- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Swahaba Mtukufu Mus’ab ibn Umair, Mwenyezi Mungu (swt) Amuwie Radhi
Mu’nis Hamid, Iraq
(Imetafsiriwa)
https://www.al-waie.org/archives/article/19949
Jarida la Al-Waie, Toleo 469
Mwaka wa Thelathini na Tisa, Safar 1447 H, sawia na Agosti 2025 M
Katika kundi la majina yenye kung'aa ya maswahaba watukufu, jina la Mus’ab bin Umair (ra) linajitokeza kama ishara ya muhanga na uthabiti. Mus’ab alikuwa mshika mwenge wa Da’wah katika hatua zake zote, kwani alikuwa ni kijana miongoni mwa vijana bora wa Makka, aliyejulikana kwa uzuri wake, harufu ya kupendeza, na maisha ya anasa, kiasi kwamba Maswahaba, Mwenyezi Mungu (swt) awawie radhi wote, wakasema juu yake, ما رأينا بمكة أحدا انعم عيشا من مصعب بن عمير “Hatujamuona mtu yeyote mjini Makka ambaye aliishi kwa neema kuliko Mus’ab bin Umair.”
Swahaba huyu mtukufu alisilimu mwanzoni mwa Da’wah ya siri, iliyeathiriwa na Da’wah ya Mtume Muhammad (saw), licha ya hadhi yake ya kijamii na kubahatika. Mama yake, Khunas binti Malik, alipogundua kwamba amesilimu, alipinga vikali kusilimu kwake, na hata akamfunga ndani ya nyumba yake kwa ajili ya kumzuia asikutane na Mtume (saw). Hata hivyo, alibaki imara katika dini yake na akatoka akiwa na imani zaidi, nguvu, na azma zaidi. Baada ya Ba’yah ya Kwanza (Kiapo cha Utiifu) pale Aqabah, Mtume (saw) alimchagua kuwa Daee (mbebaji dawah) na balozi wa kwanza wa Uislamu mjini Madinah. Alipata heshima ya kuwa wa kwanza kuanzisha kiini cha kwanza cha umma wa Kiislamu (jamaa ́ah) hapo. Miongoni mwa watu mashuhuri zaidi waliosilimu mikononi mwake mjini Madina ni, As`ad ibn Zararah, Sa`d bin Mu`adh, na Asid bin Hudayr, Mwenyezi Mungu (swt) awe radhi nao wote. Wote wakawa nguzo katika kujenga dola ya kwanza ya Kiislamu. Swahaba huyu alishiriki katika Vita vya Badr na alikuwa mshika bendera wa Waislamu huko Uhud, ambapo alipigana vyema mpaka akauawa shahidi, huku akimhami Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mikono yake ilikatwa akiwa ameshika bendera, basi bendera ikaanguka na kuinuliwa na Maswahaba watukufu. Alipopatikana, hawakupata sanda kamili ya mwili wake safi, kwa hivyo ikiwa wakifinika kichwa chake, miguu yake inakuwa wazi, na wakifinika miguu yake, kichwa chake kinakuwa wazi.
Ndiyo, Imani inaweza kubadilisha njia ya mtu kutoka maisha ya anasa hadi njia ya kujitolea kwa ajili ya maadili. Vijana wana uwezo wa kubeba majukumu makubwa ya kulingania Uislamu, kwa ajili ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Mus’ab, Mwenyezi Mungu (swt) awe radhi naye, ni kielelezo angavu na kielelezo cha jinsi neno jema linavyoweza kufungua nyoyo, na kuleta mabadiliko kwa wale wanaotaka mabadiliko.
Wasifu wa Mus’ab sio tu hadithi ya Swahaba yeyote peke yake, bali ni somo la kina katika uthabiti, uaminifu na ikhlasi. Aliishi maisha mafupi lakini yalikuwa yamejaa ushawishi mzuri. Ndiyo, alikuwa kweli balozi wa kwanza wa Uislamu, mmoja wa waanzilishi wa mabadiliko ya kweli mwanzoni mwa Dini hii. Hebu na tuwashe moto wa Iman katika nyoyo zetu, na tuibebe Rayah (bendera) kama alivyoibeba Mus’ab, na tuyafanye maisha yetu yawe ni risala, sio mapumziko, na siku zetu ziwe ni miale ya Da’wah, sio viti vya kupumzikia... kuwa Mus’ab wa zama hizi... kwani Ummah bado unangoja...