Jarida la Mukhtarat - Toleo 60
- Imepeperushwa katika Mukhtarat
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jarida la Mukhtarat kutoka Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Toleo 60 Ramadhan 1446 H - Machi 2025 M
Jarida la Mukhtarat kutoka Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Toleo 60 Ramadhan 1446 H - Machi 2025 M
Hizb ut Tahrir / Tanzania inalaani kwa nguvu zote kitendo cha kukamatwa tena mara ya pili kwa wanaodaiwa kuwa watuhumiwa wa ugaidi ambao waliachiwa huru mnamo tarehe 4 Machi 2025 baada ya kushikiliwa kwa miaka kumi.
Khilafah ni Izza na Njia ya Wokovu kwa Wanadamu! Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 104 H wa kuvunjwa dola ya Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab al-Muharram 1342 H sawia na 03/03/1924 M mikononi mwa wahalifu wa Kiarabu na Kituruki.
Gaza haihitaji mipango zaidi inayoiweka chini ya ukaliwaji kimabavu na udhibiti wa Mayahudi. Kinachohitaji kwa hakika ni hatua ya dhati kutoka kwa Ummah na majeshi yake ili kuinusuru na kuikomboa kutokana na mitego ya Mayahudi na Marekani. Bila haya, tutaendelea kuwahesabu mashahidi na majeruhi, tukishuhudia unajisi na kiburi cha Mayahudi—wakati wote huku watawala wa Waislamu wakiendelea kuusaliti Umma na utumwa wao kwa Amerika.
Katika Arabuni ya kabla ya Uislamu, baadhi ya Waarabu walikuwa wakitengeneza masanamu yao kutokana na tende; walipohisi njaa, wangekula miungu yao! Leo, historia inajirudia yenyewe, lakini kwa umbo gumu zaidi. Mfumo wa Kimagharibi ambao hapo awali uliinyanyua fahamu ya uhuru hadi kwenye hadhi takatifu—uhuru wa fikra, dhamiri, na dini; uhuru wa kuzungumza na kujieleza; uhuru wa kukongamana kwa amani; ushiriki wa kisiasa; ulinzi wa haki za walio wachache; na kukataza utesaji na kutendewa kikatili – sasa unasaliti maadili haya haya yanapokinzana na maslahi ya mabepari na kipote cha watawala.
Mnamo tarehe 11 Februari 2025, taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa kwenye tovuti ya Mahakama ya Upeo ya Pakistan, ambayo ilifichua mabaki ya udanganyifu wa ubwana wa kitaifa. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa Jaji Mkuu na maafisa wengine wa mahakama walikutana na ujumbe wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na kuwaeleza kuhusu masuala ya Mahakama ya Upeo. Katika taarifa hiyo, Jaji Mkuu alithibitisha kuwa Mahakama ya Upeo inakamilisha ajenda ya kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Mahakama ya Utungaji Sera (NJPMC) katika wiki ya mwisho ya Februari. Hata aliwaalika wajumbe wa wakoloni pia kutoa mapendekezo yao katika suala hili.
Ramadhan ya Mwaka Huu, Yaupasa Umma na Majeshi yake Wakabiliana na Dhulma ya Ukoloni wa Marekani!
Dola za kiliberali za kirasilimali zimeundwa kupitia mpango wa kifedha wa kila mwaka wa uendeshaji wa mapato na matumizi ya serikali. Sera hii ya kifedha ambayo inashirikisha nchi za ulimwengu wa tatu katika shinikizo kubwa la kuweka usawa kati ya usimamizi wa serikali wa mambo ya watu na utawala wa kikoloni. Sera ya fedha ya kimataifa (mfumo wa fedha zisizo na thamani ya dhati (fiat)) ambazo thamani zake zimeegemezwa kwa dolari kwa Petroli lazima zisawazishe biashara (mahuruji na maduhuli) ili kuelea thamani ya sarafu ya ndani kutokana na kuzama kwenye dimbwi la mporomoko wa kiuchumi.
Mnamo tarehe 18 Februari 2025, kikosi cha Rapid Support cha Sudan kilifanya mkutano katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta (KICC) jijini Nairobi kuzungumza uundaji wa serikali ya umoja ya majimbo yanayodhibitiwa na kikosi hicho nchini Sudan. Utawala nchini Kenya unashikilia kudai kwamba kujihusisha kwake kwenye mazungumzo hayo ni kuimarisha “juhudi za amani nchini Sudan”. Nairobi imetetea uamuzi wake wa kuwa mwenyeji wa kufanya mazungumzo na kikosi cha wapiganaji yanayolenga kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa. Maafisa wa Kiutawala wa Sudan wameiona hatua hii kama jaribio la kuanzisha utawala mwengine sambamba na ule wa Khartoum, hatua hii ya Kenya imepelekea kulaumiwa kwake kwa kukiuka ubwana wa Sudan na kujihusisha na matendo ya kiuhasama.