Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 20 Safar 1447 | Na: 1447/13 |
M. Alhamisi, 14 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kauli za Netanyahu baina ya Uhalisia wa Umbile lake na Msimamo Unaofifia wa Serikali ya Misri
(Imetafsiriwa)
Kauli za Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu, ambazo alizungumza moja kwa moja kuhusu kile kiitwacho “Israel Kubwa zaidi” na kuhusu mipango ya uhamishaji na upanuzi, zinafichua kwa mara nyengine tena itikadi iliyokita mizizi ndani ya nyoyo za viongozi wa umbile hili; itikadi ya khiyana, usaliti, na ulafi wa ardhi ya Waislamu. Matamshi haya si kuteleza kwa ulimi, bali ni tafsiri ya kivitendo ya mipango iliyoandikwa katika fikra ya kisiasa ya Kizayuni, na mipango inayotekelezwa uwanjani hatua kwa hatua.
Viongozi wa Mayahudi wamezoea kueleza matamanio yao kwa ujasiri kila wanapohisi kwamba mazingira ya kisiasa yanayowazunguka ni salama, na kwamba Dola za Kiarabu zinazowazunguka hazina uwezo au zinashiriki nao. Netanyahu asingetamka maneno haya kama asingejua kwamba Misri, pamoja na jeshi lake kubwa, idadi kubwa ya watu, na eneo lake la kistratejia, utashi wake umefungwa pingu, na kwamba mfumo wake wa kisiasa umejikita katika kulinda usalama wa Mayahudi na juu ya usalama na uratibu wa kijeshi pamoja nao, kwa kisingizio cha "amani" na makubaliano ya khiyana.
Alitanguliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa kusema kuwa "Israel ni ndogo sana" na kwamba anaona ulazima wa kuipanua. Matamshi haya, yawe yanatoka kwa afisa katika umbile hilo nyakuzi au kutoka kwa wafuasi wake katika nchi za Magharibi, yanathibitisha kwamba kuna mradi mpana wa kisiasa, usalama, na kiuchumi unaofanya kazi ya kuchora upya ramani ya eneo hilo kwa ajili ya kuimarisha uwepo wa umbile hilo na kupanua ushawishi wake.
Mbele ya kauli hizi zinazogusa madai ya usalama wa taifa la Misri kabla ya ile ya nchi zengine, majibu rasmi ya Misri kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje yalikuja kwa njia ya "kulaani na kutaka ufafanuzi," kana kwamba suala hilo ni suala la mzozo wa vyombo vya habari au sintofahamu ya kisiasa, na sio tishio la moja kwa moja kwa ubwana wa Misri, ardhi yake na rasilimali zake! Serikali haikutangaza hali ya hofu, wala haikutoa wito kwa Ummah kuhamasika, wala haikuchukua hatua zozote za kivitendo zinazoonyesha nia ya kweli ya kukabiliana na njama hizi.
Jibu hili la serikali ya Misri si geni, bali ni muendelezo wa sera inayodhibiti hatua zake kwa mujibu wa ahadi za kimataifa na za kieneo, mashuhuri zaidi kati yake ni Makubaliano ya Camp David, ambayo yaliweka vikwazo vya harakati za jeshi la Misri na kufunga usalama wa Sinai na eneo hili kwa dira ya Marekani na washirika wake. Kwa hivyo, maswala ya hatari yamegeuka kuwa faili za kidiplomasia zinazosimamiwa na kauli baridi ambazo zinawatia watu ganzi na kumhakikishia adui kwamba mambo yamedhibitiwa, badala ya kuwa uwanja wa kazi makini ya kulinda ardhi na heshima.
Serikali ya Misri, kama serikali nyenginezo katika ardhi za Kiislamu, hazichukui hatua kwa mujibu wa Aqida (itikadi) ya Kiislamu ambayo imefanya kupigana na mvamizi kuwa ni faradhi, bali inasonga mbele kwa mujibu wa maslahi yake finyo na mafungamano ya kimataifa, hususan kulinda usalama wa umbile la Kiyahudi na kuhakikisha kwamba linabakia hai. Kwa sababu hii, jibu lilikuwa ni jaribio tu la kuokoa uso mbele ya rai jumla, bila kugusa dhati ya uhusiano halisi wa kirafiki kati yake na umbile la Kiyahudi.
Kauli hizi na vitisho na miradi ya upanuzi wanayobeba si chochote ila ni tangazo jipya la vita dhidi ya Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا]
“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqarah: 217]. Na Mayahudi ndio mfano wa wazi wa ukweli huu, kwani walisaliti maagano, walivunja mikataba, walipigana na Waislamu, na walijifungamanisha na washirikina dhidi ya dola ya Kiislamu. Leo, vizazi vyao vinarudia, hata zaidi kupitia ukaliaji kimabavu, uhamishaji, kuua, na kufukuza kwa njia kali zaidi na ya kihalifu, wakiungwa mkono na Magharibi.
Umbile hilo la Kiyahudi linaziona serikali za nchi za Kiislamu ikiwemo serikali ya Misri kuwa walinzi wa mipaka yake na wadhamini wa usalama wake, hata kama watarushiana maneno ya kashfa mbele ya vyombo vya habari. Uhalisia ni kwamba serikali ya Misri inatembea tu ndani ya mipaka iliyowekwa kwa ajili yake na Marekani, na mipaka hii inaweka ulinzi wa usalama wa Mayahudi juu ya kitu chochote kile, hata juu ya damu na heshima ya Waislamu.
Kwa kuchanganya kauli ya hivi karibuni ya Netanyahu na kauli ya awali ya Trump inafichua kwamba matamanio yao hayaishii kwa Jerusalem, Ukingo wa Magharibi na Gaza pekee, bali pia yanajumuisha Sinai, Mto Nile na baadhi ya maeneo ya nchi za Kiarabu. Hii si ndoto ya kisiasa, bali ni sehemu ya machapisho yao na mipango iliyotangazwa, na inapaswa kuwa dalili kwamba upole wowote katika kukabiliana nao unafungua milango kwao kufikia malengo yao. Kauli hizi ni ujumbe kwa kila Muislamu kwamba adui yako anapanga kumeza ardhi yako, historia yako, na Dini yako, na kwamba wakati umefika wa kuchukua hatua kali, pamoja na jeshi ambalo Aqida yake ni jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, sio kulinda makubaliano ya khiyana!
Enyi Watu wa Misri - Kinanah: Kauli za viongozi wa Mayahudi na wafuasi wao wa Magharibi ni ujumbe ulio wazi. Jibu kwao si kwa kauli wala kwa diplomasia, bali kwa vitendo vinavyoweka uhalisia mpya kwa adui huyu.
Enyi Askari wa Kinana: Uwezo wenu na eneo la nchi yenu vinaweka juu yenu jukumu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, basi msiiache fursa hii ipite kwenu, kwani vita na Mayahudi ni vita vya Aqida na uwepo, na havitaamuliwa isipokuwa kwa kuikomboa Palestina. Wajibu wenu ni kutangaza vita kamili dhidi ya umbile hili nyakuzi, kuling'oa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa, kuikomboa kikamilifu, na kuregesha mamlaka yaliyonyakuliwa ya Umma.
[وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ * الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj: 40-41]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |