- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Mkakati wa Amerika na Suluhisho la Dola Mbili
(Imetafsiriwa)
Swali:
Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai? Shukran.
Jibu:
Ili kufafanua jibu, hebu tuhakiki mambo yafuatayo:
1- Mnamo 1959, mwishoni mwa muhula wa Eisenhower, Amerika ilitabanni mradi wake wa suluhisho la dola mbili, ambao unaweza kufupishwa kama "kuunga mkono na kuhifadhi umbile la Kiyahudi na kuanzisha umbo la Palestina kando yake." Vibaraka wake katika eneo hilo, hasa serikali ya Misri, walianza kufanya kazi ili kutekeleza mradi huo, na kwa ajili hiyo, Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) lilianzishwa. Hata hivyo, Uingereza, kupitia utawala wa Jordan, ilipinga vikali mradi huo na ikatabanni mradi wa dola ya kisekula ya Palestina inayodhibitiwa na Mayahudi, sawia na dola ya kisekula ya Lebanon, ambayo inadhibitiwa na Wakristo.
2- Haya yote yalikuwa wakati Ukingo wa Magharibi ulipokuwa chini ya utawala wa Jordan, na Gaza ilikuwa chini ya utawala wa Misri. Walakini, wakati Ukingo wa Magharibi na Gaza, pamoja na Sinai na Milima ya Golan, zilipoanguka chini ya udhibiti wa umbile la Kiyahudi katika vita vya kisanii mnamo Juni 1967, mazungumzo hayakuwa tena kuhusu kuanzishwa kwa dola ya Palestina, lakini juu ya kujiondoa kwa umbile la Kiyahudi kutoka kwa maeneo haya yaliyokaliwa kwa msingi wa Azimio la Baraza la Usalama la 242. Kisha Amerika ikaiweka pembeni kadhia ya Palestina na kuanza kuandaa vita vya uchokozi. Hivi vilikuwa ni Vita ya Oktoba ya 1973 ili kuanzisha mchakato wa amani. Serikali ya Misri, ikiongozwa na Anwar Sadat, ilitia saini Makubaliano ya Camp David mnamo Septemba 1978. Kulingana na makubaliano haya, umbile la Kiyahudi lilijiondoa kutoka Sinai, huku likibaki kufungwa katika silaha zake kama eneo la usalama (buffer) kulinda mipaka ya umbile hilo. Inaendelea kuwa hivyo hadi leo, licha ya vita vya maangamizi vilivyoanzishwa na umbile hilo halifu mjini Gaza kwenye mpaka wa Sinai!
3- Kisha Amerika ikahamia upande wa kaskazini, na kuamuru umbile la Kiyahudi kuivamia Lebanon mnamo 1982 ili kuifukuza Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina kutoka huko na kuilazimisha kulitambua umbile la Kiyahudi na kuhitimisha makubaliano ya amani nalo. Mkuu wa shirika hilo, Yasser Arafat, alitia saini haya mnamo 25/7/1982, katika kile kilichojulikana kama Hati ya McCloskey, ambapo alisema: "Shirika hili sasa linatambua haki ya Israel ya kuwepo." Mnamo 1988, Arafat alitangaza katika Kongamano la Kitaifa la Palestina lililofanyika nchini Algeria, na vile vile katika mkutano mbele ya Umoja wa Mataifa jijini New York, kukubali kwake kuanzishwa kwa dola ya Palestina. Kisha Uingereza na kibaraka wake, Mfalme wa Jordan, walikubali kujitenga na Ukingo wa Magharibi katika mwaka huu.
4- Baada ya hapo, Amerika ilifanya Kongamano la Madrid mnamo 1991 ili kuendelea na utekelezaji wa mradi wake wa suluhisho la dola mbili. Kisha, Makubaliano ya Oslo yalihitimishwa kati ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na umbile la Kiyahudi mnamo 1993, ili shirika hilo kutambua rasmi umbile la Kiyahudi. Pia, Mkataba wa Wadi Araba (26/10/1994) ulihitimishwa kati ya shirika hilo na Jordan, kwa Jordan kutoa Ukingo wa Magharibi ambao ulikuwa sehemu yake, na kisha kutangaza utambuzi wake wa umbile la Kiyahudi. Amerika iliinuka na kuyadhibiti makubaliano hayo mawili ya kutekeleza mradi wake wa suluhisho la dola mbili. Baada ya kumalizika kwa mihula miwili ya Bush mwishoni mwa 2008, Obama aliingia madarakani jijini Washington. Aliomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Mamlaka ya Palestina na umbile la Kiyahudi chini ya ufadhili wa Amerika mnamo 2/9/2010, akitumai kuwa ndani ya mwaka mmoja suluhisho la dola mbili litatekelezwa. Hata hivyo, mazungumzo hayo yalimalizika bila kufikia muafaka.
5- Baada ya mihula miwili ya Obama mwishoni mwa 2016, Trump aliingia madarakani mapema 2017 na kuendelea na muhula wake wa kwanza, kisha kushindwa katika uchaguzi. Biden alimrithi mapema 2021. Baada ya mwisho wa muhula wa Biden, Trump alishinda tena na kuwa rais mapema 2025.
Katika vipindi hivi viwili – enzi za Trump na Biden – mwelekeo tofauti uliibuka kutoka kwa marais waliopita wa Amerika. Tangu Amerika ilipotangaza mwelekeo wake wa suluhisho la dola mbili, marais waliopita walikuwa wametaja suluhisho hilo bila kuelezea kwa undani juu ya dola ya Palestina. Watu wasioona mbali walidhani kwamba Wapalestina wangepewa dola huru katika sehemu ya Palestina. Trump na Biden walipoingia madarakani, walichunguza baadhi ya maelezo, wakisema kwamba kile Wapalestina wangepewa ni dola isiyo na nguvu za kijeshi, sawa na uhuru mdogo, usio na nguvu, unaotawaliwa na Mayahudi, huku kukiwa na tofauti kati yao katika nguvu na utata wa kauli zao. Hapa, maswali yalizuka: Je, mradi wa suluhisho la dola mbili wa Marekani umemalizika, au haujakwisha ungali unaendelea? Ni muhimu kutaja kuwa kauli ya Mayahudi kuhusu Palestina haina uzito wowote isipokuwa kwa kamba (msaada) kutoka kwa watu (Marekani). kauli ya Marekani ndiyo mada ya majadiliano:
6- Uchunguzi wa kina wa suala hilo unaonyesha yafuatayo:
A- Hapo awali tulijibu Jibu la Swali la tarehe 23/2/2017, kuhusu suluhisho la dola mbili baada ya Trump kuanza muhula wake wa kwanza madarakani, ambalo lilisema:
[(1- Maandishi ya taarifa za Rais Trump kama ilivyoripotiwa katika ulimwengu wote na vyombo vya habari vya ndani na kama ilivyotangazwa moja kwa moja, ni kama yafuatavyo:
"Rais wa Marekani Donald Trump ameandika mnamo Jumatano mtazamo mpya katika sera ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati baada ya kuthibitisha kwamba suluhisho la dola mbili sio njia pekee ya kumaliza mzozo wa Israel na Palestina, akionyesha kuwa yuko tayari kwa chaguzi badali ikiwa zitaleta amani. Marais wote wa zamani wa Marekani wametetea suluhisho la dola mbili, iwe wa Republican au Democrats" (Tovuti ya France 24, 16/2/2017) na Trump akasema, “Naliangalia suluhisho la dola mbili na suluhisho la dola moja (...) kama Israel na Wapalestina watafurahi, nitafurahishwa na (suluhisho) wanalopendelea, masuluhisho yote mawili yananifaa" (Tovuti ya Aljazeera Live, 16/2/2017), azimio la dola moja lililotajwa na Amerika kwa mara ya kwanza kupitia Trump, hakulifafanua, je ina maana ya kutoa uhuru wa kujitawala kwa Wapalestina ndani ya dola moja ya Kiyahudi?! Au ina maana ya dola ya kisekula ambayo Wapalestina wanashiriki katika usimamizi wa dola ya Kiyahudi, ambayo ni sawa na mradi wa Kiingereza ulioanzishwa na Uingereza mwaka wa 1939 wakati ilileta Kitabu Cheupe juu ya fomula ya Lebanon? Kumbuka kuwa suluhisho la dola mbili ni mradi uleule wa Marekani ulioanzishwa tangu 1959, enzi za Rais wa Republican Eisenhower na uliifanya ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa iukubali na kutupilia mbali mpango wa dola moja ulioanzishwa na Uingereza. Vyovyote iwavyo, kinachoonekana kutokana na kuzichambua kauli hizi na dalili zake ni kwamba Marekani haijaliacha suluhisho lake la dola mbili; balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alithibitisha hili na kusema: "Kwanza kabisa, suluhisho la dola mbili ndilo tunalounga mkono. Yeyote anayesema kwamba Marekani haiungi mkono suluhu ya dola mbili atakuwa amekosea ... hakika tunaunga mkono suluhisho la dola mbili, lakini pia tunafikiri nje ya sanduku ... ambapo inahitajika ili kuvutia pande hizo mbili kwenye meza, ambalo ndilo tunalohitaji ili kukubaliana." (Reuters, 16/02/2017).
Hili linathibitisha kwamba Trump hakuachana na suluhisho la dola mbili, ambalo ni sera ya serikali ya Marekani tangu 1959, lakini alitaka kujaribu njia nyengine ya kuweka shinikizo, kama balozi wake alivyosema (hakika tunaunga mkono suluhisho la dola mbili, lakini pia tunafikiri nje ya sanduku ...) kwamba ni kwa kuzingatia matumizi ya mbinu nyenginezo.] MWISHO WA NUKUU.
B- Kauli za Trump (Republican) za kuwaunga mkono Mayahudi zilishika kasi katika muhula wake wa kwanza na wa pili madarakani:
*Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza Marekani kuitambua Al-Quds (Jerusalem) kama mji mkuu wa "Israel." Trump pia alithibitisha kuwa Marekani inaunga mkono suluhisho la dola mbili iwapo litaidhinishwa na Waisraeli na Wapalestina. (BBC, 6/12/2017)
*Rais Trump wa Marekani alisema kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, anaamini kuwa suluhisho la dola mbili katika mzozo wa Israel na Palestina “litafanya vyema zaidi,” na kuongeza, “Ni ndoto yangu kuweza kufanikisha hilo kabla ya mwisho wa muhula wangu wa kwanza.” (BBC, 26/9/2018)
* Rais Trump wa Marekani alisema, “Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, Israel ni sehemu ndogo ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa. Kwa hakika nilisema: ‘Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo mno...” (Sky News, 19/8/2024).
* Hapo awali, Rais wa Marekani Donald Trump alisisitiza mpango wake kwa Marekani kudhibiti Gaza na kuwafukuza Wapalestina kutoka humo, akisema “amejitolea kuinunua na kuimiliki Gaza...” (BBC, 10/2/2025). Kisha, siku kumi baadaye, alitangaza, “Hatalazimisha mpango wa kuwafukuza Wapalestina kutoka Gaza, lakini badala yake ‘anapendekeza’...” (CNN, 21/2/2025). Huku ni kudanganya kimaneno!
C- Kwa upande mwingine, kauli za Biden (Democrat) wakati fulani zimekwenda zaidi ya zile za Trump za kuwaunga mkono Mayahudi:
* Wakati Trump alipopoteza uchaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na Biden mwanzoni mwa 2021, Amerika iliregea kuzungumza juu ya kuanzisha dola ya Palestina kwa namna fulani, bila kutaja jinsi au wapi. Rais wa Marekani Joe Biden aliwaambia waandishi wa habari mnamo tarehe 3/9/2024, “Kuna mifano kadhaa ya suluhisho la dola mbili, akibainisha kuwa nchi kadhaa katika Umoja wa Mataifa hazina vikosi vyao wenyewe vya kijeshi.” Biden anakusudia dola ya Wapalestina ya mojawapo ya aina hizo, bila majeshi, yaani, yenye kujitawala wenyewe au kitu kama hicho!
* Wakati Rais Biden wa Marekani alipotembelea Tel Aviv mnamo tarehe 18/10/2023, kufuatia Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa, alikutana na maafisa huko na kusema: “Israel lazima tena iwe mahali salama kwa Mayahudi. Kama kusingekuwa na Israel, tungelazimika kubuni moja.” (Al Jazeera, 18/10/2023).
* Katika hotuba moja aliyoitoa katika Ikulu ya White House wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Kiyahudi ya Mwanga (Hanukkah), Biden alisema: “Si lazima uwe Myahudi ili uwe Mzayuni, na mimi ni Mzayuni.” (Asharq Al-Awsat, 12/12/2013).
7- Kwa kutafakari Swali na Jibu lililopita, pamoja na kauli na misimamo hii, inadhihirika kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya misimamo ya Trump na Biden isipokuwa katika baadhi ya njia ambazo hazibadilishi kiini cha suala hilo hata kidogo…Marekani ndiyo inayosimamia suala hili kwa msingi wa dola mbili: dola ya Mayahudi katika sehemu kubwa ya Palestina, ambayo inaiunga mkono kifedha, kijeshi, kimataifa, na hata kieneo kupitia vibaraka wake na wafuasi wake miongoni mwa watawala katika nchi za Kiislamu.. na dola isiyo na jeshi (inayojitawala) kwa Wapalestina katika sehemu ya Palestina yenye udhibiti wa Kiyahudi juu yake!! Bila kujali hamu ya “Mamlaka ya Palestina (PA) na watawala vibaraka” kuiita dola ya Palestina, hii haibadilishi chochote katika uhalisia wake, kwani Amerika haitaki iwe dola yenye ubwana hata juu ya sehemu ya Palestina, bali zaidi kama kujitawala wenyewe bila silaha isipokuwa kile ambacho ni muhimu kwa polisi ndani ya udhibiti wa Kiyahudi!! Mambo mawili yaliibuka wakati wa mihula ya urais wa Trump na Biden ya kuimarisha umbile la Kiyahudi ambapo inathibitisha kile tulichotaja hapo juu, ingawa yalikuwa maarufu zaidi wakati wa Trump, nayo ni:
La kwanza: ambalo linafanyika hivi sasa, ni kulitia nguvu umbile la Kiyahudi na kulipatia fedha na silaha ili libaki kuwa nguvu kuu ya kijeshi kuliko dola zote zinazolizunguka.
La pili: kuhalalisha mahusiano, katika kile Trump alichokiita Mkataba wa Abraham; ambacho ndicho alichokipata katikati ya muhula wake wa kwanza na sasa anataka kukimaliza. Kwa hiyo, wajumbe wa Marekani wanazuru katika eneo hilo sio tu ili kuishawishi Saudi Arabia kujiunga na kile kiitwacho Makubaliano ya Abraham, lakini pia wanaweka msingi na kufungua mazungumzo, ambayo kwa sasa yanaendelea kati ya Syria na Lebanon na umbile la Kiyahudi. Marekani inataka kupanua mchakato huu ili kujumuisha watawala wengine vibaraka katika nchi za Kiislamu!
Kwa kumalizia, Amerika haikuachana na suluhisho la dola mbili, lakini chini ya Trump na Biden, imetangaza dola inayokusudiwa ya Palestina kuwa aina fulani ya uhuru wa kujitawala unaodhibitiwa na Mayahudi. Hata hivyo, marais waliotangulia walitaja suluhisho la dola mbili bila ya kuzama katika umbile la dola hiyo wanayoitazamia kwa Wapalestina!
8- Hatimaye, Palestina ni johari katika historia ya Waislamu kwani Mwenyezi Mungu (swt) aliiunganisha na Nyumba yake tukufu kwa fungamano moja, pale alipomtoa Mtume wake (saw) kutoka katika Msikiti Mtakatifu hadi kwenye Msikiti wa Al-Aqsa.
[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]
“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka.” [Al-Isra: 1]
Na kuifanya ardhi nzuri na yenye baraka. Na akazivutia nyoyo za Waislamu kwenye mji mkuu wa Palestina (Bait ul Maqdis) kwa kuufanya Kibla chao cha kwanza kabla ya Mwenyezi Mungu kuwapa Waislamu Kibla chao cha pili (Ka’ba tukufu) miezi kumi na sita baada ya Hijra. Hiyo ilikuwa kabla ya Palestina kuwa chini ya utawala wa Uislamu wakati Khalifa wa pili, Omar ibn al-Khattab (ra), alipoifungua katika mwaka wa 15 H. Aliichukua kutoka kwa Sophronius na akampa agano lake maarufu (Agano la Omar), moja ya maandishi, kulingana na ombi la Wakristo huko, ilikuwa (kwamba Mayahudi wasiishi nao hapo). Kisha Palestina ikawa makaburi ya Mkruseda na Watatari. Kulikuwa na vita vya maamuzi kwa Makruseda na Watatari: Hattin (583 H - 1187 M), na Ain Jalut (658 H - 1260 M), na vitafuatwa, Mwenyezi Mungu akipenda, na vita vyengine vya maamuzi kwa Mayahudi ili kurudisha Palestina takatifu na safi kwenye nyumba ya Uislamu.
Kuendelea kuwepo kwa umbile la Kiyahudi nchini Palestina hadi leo hakutokani na nguvu zao, kwani wao si watu wa kupigana na kushinda, bali kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:
[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]
“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i-Imran: 111].
Kuishi kwao kunatokana na kufeli kwa watawala katika nchi za Kiislamu. Mkosi wa Waislamu uko kwa watawala wao, kwani wao ni watiifu kwa wakoloni makafiri, maadui wa Uislamu na Waislamu. Wanaona na kusikia kuhusu uvamizi wa Mayahudi nchini Palestina, uhalifu wao wa kikatili, na mauaji yao mbalimbali, lakini ni kana kwamba hawaoni wala hawasikii.
[صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ]
“Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.” [Al-Baqarah: 18]
Wamezuia majeshi kuwanusuru ndugu zao wa Gaza hadi leo, na mashahidi wanaongezeka na majeruhi wanaongezeka ... na watawala wanatazama kinachotokea, na mbora wao ni yule anayehesabu mashahidi chini ya jina la maiti, kisha anawahesabu waliojeruhiwa kana kwamba yeye ni upande usioegemea kokote, ingawa yeye yuko karibu na Mayahudi! Wanaweka “viti vya madaraka” juu ya nchi yao na watu wao! Ijapokuwa, Ummah huu ndio umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, hautakaa kimya kwa muda mrefu, Mwenyezi Mungu akipenda, kuhusiana na utawala huu dhalimu wa hawa Ruwaibidha (watawala wajinga wasio na umuhimu). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitupa bishara njema ya kuregea Khilafah Rashida baada ya utawala huu dhalimu kama ilivyoelezwa katika Musnad Al-Imam Ahmad na Al-Tayalisi kutoka kwa Hudhayfah ibn Al-Yaman: «... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ» “…Kisha kutakuwa na utawala wa kidhalimu (ملكًا جبرية) kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa atakapo, na kisha itakuweko Khilafah kwa njia ya Utume.’ Kisha yeye (saw) akanyamaza.” Waislamu watapewa izza na makafiri watadhalilishwa.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]
Jambo la ajabu ni kwamba Makafiri, hasa Mayahudi, wanalitambua hili zaidi kuliko Waislamu wengi wa leo. Mayahudi wanatambua kwamba Khilafah itawapeleka kwenye maangamivu yao. Waziri Mkuu wao alisema katika mkutano na waandishi wa habari uliopeperushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, ikiwemo Al Jazeera, mnamo tarehe 21/4/2025: “Hatutaruhusu kusimamishwa kwa Khilafah kwenye mwambao wa Bahari ya Mediterania.” Aliongeza, "Hatutakubali kuwepo kwa dola ya Khilafah hapa au Lebanon, na tutafanya kazi ili kuhakikisha usalama wa Israel."
Hata hivyo, itasimama, Mwenyezi Mungu akipenda, dhidi ya matakwa yao, na itawaondoa katika ardhi hii safi, hasa kwa vile Hizb ut Tahrir, chama kilichojitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na chenye ukweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ndicho kinachoongoza juhudi za kusimamisha Khilafah pamoja na watu ambao ni wakweli kwa ahadi yao na Mwenyezi Mungu, na ambao wanahakikishiwa ushindi wa Mwenyezi Mungu:
[وَاللّٰهُ غَالِبٌ عَلَى أَمرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]
10 Rabii’ Al-Awal 1447 H
2/9/2025 M