Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 17 Sha'aban 1446 | Na: 30 / 1446 |
M. Jumapili, 16 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Majeshi! Chagueni kati ya Watawala hawa ambao ni Watiifu kwa Trump, na Khalifa Rashid ambaye ataikomboa Gaza na Palestina nzima kupitia Nguvu za Kijeshi!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumanne 4 Februari 2025, akiwa ameketi ubavuni mwa muuaji wa Gaza, Benjamin Netanyahu, Rais Trump wa Marekani alitangaza, "Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya kazi nayo pia." Tamko la kiburi la Trump kuhusu Gaza ni kofi kwenye uso wa watawala wa Waislamu, ambao wametekeleza kwa utiifu amri ya Marekani, na kuzuia vikosi vya majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, na hivyo kuruhusu mauaji ya Waislamu nchini Palestina. Watawala wa sasa wa Waislamu, kama wale waliotangulia, wanajifunza kwamba Marekani haiwajali wao, au viti vyao vya khiyana. Marekani itaendelea kuwadhalilisha na kuwashusha hadhi mbele ya dunia na watu wao wenyewe. Kwa hakika, kushiriki katika mfumo wa dunia unaoongozwa na Marekani, na kushikamana na sheria za kimataifa na taasisi za kimataifa, si chochote ila unyenyekevu na utiifu kwa Marekani na rais wake. Hata hivyo watawala hawa hawajali. Hata hivi sasa wanakimbilia kumfurahisha na kumtuliza bwana wao, Amerika, wakijaribu kuwasilisha kwake "mpango wa amani wa Waarabu" wao wenyewe.
Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ لَا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا ٱللَّهُۚ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرَدُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فِيٓ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَقَالُوٓاْ إِنَّا كَفَرۡنَا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ وَإِنَّا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَنَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ]
“Je! Hazikukufikieni khabari za walio kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na A'adi, na Thamud, na walio baada yao, ambao hapana awajuaye ila Mwenyezi Mungu? Mitume wao waliwajia kwa hoja zilizo wazi, na wao wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao, wakasema: Hakika sisi tumeyakataa hayo mliyo tumwa, na hakika sisi tuna shaka kubwa na mnayo tuitia.” (Surah Ibrahim 9)
Kukataa kwa watawala amri za Mwenyezi Mungu (swt) ni wazi kwa kila mtu kuona. Wamewatelekeza watu wetu, ardhi na rasilimali zetu kwa Amerika na rais wake. Wanaamini uwezo, mamlaka na nguvu zinatoka Washington, lakini nyinyi munasimama wapi? Je, mutaendelea kusitasita katika kufanya uamuzi wenu wa kuondoa uungaji mkono wenu kutoka kwa watawala hawa? Je, munasitasita kupigana na Marekani na kugongana na mfumo wake wa dunia, na munapendelea kudhalilishwa na Trump na wafuasi wake miongoni mwa watawala wa Waislamu? Je, mnakubali kwamba Trump anatangaza ardhi zenu kuwa ni zake, na kwa khiyari yake anazunguka katika ardhi za Kiislamu, akijichukulia anachotaka, hali nyinyi mna uwezo na nguvu, na ni wajibu wa Shariah kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kulinda ardhi za Waislamu na Ummah! Mcheni Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake! Tendeni kama wanaume wenye heshima! Kumbukeni kiapo chenu! Kufa shahidi katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na kukataa kujisalimisha kwa dhalimu wa dunia ni bora kwa afisa wa Kiislamu kuliko udhalilifu ambao kutochukua kwenu hatua kunakuleteeni juu yenu.
Umma umeona mitihani mingi kabla yenu! Tulikabiliana na Wamongolia wenye nguvu, ambao walianzisha milki kubwa zaidi ya ardhi katika historia ya wanadamu. Lakini Saifuddin Qutuz alikataa kusujudu mbele yao, hata baada ya kunyang'anywa Baghdad, na kuuawa kwa Khalifa wa Abbasiya. Ilikuwa mikononi mwa Qutuz, ambapo mbegu za uharibifu wa milki ya Wamongolia ziliwekwa, alipowashinda katika vita vya kukata shauri huko Ain Jaloot.
Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Ni juu yenu kuchagua sasa kati ya watawala hawa na uongozi wa kijeshi uliotiifu kwa Trump au utiifu kwa Khalifa ambaye anakataa mfumo wa dunia wa Marekani. Khalifa Rashid ndiye atakayeikomboa Gaza na Palestina nzima, kupitia Jihad yenye nguvu ambayo itatikisa mfumo wa dunia unaoporomoka. Toeni Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida na mumalize zama hizi za fedheha na udhalilifu kwa Umma wa Kiislamu.
[فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَقُلۡ أَنذَرۡتُكُمۡ صَٰعِقَةٗ مِّثۡلَ صَٰعِقَةِ عَادٖ وَثَمُودَ]
“Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A'di na Thamudi.” (Surah Fussilat Ayat 13)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |