Alhamisi, 19 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mtihani wa Gaza

(Imetafsiriwa)

https://www.al-waie.org/archives/article/19956

Jarida la Al-Waie, Toleo 469

Mwaka wa Thalathini na Tisa, Safar 1447 H, sawia na Agosti 2025 M

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[الٓمٓ ١ أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن يُتۡرَكُوٓاْ أَن يَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا يُفۡتَنُونَ ٢ وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَٰذِبِينَ]

“Alif, Lam, Meem. (1) Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? (2) Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo. (3)” [Surah Al-Ankabut: 1-3].

Ibn Kathir asema katika tafsiri yake ya Aya hii tukufu, “Ama maneno Yake, “Je, watu wanadhani kwamba wataachwa peke yao na kusema, “Tumeamini” na wala hawatajaribiwa?” Kuhusu, “Na hawatajaribiwa?” Hili ni swali kwa mtindo wa kukanusha na maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Aliyetukuka, bila shaka atawajaribu waja Wake Waumini kulingana na kiwango cha Imani walicho nacho, kama ilivyoelezwa katika Hadith Sahihi, «أَشَدُّ النَّاسِ بَلَاءً الْأَنْبِيَاءُ ثُمَّ الصَّالِحُونَ، ثُمَّ الْأَمْثَلُ فَالْأَمْثَلُ، يُبْتَلَى الرَّجُلُ عَلَى حَسَبِ دِينِهِ، فَإِنْ كَانَ فِي دِينِهِ صَلَابَةٌ زِيدَ فِي الْبَلَاءِ»Watu wenye kupewa mitihani mizito ni Manabii (as), kisha wachaMungu, kisha wanaofuata kwa ubora na kisha wanaofuata kwa ubora. Mtu hujaribiwa kulingana na kujitolea kwake katika Dini. Ikiwa kujitolea kwake katika Dini ni thabiti, itaongezewa mtihani.”

Mwenyezi Mungu (swt) hakumuumba mwanadamu bila ya kuweka mbele yake mitihani kulingana na ukubwa wa Imani yake na kujitolea kwake katika Dini, ili Mwenyezi Mungu (swt) apate kujua ni nani atakayekuwa na subira mbele ya mitihani hiyo na kuweka tegemeo lake (tawakkul) kwa Mwenyezi Mungu (swt) . Haya ni ili Mwenyezi Mungu (swt) amuepushe na fitna. Ama wale ambao watafeli ndani ya mitihani hiyo, watafeli tu kwa sababu ya hukumu yao mbaya, kughafilika kwao na Amri za Mwenyezi Mungu (swt), na Imani yao dhaifu.

Miongoni mwa mitihani hii ambayo imeupata Umma mzima hivi leo ni mtihani wa Gaza, ikiwemo yanayotokea huko, na msimamo wa Waislamu kwake kutoka Mashariki na Magharibi. Waislamu wengi, na hapa tunamaanisha Waislamu, sio wanafiki, wahalalishaji mahusiano na Mayahudi, walioghafilika, au wale wanaofuata njia ya makafiri, wanasema, ‘Lau Hamas isingefanya ilichofanya, yasingetokea yaliyotokea, na mauaji haya makubwa ya watu wake yasingetokea Gaza, pamoja na kuharibiwa kwa nyumba zake na njaa ya watu wake.’ Kisha wanaongeza, ‘Watu wa Gaza walikuwa na maisha.’

Ni kana kwamba Muislamu ameumbwa ili tu ale na kuzaa kama wanyama wanavyofanya, Mwenyezi Mungu (swt) atulinde sote. Hakika huu sio uhalisia wa Waislamu, na wala sio moja ya malengo yao, isipokuwa kwa wale wanaokubali kuishi maisha ya wanyama. Hatuwezi kuwachukulia watu wa aina hiyo kuwa ni wenye kufahamu Waislamu wanaojitahidi kunyakua fahari na utu wao kutokana na vituko vyenye madhara vya maadui zao. Mwenyezi Mungu (swt) alitupa mifano miwili ya hivi karibuni, kabla na wakati wa matukio ya Gaza, kama funzo kwa watu. Mnamo 6 Februari 2023, maeneo ya Uturuki na Syria, ambayo ni Kahramanmaraş na Maraş, yalikaribia kuangamizwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha mamia ya majengo ya makaazi kuanguka juu ya vichwa vya wamiliki wa maeneo hayo mawili. Wahasiriwa hao walifikia makumi ya maelfu, huku 44,212 wakiwa wamekufa kwa upande wa Uturuki na 5,914 waliokufa kwa upande wa Syria, kwa jumla vifo zaidi ya elfu hamsini katika muda wa sekunde! Miezi saba baadaye, usiku wa Septemba 10 na 11, mabwawa mawili katika eneo la Derna nchini Libya yalibomoka kufuatia kimbunga Daniel. Hii ilisababisha takriban mita za ujazo milioni 30 za maji kutiririka kuelekea makaazi ya watu kando ya mto, na kusababisha vifo vya takriban watu 4,333. Haya ni matokeo ya awali kutoka kwa janga hili chungu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu wote.

Kuanzia hapa tunaelewa kwamba watu, kibinafsi na kwa pamoja, wako wazi wakati wowote kwa kifo kwa njia mbalimbali. Wale waliokufa katika tetemeko la ardhi na mafuriko hawakuwa kwenye uwanja wa vita, wala hawakuinua silaha zao dhidi ya adui zao. Badala yake, walikuwa wamelala fofofo, wakiota kesho nzuri. Basi kwa nini walikufa wote mara moja? Hayo ni Mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) husimamia mambo ya waja wake apendavyo na kwa namna atakavyo. Kwa hivyo idadi kubwa ya mashahidi wetu mjini Gaza sio sababu ya sisi kuwalaumu mujahidina wa huko kwa yale waliyoyafanya katika kumdhalilisha adui, kuharibu viwango vyao vyote vya ulinzi, kuwachukua mateka kwa nguvu, na kuua idadi kubwa ya askari wao waoga, na kufichua aibu ya hali dhaifu ya wale waliomkasirisha Mwenyezi Mungu, ambayo isingekuwepo na kubakia lau si kwa ulaji njama na khiyana ya watawala wa Waislamu katika eneo hilo, na watawala saliti walio mbali nao wanaozidhibiti nchi nyingine za Kiislamu.

Yeyote miongoni mwa Waislamu waliokufa huko Gaza, alikufa mwishoni mwa muda wa uhai (ajal) waliowekewa na Mwenyezi Mungu (swt), bila ya kuzidisha au kupungua, huku akipata heshima ya kifo cha kishahidi mikononi mwa adui muoga na mwenye khiyana. Kwa wale wanaolaani vitendo vya mujahidina kwa msingi wa idadi kubwa ya waliokufa, tunasema, watu wote hawa wangeweza kufa katika tetemeko la ardhi kama lile la Uturuki, au kuzama katika tsunami ya kutisha kama ilivyotokea miaka iliyopita huko Indonesia, ambapo karibu watu 227,000 waliuawa. Idadi ya mashahidi mjini Gaza sio hoja kwetu sisi kupinga amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ya kulinda mambo ya waja wake hapa duniani. Kuanzia hapa, ni lazima tujichunguze katika msiba huu mkubwa. Je, ninajishughulisha na Gaza na kusimama nayo, au ninashughulishwa nayo na kuipuuza, kuwalaumu watu wake, kuwashambulia wao na matendo yao, na kudunisha waliyoyafanya?

Ewe Mwenyezi Mungu (swt), tuonyeshe haki kuwa ni haki na utuwezeshe kuifuata, na utuonyeshe batili kuwa ni batili na utuwezeshe kuiepuka.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu