Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Barua ya Wazi kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwenda kwa Waziri wa Sheria na Haki za Binadamu Mada: Kuongezeka kwa Ukamatwaji Mara Kwa Mara wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
(Imetafsiriwa)

Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Tunawasilisha ombi hili la malalamiko kwako kuhusu kukamatwa mara kwa mara ambako wawakilishi wa Afisi ya Mashtaka ya Umma wamekufanya ndani ya mahakama mbalimbali katika kukabiliana na wanachama wa Hizb ut Tahrir, kwa ajili hiyo, tunaweza tu kukumbusha mambo yafuatayo:

Kwanza: Inajulikana vyema kwamba Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu na kinafanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, kwa mujibu wa iliyotangaza ndani ya sheria yake ya msingi. Ili kufikia lengo hili, inatekeleza shughuli zake kwa kutegemea mvutano wa kifikra na kisiasa na haifanyi vitendo vyovyote vya kisilaha hata kidogo. Bali, inaharamisha kufanya vurugu au kutafuta usaidizi wa kigeni, kwa kuzingatia kwamba hili limeharamishwa na Sharia.

Pili: Kabla ya mapinduzi, Hizb ut Tahrir ilikabiliwa na mashtaka mengi yasiyo ya haki kuanzia mwaka 1983 hadi 2010, na hukumu zote zilizotolewa dhidi ya wanachama wake zilikuwa za "kujiunga na chama kisichoruhusiwa." Hukumu za kutiwa hatiani zilianzia mwaka mmoja hadi miaka miwili gerezani, isipokuwa kwa hukumu zilizohusisha wanajeshi.

Tatu: Baada ya mapinduzi, wanachama waliohukumiwa wa Hizb ut Tahrir walipata msamaha wa jumla na kupata haki zao za kiraia. Pia walipata visa ya kazi ya kisheria kwa kuzingatia Amri Na. 87 ya 2011 ya Septemba 24, 2011 inayohusiana na upangiliaji wa vyama vya kisiasa. Pamoja na hayo, wanachama wake waliendelea kukabiliwa na misukosuko ya usalama na kukamatwa kiholela, jambo ambalo lilikomeshwa haraka mara tu walipofika mbele ya mjumbe wa afisi ya Mashtaka ya Umma aliyekuwa akisimamia faili la utafiti.

Nne: Baada ya Julai 25, 2021, hali haikufungika tena katika vitendo vya polisi. Badala yake, wawakilishi wa Afisi ya Mashtaka ya Umma, licha ya hali yao ya kimahakama, wana dori hasi, na katika hali nyingi wanafuatana na vitendo hivi vya nasibu, hata baadhi ya waendesha mashtaka hata hupeleka ripoti za utafiti kwa mjeledi wa mahakama wa ugaidi, ambayo ilileta mabadiliko ya hatari kwa sera ya adhabu ambayo ina upendeleo kwa kuzuia na kuzingira shughuli ya Hizb ut Tahrir na kujaribu kuwatisha wanachama wake.

Tano: Katika hatua nzito inayofichua mabadiliko ya sera hiyo ya adhabu, mkuu wa afisi ya eneo ya Hizb ut Tahrir katika eneo la Kelibia, Bw. Adel Al-Ansari, alikamatwa na kuregelewa kesi ya uwasilishaji kwa umma wa Tukio la Kwanza la Mahakama ya Kiidara, Mzunguko wa Tatu huko Nabeul (faili ya kesi Na. 23/1846), ambayo haikumruhusu kuwa na haki ya kujitetea na kukataa ombi lake la kuchelewesha kazi ya wakili na kumhukumu mara moja kutiwa hatiani kwa "kukiuka sheria ya dharura na kusambaza vipeperushi ambavyo vitavuruga amani ya utulivu wa umma" kwa kufungwa kwa muda wa miaka miwili na utekelezwaji wa haraka!!

Sita: Uamuzi huu wa kimahakama usio wa haki, ambao kwa kiasi fulani ulibatilishwa na Mahakama ya Rufaa ya Nabeul (kesi ya Uamuzi wa Rufaa Na. 1363) na kuridhika na ripoti ya hatia ya kusambaza vipeperushi na kupunguza adhabu ya viboko hadi kifungo cha miezi mitatu jela, inadhihirisha kukwama kwa sera iliyoidhinishwa ya adhabu ambayo inatishia kudhoofisha mafanikio muhimu zaidi ya mapinduzi - kama ilivyosemwa - katika uhuru wa mahakama na kuheshimu haki za msingi ambazo zimeidhinishwa na sheria za nchi, hasa amri kuhusiana na mpangilio wa vyama vya kisiasa, kwa kuzingatia kwamba kesi hii imerudiwa dhidi ya wanachama wengi wachangamfu wa Hizb, lakini kwa hukumu nyepesi na zisizo kali.

Saba: Mtazamo huu mpya wa kimahakama ambao unashutumu shughuli za kisiasa tu na kuzingatia taarifa za kisiasa kama "machapisho yanayovuruga amani ya utulivu wa umma" utasababisha uharibifu mkubwa kwa sifa ya mahakama, ambayo umechukua jukumu la kuisimamia, na kuifanya iwe hatarini kuwa ni ya kudharauliwa na kila mtu pale inapopuuza viwango vya chini vya uhuru na kukiuka nususi za kisheria za haki za binadamu ambazo bado zinatumika, kwa kuongozwa na maagizo ya kisiasa yasiyo ya haki. Je, sheria zinatungwa ili zikanyagwe?

Nane: Katika wakati ambapo tunaibua shutuma hizi zinazofichua kushindwa kwa mfumo wa mahakama katika nchi yetu na kupuuza kwake viwango vya chini kabisa vya uhuru na usawa, tuna hakika kwamba mahakama haiwezi kuwa huru na ya haki isipokuwa chini ya mfumo wa sheria wa Kiislamu ndani ya mfumo wa utawala wa haki uliojengwa juu ya Uislamu; ni kanuni ambayo haijui upendeleo au kunyenyekea kwa dhalimu au dikteta, katika kutabikisha kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ لِلّهِ شُهَدَاء بِالْقِسْطِ وَلاَ يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلاَّ تَعْدِلُواْ اعْدِلُواْ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَاتَّقُواْ اللّهَ إِنَّ اللهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Ma’idah 5:8] and

[وَزِنُواْ بِالقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]

“Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na khatimaye ndio bora.” [Al-Isra 17:35].

Hii ni notisi yetu kwako, tukitaraji kuwa utaifahamu kwa sikio la ufahamu.

Wa Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

H. 12 Dhu al-Qi'dah 1444
M. : Alhamisi, 01 Juni 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu