’wah ya Kiislamu kuwa ndio mhimili ambao pambizoni mwake sera ya kigeni inazunguka, na kwa msingi wake uhusiano wa dola na dola zote umejengwa.

Wapendwa Watu katika Tunisia ya Kijani: Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunawalinganieni kuung'oa ukoloni na ala zake nchini na kuukataa mfumo wa kisekula wa kirasilimali, na kuutabanni mfumo wa Kiislamu na mradi wake wa kihadhara ndani ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na tunatambua kuwa tofauti kati ya mulichomo ndani yake sasa na kile tunachokuitia ni jambo kubwa sana, lakini mpito kwa kile tunachokulinganie kwake ni rahisi kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfanyia kuwa rahisi kwake, na ambaye ametimiza sharti lake, na nia ya dhati kwa Mwenyezi Mungu (swt), na kutegemea bora zaidi juu Yake, na kufanya kazi ya kubadilisha uhalisia kulingana na njia ya Mtume (saw) na kwa Mwenyezi Mungu ndio matokeo ya mambo. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj: 41].

H. 26 Safar 1444
M. : Alhamisi, 22 Septemba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu