Ijumaa, 28 Ramadan 1446 | 2025/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  11 Ramadan 1446 Na: 07 / 1446 H
M.  Jumanne, 11 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mlipuko Pekee katika Njama ya Ugaidi Bandia ni Ufichuzi wa Uongo wake

(Imetafsiriwa)

Polisi wa Serikali ya Majimbo ya Australia wamefichua taarifa tete kuhusu msururu wa matukio ya hivi majuzi ya madai ya chuki dhidi ya Mayahudi, ikiwa ni pamoja na madai ya njama ya ugaidi, yote ni uzushi kabisa wa wahalifu wanaoishi ng'ambo.

Cha kushangaza, saa chache baada ya kugunduliwa kwa gari lililokuwa na vilipuzi huko Dural, polisi wa kupambana na ugaidi tayari walitupilia mbali dhana ya ugunduzi kama huo kuwa tukio la 'majeruhi wengi'.

Lakini hilo halikuwazuia wanasiasa wa serikali na majimbo, na mashirika ya wawakilishi yaliyoathiriwa, hatimaye kuwasha moto wa kile kinachoitwa mlipuko wa chuki dhidi ya Mayahudi nchini Australia, na katika mchakato huo, kuharakisha sheria za kauli za chuki zinazofikia mbali na kuongeza mipango ya ufadhili kwa jamii zilizoathiriwa.

Muhimu zaidi, sauti zinazoiunga mkono Palestina zimechafuliwa kwa njia ya kudumu katika mchakato huo, huku watetezi wa mauaji ya halaiki wakitafuta kwa makusudi kupatiliza unyanyasaji uliokithiri ili kuzima upinzani dhidi ya mauaji ya halaiki.

Mengi yamefichuliwa hadi sasa, lakini mengi zaidi bado hayajajibiwa.

Maswali mazito sasa yanahitaji kuulizwa:

1. Polisi walijua nini hasa kuhusu matukio haya, na ni lini walipata kujua ukweli huu?

2. Polisi walitoa taarifa kwa nani kuhusu uchunguzi huu, na taarifa hizi zilifanyika lini?

3. Je, wanasiasa wa serikali na majimbo walipuuza matokeo ya utekelezaji wa sheria ili kutumia machafuko ya jamii kwa madhumuni yao wenyewe ya kisiasa?

4. Je, mashirika ya uwakilishi yaliyoathiriwa yalikuwa yakifahamishwa kuhusu uchunguzi unaoendelea wa polisi, na je, matangazo yao ya hadharani yalionyesha ukweli unaoendelea?

5. Kwa kuzingatia kwamba bosi wa ASIO Mike Burgess amekuwa akionya hadharani, tangu angalau 2024, kuhusu 'nchi rafiki' zinazotaka kutumia vibaya mivutano ya kijamii, je, nchi kama hizo zina dori gani, kama ipo yoyote, zinazocheza kwa kuzingatia ufichuzi wa sasa?

Kwa kuzingatia uzito wa ufichuzi huu, na kwa maslahi ya uwajibikaji wa umma, maswali haya na mengine mengi yanahitaji kuchunguzwa ipasavyo kwa haraka kabisa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Vilio vya Kuficha Mauaji ya Halaiki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu