Ijumaa, 28 Ramadan 1446 | 2025/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafanikio ya Kweli Mpaka Siku ya Mwisho ni kwa Umma wa Kiislamu Pekee

(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu (swt) aliusifu Ummah huu wa Kiislamu kama "umma bora uliotolewa kwa ajili ya Wanadamu".

[Aal-i ‘Imran 110] na akaongeza kusema, [وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَٰكُمْ أُمَّةً وَسَطًا] “Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani...” [Al-Baqarah 143].

Ibn Kathir anafafanua aya “Ummatan Wasatan”, kama “mwenye uadilifu,” “bora zaidi (katika wema au ubora),” “chaguo la juu,” “bora zaidi,” na “ummah (taifa) wenye kuheshimika zaidi. Kwa hivyo, Ummah huu ni "mwenye" kiigizo chema kwa wanadamu. Kwa sababu, ni Ummah huu, ambao unafuata na kuchukua usukani katika kutekeleza, kuongoza na kutengeneza njia ya maisha bora pekee ya mwanadamu, ambayo yameamuliwa na Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wa wanadamu hawa, yeye mwenyewe. Ni sehemu hiyo teule ya wanadamu, ambayo haivuki mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu (swt) (ifrat) au kupungukiwa katika kutimiza wajibu wake uliowekwa na Mwenyezi Mungu (tafrit).

Hivyo, una uwezo wa kusimamisha haki (haqq) na uadilifu (adala). Unafafanua maadili na vima ambavyo humwinua mwanadamu kutoka kwa maumbile duni hadi mauumbile bora zaidi; yaani kutoka kuwa kiumbe anayetenda kulingana na silika (ghariza) na mahitaji yake ya kimwili, hadi kuwa mwanadamu mwenye akili, aliyetimilika, ambaye anaweza kuingiliana kwa amani na watu wengine, mataifa, dini nk. Fikra ya Ummah huu, hukmu yake ndiyo kigezo cha kufikiri, hukmu za thamani, vipimo na matendo. Una usemi wa mwisho juu ya kipi ni "kizuri/kheri" na ni kipi "kibaya/shari". Hiki ndicho kinachoufanya kuwa "WASATAN", ambayo maana yake halisi ni bora, tukufu, heshimika, mashuhuri.

Kwa hiyo, ni nani asiyekubali kwamba hii ndiyo “aina ya mwisho kabisa ya mafanikio” kwa mwanadamu binafsi, na pia Umma mzima?

Hata hivyo, tangu zaidi ya miaka mia moja, tumefanywa kuamini kwamba hatuna uwezo wa kusimamia nyanja yoyote ya maisha ya dunia hii, na hatuwezi kuwa Umma wenye maendeleo na mafanikio. Ukweli ni kwamba, tumepuuzwa na thaqafa ya Kimagharibi, tukitazama mafanikio kulingana na fahamu, desturi, maadili na vima vya mataifa yasiyo ya Kiislamu, wanasiasa, wanafikra na dola, na ambao walifafanua kipimo cha mafanikio kama kufikia demokrasia, uhuru huria, usawa wa kijinsia, na kutii kanuni na makubaliano ya kimataifa. Ukweli ni kwamba, mtazamo huu unatumika tu kututia ulemavu na kubaki chini ya utawala na utashi wa Magharibi. Muhimu zaidi, tumefumbwa macho na watawala wasio na ari na wasio na dhamiri, ambao hutumika kama kichocheo cha ukeketaji wa kiakili na kisiasa, kurudi nyuma kiuchumi, unyonyaji na umaskini katika nchi za Waislamu. Hao ni mabwege wanaoulaumu kwa sauti kubwa Uislamu na Waislamu kwa kila balaa na kufeli, huku wakitufunika sisi kwa hofu zao wenyewe. Hao ndio wapambe wa nchi za Magharibi wanaoponda kila juhudi za Kiislamu kupinga udhalimu wao.

Ni lazima tusafishe akili zetu kutokana na simulizi potofu kwamba Waislamu ni dhaifu au hawana malengo. Kinyume chake! Sisi, Umma wa Kiislamu, tuna mfumo imara sana, wenye nguvu na uwezo ambao unaweza kuhakikisha furaha kwa wanadamu wote (na sio tu kwa wamiliki wachache wa mitaji). Uislamu unahakikisha maendeleo na ustawi mzuri kwa kila mtu binafsi, yaani, sio tu kiuchumi, lakini furaha katika maadili na akhlaki, katika nyanja za ubinadamu, kithaqafa na kisayansi, na kuhakikisha kwamba hili linapatikana kwa kila mtu, bila kujali imani yake, rangi, taifa au jinsia. Uislamu, tofauti na mifumo iliyobuniwa na mwanadamu, unahakikisha maendeleo kwa uwiano na maumbile ya mwanadamu, badala ya kugongana nayo - hiyo ndiyo sababu kuu kwa nini watu katika ulimwengu wa kidemokrasia wa kirasilimali daima wanatafuta mfumo badali wa maisha.

Tumetoa hayo kwa miaka 1300 kwa kila mwanadamu chini ya utawala wetu; na hata nyakati zenye nguvukazi chache, rasilimali kidogo, teknolojia ndogo.

Hata leo, katikati ya misiba isiyohesabika na isiyoweza kuvumilika, Ummah huu umethibitika kuwa thabiti katika kitambulisho chake na hivyo hauwezi kuangamizwa. Imethibitika kuwa unastahiki vyeo ulivyotunukiwa na Mola wa walimwengu, Mwenyezi Mungu Azza wa Jall! Angalia Kashmir, India, Afghanistan... Angalia Waislamu wa Syria, Turkestan Mashariki, Myanmar, katika nchi za Afrika, duniani kote, na mwisho kabisa Waislamu wa Palestina na hasa Gaza! Magaidi hao wa Kizayuni wameshindwa katika kila lengo lao kuhusu Gaza. Ummah huu umethibitisha mara kwa mara, kwamba uwepo wake hauzimiki! Hata adui zake wawe wakatili kiasi gani!

Ni ukweli usiopingika kwamba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, Mtukufu hatunuku cheo hicho adhimu kwa umma wake anaoupenda sana miongoni mwa wanadamu, kisha kuuacha utoweke! Hata hivyo, Yeye (swt) ameambatanisha masharti fulani katika kushikilia cheo hiki cha kipekee cha “umma bora (khayra ummatan) na umma wa kati na kati (ummatan wasatan)”...

Anachotaka tu (swt) kutoka kwetu ni kumtii Yeye pekee.

[ٱتَّبِعُوا۟ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ]

“Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake.” [Al-A’raf 3]. Na Anasema: [ ءَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ ٱللَّهُ] “Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?” [Al-Baqara 140] Hivyo basi, [وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ] “Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume!” [An-Nisa 59].

Na ikiwa hamutafanya hivyo, basi matokeo yatakuwa kama ifuatavyo:

[يَٓا اَيُّهَا الَّذ۪ينَ اٰمَنُٓوا اِنْ تُط۪يعُوا الَّذ۪ينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلٰٓى اَعْقَابِكُمْ فَتَنْقَلِبُوا خَاسِر۪ينَ]

“Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.” [Aal-i Imran 149]. Naye (swt) anatuonya:

[وَمَنْ اَعْرَضَ عَنْ ذِكْر۪ي فَاِنَّ لَهُ مَع۪يشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيٰمَةِ اَعْمٰى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [TaHa: 124].

Neno "DHANKA" hapa sio la kusikitisha tu, lakini ni baya zaidi ya mbaya. Ni kufeli kabisa na kamili, haikufungika tu kwa ulimwengu huu, bali kuenea hadi Akhera! Hata hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu pia ni Mwingi wa kusamehe! Kwa hiyo, njia ya kurudi kwenye mafanikio ni katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na kufuata ujumbe huu wa kipekee:

[الٓمٓ ذَٰلِكَ ٱلْكِتَٰبُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ] “Alif-Lãm-Mĩm. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu!” [Al-Baqara 1-2]

[أُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدًۭى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ] “Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, NA HAO NDIO WALIO FANIKIWA.” [Al-Baqara 5].

Bila shaka, njia iliyo salama ya mafanikio ni kuwaondoa wale wote na kila kitu kinachozuia kumtii Mwenyezi Mungu, na kisha kutekeleza hukmu yake chini ya mfumo mmoja, chini ya Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, ambayo ni dola ambayo imejengwa juu ya misingi, imani, sheria na Nidhamu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuwekea! Na mafanikio hayo yamedhaminiwa na Mwenyezi Mungu (swt)!

[وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao...” [Surah Al-Nur: 55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Wanawake Waliofaulu katika Uislamu wana Sifa hizi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu