Ijumaa, 28 Ramadan 1446 | 2025/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanawake Waliofaulu katika Uislamu wana Sifa hizi

(Imetafsiriwa)

Kila Muislamu anataka kufanikiwa katika maisha haya na yajayo; hata hivyo, ili kufikia hili, ni lazima tufahamu nini mafanikio katika Uislamu.

[وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ]

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.” [Surah An-Nur; 24:52]

Kutokana na dalili hii, tunaweza kuona kwamba mafanikio hayakufungwa katika ufafanuzi kwa mwanamume au mwanamke.

Kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) na kuwa na taqwa (kumcha Mungu (swt)).

Kwa kuzingatia hili sisi kama wanawake wa Kiislamu katika Uislamu tunaweza kumtazama Mtume (saw) kama kielelezo cha mafanikio, kama mfano wa kuigwa kwa wanadamu. Pia tunao wanawake watukufu wa Kiislamu ambao walidhaminiwa Jannat. Ashara Mu’bashireen walioahidiwa Jannah walikuwa 10 na kutoka kwao 4 walikuwa wanawake;

1. Khadija Bint Khuwaylid (ra). Alikuwa mke wa kwanza wa Mtume (saw) na mfuasi wake imara kabisa, ambaye mara nyingi hujulikana kama "Mama wa Waumini."

2. Maryam binti Imran (ra). Hakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mtume (saw) lakini anaheshimika sana katika Uislamu kama mama yake Nabii Isa (Yesu, amani iwe juu yake).

3. Asiyah Bint Muzahim (ra). Hakuwa na udugu na Mtume (saw) lakini anaheshimika katika Uislamu kama mke mwema wa Firauni na mmoja wa wanawake wanne wakubwa katika mila ya Kiislamu.

4. Fatima Bint Muhammad (ra). Alikuwa binti kipenzi cha Mtume (saw) na ni mmoja wa wanawake wenye heshima kubwa katika Uislamu.

Tunapowaangalia wanawake waliodhaminiwa Jannat, tunapaswa kuelewa kwamba mafanikio yao hayakuhusiana na jina au cheo.

Katika Uislamu, hakuna fahamu ya kuingia Jannat kulingana na nani unamjua na hadhi yako ya kidunia ni ipi. Wote walisifiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu ya sifa zao za pamoja za kuwa karibu katika utendaji wao wa kuwa kama mfano wa Mtume (saw). Ikiwa tunataka hadhi sawa ya kuingia Jannat lazima basi tufuate mfano wao wa kufanikiwa. Sifa zifuatazo basi zinahitajika.

Khadijah Bint Khuwaylid

Imani na uungaji mkono usioyumba – Yeye (ra) alimwamini Mtume (saw) tangu mwanzo kabisa na akamuunga mkono kwa moyo wote katika utume wake.

Kujitolea mhanga kwa ajili ya Uislamu – Alitoa mali na rasilimali yake kumsaidia Mtume (saw) na Waislamu wa mwanzo.

Huruma na hekima – Alijulikana kwa tabia yake ya upole na ushauri wa busara, akiakisi huruma ya Mtume (saw).

Maryam Bint Imran

Kujitolea katika ibada – Yeye (ra) alijitolea sana kwa maombi yake na uhusiano na Mwenyezi Mungu, akiakisi kujitolea kwa Mtume (saw) katika ibada.

Utakatifu na kujihifadhi na machafu – Alishikamana na viwango vya juu vya maadili, akiishi maisha ya uongofu na ya kuwa na haya.

Uvumilivu katika mitihani – Alistahamili hukumu ya jamii kwa imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu, akionyesha ustahamilivu katika shida.

Asiyah Bint Muzahim

Imani katika kukabiliana na ukandamizaji – Yeye (ra) alibakia kuwa muumini wa Mwenyezi Mungu (swt) licha ya kuolewa na Firauni, dhalimu mkandamizaji zaidi.

Ujasiri na uthabiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) – Alisimama imara katika imani yake na akatafuta malipo ya Mwenyezi Mungu, akiiga uimara wa Mtume katika dhiki.

Upole na unyenyekevu – Licha ya wadhifa wake kama mke wa Firauni, aliendelea kuwa mnyenyekevu na kutafuta rehema za Mwenyezi Mungu (swt).

Fatima Bint Muhammad

Uchamungu na haya – Yeye (ra) alitoa mfano wa tabia za Muislamu mchamungu, akiiga unyenyekevu na haya ya babake, Mtume (saw).

Kujitolea kwa familia – Alionyesha upendo mkubwa na utunzaji kwa familia yake, akifuata mfano wa Mtume wa huruma na uwajibikaji.

Uvumilivu katika shida – Alivumilia mapambano ya kuwa sehemu ya nyumba ya Mtume kwa subira na neema.

Kutokana na mifano hii mitukufu, tunaweza kutumia orodha hii kwa maisha yetu ya kila siku kama wanawake wa Kiislamu wanaojitahidi kupata mafanikio!

[وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ]

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.” [Surah An-Nur; 24:52]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohamed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu