Jumamosi, 29 Safar 1447 | 2025/08/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Matukio nchini Armenia na Azerbaijan

(Imetafsiriwa)

Swali:

Uwepo wa Urusi katika Caucasus Kusini umetikiswa “kufuatia Armenia na Azerbaijan kutia saini tamko la pamoja na Marekani juu ya suluhisho la amani na makubaliano katika maeneo ya biashara na usalama baada ya mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka 35 kati ya nchi hizo mbili jirani...” (Al Jazeera, 15/8/2025). Azerbaijan na Armenia zilitoa taarifa ya pamoja mnamo tarehe 11/8/2025, kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini kati yao jijini Washington mnamo tarehe 8/8/2025, yakizitaka pande nyingine kufunga Kundi la Minsk lililoundwa mwaka 1992 ili kutatua masuala kati ya nchi hizo mbili. Iliweka wazi kufunguliwa kwa mafungamano kati yao kwa usafiri wa ndani, baina ya nchi mbili na kimataifa. Hili lilifikiwaje wakati ambapo mahusiano kati yao yalikuwa ya mvutano na yakiathiriwa na vita, hasa katika nyakati za hivi karibuni? Malengo yake yalikuwa yapi? Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu:

Ili kupata jibu la wazi, hebu tuhakiki nukta zifuatazo:

1- Mnamo tarehe 9/8/2025, ukurasa wa Armen Press Arabic ulichapisha maandishi ya makubaliano yaliyotiwa saini na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbajan Ilham Aliyev mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House jijini Washington, D.C. Ilisema: “Kuanzishwa kwa maandishi yaliyokubaliwa ya makubaliano ya kuanzishwa kwa amani na mahusiano ya kimataifa baina ya nchi mbili, Azerbaijan na Armenia, na kuendelea kwa juhudi zaidi kufikia mwisho wa kutia saini, kusisitiza uhifadhi na uimarishaji wa amani kati yao, na kupanga njia ya siku zijazo ambayo haitaamuliwa na mizozo ya zamani, kwa mujibu wa Hati ya Umoja wa Mataifa na Azimio la Alma-Ata la 1991, ambalo ni tamko linalohusiana na makubaliano ya kuweka mipaka kati ya nchi hizo mbili baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, na kujitenga kwa Azerbaijan na Armenia na kutokana nao, kutambuana baina yao, na kuheshimu ubwana, na kutotumia nguvu kusuluhisha mizozo. Pande hizo mbili zilisisitiza tena umuhimu wa kufungua mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya usafiri wa ndani, baina ya nchi hizo mbili na kimataifa, kwa kuzingatia heshima ya ubwana, hadhi ya eneo, na mamlaka ya nchi, ili kuendeleza amani, utulivu na ustawi.” Juhudi hizi zitajumuisha mawasiliano yasiyozuiliwa kati ya sehemu kuu ya Azerbajan na Mkoa unaojitawala wa Nakhichevan (Nakhchivan) kupitia eneo la Armenia.")

Kwa hivyo, makubaliano hayo yalilenga kufungua mawasiliano, uchukuzi na barabara kati ya nchi hizo mbili, kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili. Eneo la Nakhchivan ya Azerbaijan halijaunganishwa nayo, na limekatwa na Armenia. Ili kuungana, Waazerbajani lazima wapite Iran. Makubaliano hayo yanataka kufunguliwa kwa barabara kati ya Azerbaijan na eneo lake la Nakhchivan. Pia yanataka kufunguliwa barabara kati ya Azerbajan na Uturuki, kwani Armenia iko katikati yao. Mawasiliano ya ardhini yanawezekana tu kupitia Armenia. Kwa njia hii, Amerika inaweza kuimarisha ushawishi wake nchini Azerbaijan, kupanua ushawishi wake nchini Armenia, na kudhoofisha au kuondoa ushawishi wa Urusi huko.

2- Makubaliano hayo pia yalibainisha, kama ilivyochapishwa na ukurasa wa Armen Press Arabic mnamo tarehe 9/8/2025, kwamba (“Armenia itafanya kazi na Marekani na kukubaliana pande tatu kuamua mfumo wa utekelezaji wa mpango wa mawasiliano kupitia kile kiitwacho ‘Trump Road to International Peace and Prosperity’ (TRIPP) katika eneo la Armenia. Tovuti ya Eye iliripoti mnamo tarehe 14/7/2025, kwamba “Marekani imependekeza kuchukua ukanda wa usafiri uliopangwa kati ya Armenia na Azerbaijan katika jitihada za kuendeleza mazungumzo ya kidiplomasia yaliyokwama kwa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili ya Caucasus, balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack, aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Ijumaa.” Tovuti ilinukuu kauli ya Barrack kuhusu barabara ya kilomita 32 akisema: “Wanashinda kuhusu kilomita 32 za barabara, lakini hili si jambo dogo. Limejikokota kwa muongo mmoja - kilomita 32 za barabara…Kwa hivyo kinachotokea ni kwamba Amerika inaingia na kusema: ‘Sawa, tutaichukua. Tukodisheni hizo kilomita 32 za barabara kwa miaka mia moja na nyote muitaitumia pamoja.”

Hii itaimarisha ushawishi wa Amerika katika nchi zote mbili. Hii inathibitishwa na kile Reuters iliripoti mnamo 8/8/2025, kwamba Armenia imekubali mpango wa Trump wa kukodisha ukanda wa mawasiliano na Jamhuri ya Azerbaijan kwa miaka 100, ikionyesha kuwa Marekani inataka kulazimisha matakwa yake juu ya mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia. Ya kwanza, kwa msaada wa Uturuki, inatafuta kufungua barabara kuelekea eneo lake la kijiografia la Nakhchivan. Armenia inaona makubaliano haya kama fursa ya kupata ulinzi wa Marekani dhidi ya shambulizi lolote linaloweza kufanywa na jirani yake, Azerbaijan, huku Urusi ikishindwa kuiunga mkono katika vita vya hivi majuzi. Armenia ilishindwa na jamhuri yake katika mkoa wa Nagorno-Karabakh, ambayo waliitangaza miaka 35 iliyopita kwa msaada wa hapo awali kutoka kwa Urusi, ikaanguka.

3- Tovuti ya Middle East Eye iliripoti kwamba "Azerbaijan imesisitiza kwamba ukanda huo haupaswi kuwekwa chini ya udhibiti kamili wa Armenia." Pia ilisema kwamba "Uturuki imehimiza kimya kimya…[kutiwa saini] kwa makubaliano ya amani... Uturuki ambayo awali ilipendekeza wazo la kampuni ya kibinafsi, iliyoidhinishwa na Armenia na Azerbaijan, kusimamia ukanda huo."

Erdogan alimpokea Rais wa Azerbaijan Aliyev mnamo tarehe 19/6/2025, na siku iliyofuata akampokea Waziri Mkuu wa Armenia Pashinyan, ambaye ziara yake nchini Uturuki ilizingatiwa kuwa ya kihistoria. Afisi ya Rais wa Uturuki iliripoti kwamba “Erdogan alisisitiza ‘umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya amani yanayoendelea kati ya Azerbaijan na Armenia... na kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa ndani ya mfumo wa mchakato wa kusawazisha mahusiano kati ya Uturuki na Armenia...” (Al Jazeera, 21/6/2025). Kwa hivyo, tunaona kwamba Erdogan amejitayarisha kutia saini mkataba huo kwa niaba ya Amerika. Yuko katika muznguko wa Amerika na anaipatia huduma za kupanua ushawishi wake katika eneo hilo kwa kubadilishana na usaidizi wake katika kusalia madarakani, na kwa Uturuki kufaidika na harakati za biashara ya ardhini kupitia Armenia hadi Azerbaijan.

4- Makubaliano hayo yalieleza kuwa (“walitoa shukrani zao za dhati kwa Rais Trump wa Marekani kwa kuandaa mkutano wao wa kilele na kuchangia kwa kiasi kikubwa mchakato wa kusawazisha mahusiano ya nchi hizo mbili”). Rais Trump wa Marekani alitaka kuangazia nafasi ya nchi yake na dori yake binafsi hasa, kwani anapenda kujitokeza na kudai kila mafanikio kwa jina lake, akidai kuwa ana uwezo wa kufikia amani na ustawi. Hivyo basi, barabara itakayojengwa kati ya Azerbaijan na eneo lake la Nakhchivan kupitia Armenia ilipewa jina lake (Trump Road). Kwa kuhitimisha makubaliano haya kati ya nchi hizi mbili, Trump pia anatarajia kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel, ambayo aliteuliwa na Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Munir Asim, na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Netanyahu. Ni muhimu kutaja kwamba amani na ustawi ambao Trump anadai kuwa anafanya kazi ili kuufikia inamaanisha kufikia maslahi ya Marekani, kupanua ushawishi wake na udhibiti wake juu ya maeneo mbalimbali ya dunia, na kurejesha ukuu wake, alipokuwa akizindua kauli mbiu “Amerika Kwanza” na “Ifanye Amerika kuwa Tukufu (MAGA).”

5- Makubaliano hayo yanasema kuwa (“Waliotia saini makubaliano hayo walitoa wito kwa dola zinazo shiriki za Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya na miundo husika kuhusu Minsk kukubali uamuzi huo”). Kwa maana nyengine, Trump analazimisha dola zengine katika Kundi la Minsk kukubali uamuzi huu wa Marekani bila ushiriki wao au hata mashauriano, na bila ya kuwapa thamani yoyote au umakini. Hii ni kweli hasa kwa Urusi na Ufaransa, ambazo zinashiriki uongozi wa Kundi la Minsk pamoja na Amerika, ambalo liliundwa kutatua tatizo la Azerbajan-Armenia mnamo 1992 kwa uamuzi wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya! Marekani ilitia saini mkataba huu bila ya kutegemea Urusi na kuupanga kabla ya mkutano wa Rais Trump na mwenzake wa Urusi, Putin, ili kuepusha pingamizi yoyote kutoka kwa Urusi, ambayo inapaswa kuhusika katika suala hilo kwani ina ushawishi katika eneo hilo, haswa nchini Armenia, baada ya kupoteza ushawishi wake nchini Azerbaijan, na kama mmoja wa viongozi wa Kundi la Minsk. Aliomba, kama alivyowataka wengine katika kundi, kutambua na kubariki makubaliano haya. Badala ya Urusi kuingilia kati na kupinga, haikufanya chochote kuonyesha udhaifu wa msimamo wake na udhaifu wa ushawishi wake, ambao unakaribia kutoweka nchini Armenia.

6- Inaonekana kwamba Urusi haiko katika nafasi ya kuingilia kati na kupinga kwa nguvu, hivyo kuishawishi Armenia kuizuia kuimarisha zaidi uhusiano wake na Amerika. Imependelea kuambatana na hali hiyo, kana kwamba imeridhika na kile kinachotokea, huku ikituma maonyo kwa Armenia ili kuepuka kuipoteza kabisa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova alisema, “Kwa hiyo, mkutano kati ya viongozi wa jamhuri za Caucasus Kusini jijini Washington, uliowezeshwa na Marekani, unastahili tathmini chanya. Tunatumai hatua hii itaendeleza ajenda ya amani.” Walakini, alisisitiza “mazungumzo ya moja kwa moja bila upatanishi wa mtu wa tatu.” na kuonya kuwa “Ushirikishwaji wa watendaji nje ya eneo unapaswa kuchangia katika kuimarisha ajenda ya amani badala ya kuunda matatizo ya ziada na kugawanya mistari.” (Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi; Al Jazeera, 9/8/2025). Kwa maana nyengine, anaonya dhidi ya kupenya kwa ushawishi wa Amerika huko. Hapo awali Armenia ilikuwa imeonywa dhidi ya kushirikiana na Magharibi. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema mnamo tarehe 24/7/2025, kwamba (“Wakati Armenia ina haki ya kuchagua mwelekeo wake wa kisiasa, Moscow inatarajia kuepuka marudio ya mabadiliko ya kijiografia yanayoshuhudiwa nchini Ukraine.” Alisisitiza kwamba “Urusi bado inaichukulia Armenia kuwa mshirika na inataka iendelee kushirikiana nasi.” Ukraine, ambapo Urusi ilipoteza ushawishi wake kufuatia kuanguka kwa kibaraka wake Yanukovych mwaka wa 2014 baada ya Marekani na Ulaya kuwachochea Waukraine kumuasi Mwaka jana, Waziri Mkuu wa Armenia Pashinyan alitangaza katika mahojiano na France 24 mnamo tarehe 23/2/2023, (“ufungiaji kivitendo wa ushiriki wa Armenia katika Shirika la Mkataba wa Usalama linaloongozwa na Urusi... kwa sababu haijafikia malengo yake kuhusiana na Armenia”).

Urusi haikuilinda Armenia wakati Azerbajan ilipoishambulia mwaka wa 2020 na 2023, na kuilazimisha iondoke katika maeneo iliyokuwa inamiliki nchini Azerbaijan. Tulikuwa tumetaja katika Jibu la Swali lililotolewa tarehe 4/10/2023 kwamba (Urusi imetambua zaidi kwamba vita hivi vinaelekezwa na kupangwa dhidi yake na Marekani kupitia Uturuki ya Erdogan na Azerbaijan, ambayo imekuwa mlinzi wake, na itaikalia bila mafanikio na kutawanya majeshi yake. Sasa inaangazia vita vyake nchini Ukraine, ambavyo ni vita vya hatari ikiwa haitaki kushindwa. Urusi inajua kuwa ikiwa itashindwa, itapoteza kila kitu, na ikiwa itashinda, itaweza kuregesha ushawishi wake katika maeneo ambayo imepoteza. Wakati huo huo, haitaki kugongana na Uturuki, ambayo inaihitaji katika dhurufu hizi na kikwazo ilichowekewa juu yake. Ndio lango lake la kuingia ulimwengu wa Magharibi. Pia inataka kudumisha mahusiano yake na Azerbaijan, kwani iko na uwekezaji wake huko, haswa katika sekta ya rasilimali za kawi zenye thamani ya worth $6 bilioni. Kiwango cha ubadilishanaji wa biashara kati yazo ni zaidi ya worth $ 4 bilioni. Ama kuhusu Armenia, inaitegemea kwa kila kitu... hakuna uwezekano kwamba itairegesha ushawishi wake kamili kama ulivyokuwa ikiwa itashinda vita nchini Ukraine).

7- Amerika imepuuza Ulaya, haswa Ufaransa, ambayo inaongoza Kundi la Minsk. Kwa hivyo Trump ameitelekeza Ulaya, ikiongozwa na Ufaransa, kama alivyofanya kwa Urusi, akiachia suala hilo kwa vyombo vyake mwenyewe. Hakika, Azerbajan na Armenia zimetoa barua ya pamoja ya kutaka kuvunjwa kwa Kundi la Minsk. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Azerbajan mnamo 11/8/2025, ilisema, (“Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo mbili walituma barua ya pamoja kwa Mwenyekiti wa Afisi ya OSCE kusitisha Kundi la Minsk.” “Kufuatia wito huu, rasimu ya azimio la kukomesha mchakato wa Minsk na miundo inayohusiana nayo ilisambazwa kati ya nchi shiriki za OSCE.” Ilitoa wito kwa “Shirika la Habari la Azerbaijan kuunga mkono uamuzi huu wa Azerbaijan.” 11/8/2025). Kwa hivyo, Amerika inaondoa ushawishi wowote wa Ulaya juu ya suala hili, ikiruhusu kudhibiti suala hilo na kupanua ushawishi wake huko haraka, ikijumuisha ("kuondoa madai na mizozo yote ya pande zote kati yao katika kiwango cha kimataifa, kama ilivyoainishwa katika makubaliano” (chanzo hicho hicho). Ufaransa ililazimishwa kutangaza kukubali kwake kuvunjwa kwa Kundi la Minsk na haikuwa na dori au ushawishi tangu 2020, baada ya Azerbaijan kutangaza vita dhidi ya Armenia na kisha kuyarudisha maeneo yake, ambayo Kundi la Minsk halikunufaika na kuyarudisha, kwani kundi hilo lilidai kuwa linafanyia kazi hili kwa njia za amani. Ufaransa ilianza kuipeti Amerika ili isionekane kuwa imeshindwa na inatafuta dori ya kucheza huko. Inadai kuwa inaunga mkono makubaliano hayo, licha ya kuwa ndiyo iliyowaunga mkono waziwazi Waarmenia dhidi ya Azerbaijan.

8- Trump pia aliipuuza Uturuki, ambayo ilikuwa ikisubiri rais wake, Erdogan, kutuzwa kwa huduma yake kwa kumwalika Washington kuhudhuria kutiwa saini kwa makubaliano hayo. Erdogan alicheza dori kubwa katika kuunga mkono Azerbaijan na kuiwezesha kuishinda Armenia na kukomboa maeneo yake yaliyokaliwa, shukrani kwa mipango ya Amerika. Lakini hata hili lilichukiwa na Trump, kwani hakuona haja ya kukamilisha makubaliano haya. Vyenginevyo, angemwita Erdogan Washington, au kumtaka aongee kwa simu na Rais wa Azerbaijan Aliyev, kama alivyomtaka aongee kwa simu na Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa wakati wa mkutano wake naye jijini Riyadh mnamo 13/5/2025, ili kutekeleza matakwa ya Amerika. Lakini katika makubaliano ya Armenia-Azerbaijan, alimpuuza! Kwa hivyo, wakoloni makafiri huvuna matunda, huku wengine wanaozunguka katika mzunguko wao au vibaraka hulima na kuhangaika kwa ajili ya malipo yao ya kubaki madarakani. Na hata hili halifanyiki kila wakati. Basi, hawatii akili?!

Ahmad on the authority of Hudhayfah, who said: The Messenger of Allah (saw) said:

9- Trump ana shauku kubwa ya kudhihirisha ukuu wa Marekani na ukuu wake mwenyewe, na kwamba yeye ndiye mtu pekee duniani anayeweza kuleta amani na kukamilisha kazi ngumu, kupigana vita vya kiuchumi dhidi ya maadui na marafiki, na kuanzisha vita vya umwagaji damu moja kwa moja au kupitia umbile la Kiyahudi, kama alivyofanya hivi karibuni nchini Iran. Anaunga mkono kwa uwazi umbile la Kiyahudi katika kuua, kuwaweka njaa na kuwahamisha watu wa Gaza bila aibu wala uoga wowote ili kufanikisha mradi wake wa kuigeuza kuwa mji wa kitalii na bila ya mtu yeyote kuingilia kati kukomesha mauaji ya halaiki huko au kuleta kipande cha mkate kwa njia ifaayo! Alisahau kwamba Mwenyezi Mungu aliangamiza kabla yake vizazi vya watu waliokuwa na nguvu zaidi, wengi zaidi, na wauaji zaidi “kuliko yeye na nchi yake, Marekani, na kambi yake, umbile la Kiyahudi.” Alisahau au akajifanya kusahau kwamba Ummah wa Kiislamu, hata kama utapata ukandamizi, kutiishwa, na dhulma kiasi gani kutoka kwa watawala wake, washirika wa makafiri, utainuka na kuasi dhidi yao, kuwapindua, na kukabidhi mamlaka yake kwa anayestahiki miongoni mwao kuutawala kwa mujibu wa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, na hivyo kuiregesha Khalifah Rashida baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi ndani yake, katika kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadith yake tukufu iliyopokewa na Ahmad kutoka kwa Hudhayfah, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

“Kisha kutakuweko na utawala wa kidhalimu (ملكًا جبرية), na utadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa akipenda kuuondoa. Kisha kutakuwa na Khilafah katika njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza. Na utapeleka ujumbe wake duniani na kuueneza, kama ilivyoelezwa katika Hadith tukufu iliyopokewa na Ahmad kutoka kwa Tamim al-Dari, ambaye amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ، وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ، بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ؛ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ، وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْر»

“Jambo (Uislamu) hili kwa yakini litafika kila panapofikiwa na usiku na mchana, na Mwenyezi Mungu hataiwacha nyumba ya matofali, ya udongo wala hema la manyoa ya ngamia isipokuwa Mwenyezi Mungu ataiingiza Dini hii, kwa izza ya mwenye izza au kwa udhalilifu wa mdhalilifu; izza ambayo kwayo Mwenyezi Mungu atawapa wakaazi wake wenye kubeba Uislamu, na udhalilifu ambao Mwenyezi Mungu atawapa wakaazi wake wenye kubeba ukafiri” hili inshaAllah litatokea.

[إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3]

22 Safar 1447 H

16/8/2025 M

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Jibu la Swali: Matukio Mjini Al-Suwayda

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu