Ijumaa, 14 Ramadan 1446 | 2025/03/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  7 Ramadan 1446 Na: 33 / 1446
M.  Ijumaa, 07 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala Vibaraka Wamefichua Udanganyifu wa Ubwana wa Kitaifa na Maslahi ya Kitaifa. Ni Hoja Gani iliyopo ya Kuzuia Kukomeshwa kwa Mfumo wa uliopo Sasa?

(Imetayarishwa)

Mnamo tarehe 11 Februari 2025, taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa kwenye tovuti ya Mahakama ya Upeo ya Pakistan, ambayo ilifichua mabaki ya udanganyifu wa ubwana wa kitaifa. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa Jaji Mkuu na maafisa wengine wa mahakama walikutana na ujumbe wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na kuwaeleza kuhusu masuala ya Mahakama ya Upeo. Katika taarifa hiyo, Jaji Mkuu alithibitisha kuwa Mahakama ya Upeo inakamilisha ajenda ya kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Mahakama ya Utungaji Sera (NJPMC) katika wiki ya mwisho ya Februari. Hata aliwaalika wajumbe wa wakoloni pia kutoa mapendekezo yao katika suala hili.

Udhibiti wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) juu ya sera ya kiuchumi ya Pakistan unajulikana sana hadi Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha hawahisi tena haja ya kuficha ukoloni wa kiuchumi. Mara kwa mara wametoa kauli kwamba watapata kibali cha wakoloni kuhusu masuala ya kutoa afueni kwa wananchi, iwe ni punguzo dogo la muda la bei ya umeme, au unafuu wa kodi kwenye sekta ya ujenzi. Kisha, baada ya kukataliwa na wakoloni, watawala wanaendelea na dori yao duni. Kama kiwango kipya cha chini, kwa mara ya kwanza, vibaraka wa ukoloni wameupa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa leseni ya kuingilia kati katika masuala ya mahakama. Hata hivyo, bila aibu yoyote, Waziri wa Ulinzi, Khawaja Asif, alitetea ukiukwaji wa ubwana wa kitaifa, akisema, “Tulipata tu nafasi ya kupumua kwa sababu ya IMF. Hatuna chaguo. Ni lazima tukubali vikwazo vyetu.”

Kwa hivyo sasa imedhihirika wazi kwamba Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni mwakilishi wa wakoloni, huku watawala ni vibaraka wa ukoloni, "nawab" na "sardars," kama tulivyoteseka wakati wa ukoloni wa Uingereza. Sasa, badala ya ukoloni wa Kiingereza, ni ukoloni wa Kimarekani! Je, sasa haiko wazi kwamba Ulimwengu wa Kiislamu unahitaji ukombozi (tahrir) kutokana na ukoloni wa kiuchumi?

Enyi Wanajeshi wa Pakistan!

Uongozi huu wa kisiasa na kijeshi unacheza na ubwana wa kitaifa na maslahi ya kitaifa kwa ajili ya maslahi ya wakoloni. Wakati wa mpango wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa wa serikali iliyopita, IMF iliidhinisha uteuzi wa Waziri wa Fedha wa Pakistan na Gavana wa Benki ya Kuu ya Serikali. Leo, hali sio tofauti. Ilikuwa ni kupitia IMF na FATF kwamba mfumo wa ulimwengu ulihakikisha kusalimishwa kwa Kashmir. Watawala hawa wamekuunguzeni kama kuni kwa maslahi ya wakoloni katika vita vya Fitna kwa miaka 25. Walakini, vibaraka wa ukoloni wanakuzuieni kutafuta kifo cha shahada na ushindi huko Kashmir na Gaza. Watawala, vibaraka wa ukoloni, wameweka vikwazo kwenye programu zetu za makombora, ili nguvu zenu zisitumike dhidi ya wapiganaji wa kimsalaba. Uongozi huu mara kwa mara unamsujudia Modi, na unaendelea kupunguza bajeti ya ulinzi katika upande wa Pato la Taifa (GDP). Vibaraka hawa hufichua siri za Waislamu kwa maadui kupitia mazoezi ya pamoja ya kijeshi. Pia wanalegeza msimamo juu ya matukufu yetu. Kwa ajili ya hadhi ya GSP Plus, kamwe hawatoa jibu muwafaka kwa majaribio ya kufuru. Na hawakukusanya vikosi vya jeshi kuwasaidia Waislamu wa Gaza.

Kwa hiyo hamuoni kwamba uongozi na mfumo huu unakuingizeni kwenye ukoloni wa Marekani? Hivi mutaendelea kulilia minyororo hii inayoweza kukatika hadi lini? Enyi waja wa Mwenyezi Mungu (swt), songeni na muwang'oe vibaraka wa ukoloni wa Marekani, ambao wanaweka nguvu zetu miguuni mwa Trump. Uongozi wenu unajitolea bila aibu kwa utiifu wa Marekani, na utiifu wenu unakufanyeni muwe washiriki wa dhambi zao. Ramadhan hii, pimeni uzito wenu katika mizani ya kusimamisha Khilafah Rashida na mujulishe uamuzi wenu!

Hizb ut Tahrir inafanya kazi ya kuhakikisha ukombozi (tahrir) wa Waislamu kutokana na ukoloni, kwa Radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Hizb ut Tahrir ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa duniani cha Waislamu. Kwa kusema ukweli, imekuwa mwiba kwa wakoloni wa Magharibi na vibaraka wao katika Ulimwengu wa Kiislamu. Hizb ut Tahrir imejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ina jeshi la watawala wanaofikiri katika kiwango cha siasa za kimataifa, na wamezama ndani kabisa katika thaqafa ya Kiislamu. Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba kamili kwa ajili ya Khilafah, na maelezo ya mifumo ya dola, katika mijeledi mikubwa. Iko tayari kuutekeleza Uislamu kikamilifu na kwa upana, na sio hatua kwa hatua. Kwa hiyo, enyi majeshi ya Pakistan! Jitokezeni na mumpe Nusrah Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, na mwanasiasa mashuhuri Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah. Toeni Nussrah kwa ajili ya kusimamishwa kwake, ili duara hili la udhalilifu liweze kumalizika. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Surah Al-Maida 5:2].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu