Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 6 Sha'aban 1446 | Na: 27 / 1446 |
M. Jumatano, 05 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Washiriki wa Kongamano lenye Kichwa:
"Kashmir na Palestina inayokaliwa kwa mabavu - Suluhisho ni Nini?"
(Imetafsiriwa)
Mtazamo wa kupuuza suluhisho la wazi la Shariah kwa kadhia za Kashmir na Palestina kwa jina la hekima, manufaa na kile kinachoitwa uhalisia ulio uwanjani lazima ukataliwe kabisa.
Iwe ni kadhia ya Kashmir au Palestina, suluhisho la Shariah kwa kadhia hizo liko wazi kabisa. Hizi ni ardhi za Waislamu zinazokaliwa kimabavu. Suluhisho pekee la Sharia ni uhamasishaji wa vikosi vya jeshi ili kukomesha ukaliaji kimabavu wa kafiri kupitia Jihad, huku Ummah wote lazima uunge mkono vikosi hivi vya jeshi. Vikosi vya kijeshi ndivyo vilivyo na uwezo wa kung'oa ukaliaji huu wa kimabavu. Ni wajibu wa Sharia kwa Ummah mzima kwa jumla, na Wanazuoni wake, vyama vya siasa vya Kiislamu, viongozi wa Waislamu na watu wenye ushawishi hasa, kushauri, kuchochea na kulazimisha vikosi vya jeshi kutekeleza jukumu hili. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu,
[وَاقۡتُلُوۡهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوۡهُمۡ وَاَخۡرِجُوۡهُمۡ مِّنۡ حَيۡثُ اَخۡرَجُوۡكُمۡ]
“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191]. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[يٰۤـاَيُّهَا النَّبِىُّ حَرِّضِ الۡمُؤۡمِنِيۡنَ عَلَى الۡقِتَالِ] “Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani.” [Surah Al-Anfal 8:65]. Kanuni (Qaidah) ya Shariah iko wazi kwamba (خطاب الرسول ﷺ خطاب لأمته) "hotuba kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni hotuba kwa Ummah wake."
Imeharamishwa waziwazi kurudi kwa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na kadhia ya Kashmir, kwa sababu Umoja wa Mataifa ni Taghut, mamlaka yaliyojengwa juu ya msingi juu wa hukmu nyengine isiyokuwa ile aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu (swt), kwa mujibu wa Sharia. Kuregelea kwa Umoja wa Mataifa ni kukaribisha Ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran Tukufu,
[اَلَمۡ تَرَ اِلَى الَّذِيۡنَ يَزۡعُمُوۡنَ اَنَّهُمۡ اٰمَنُوۡا بِمَاۤ اُنۡزِلَ اِلَيۡكَ وَمَاۤ اُنۡزِلَ مِنۡ قَبۡلِكَ يُرِيۡدُوۡنَ اَنۡ يَّتَحَاكَمُوۡۤا اِلَى الطَّاغُوۡتِ وَقَدۡ اُمِرُوۡۤا اَنۡ يَّكۡفُرُوۡا بِهٖ ؕ وَيُرِيۡدُ الشَّيۡـطٰنُ اَنۡ يُّضِلَّهُمۡ ضَلٰلًاۢ بَعِيۡدًا]
“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [Surah An-Nisaa 4:60]. Kwa hivyo, kuregelea maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa Kashmir hakuwezi kukubalika kwa jina la hekima, manufaa, au uhalisia ulioko uwanjani.
Enyi vyama vya kisiasa vya Kiislamu, viongozi wa Waislamu, watu wenye ushawishi na wanazuoni! Watawala hawa wameisalimisha Kashmir. Wako tayari kusalimisha sehemu kubwa ya Ardhi Iloyobarikiwa ya Palestina kwa Mayahudi kwa jina la "suluhisho la dola mbili." Wanajaribu kujificha nyuma ya Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kimataifa na mamlaka nyingine za Taghut ili kujikinga na ghadhabu ya Umma. Kwa hiyo, ni lazima mueleze kwa uwazi msimamo wa kweli mbele ya Ummah, na mubainishe suluhisho la Shariah, bila kulegeza msimamo wowote au udhuru. Kuunga mkono maazimio ya Umoja wa Mataifa na Waislamu kwa hakika ni sawa na kuwaunga mkono watawala hawa wasaliti. Wajibu wa Shariah juu ya maulamaa ni kutangaza haki dhahiri shahiri, bila ya woga wowote. Maulamaa lazima wasichanganye haki na batili kwa jina uhalisia ulioko uwanjani. Hili linauchanganya Ummah na hauwi kitu kimoja katika suala la kuwawajibisha watawala. Umma unazidi kupata mwamko na utambuzi, ambao kwao Ummah umewapindua watawala wa Afghanistan, Bangladesh na Syria. Ummah unaanza kuchukua mambo yake mikononi mwake. Mwenyezi Mungu (swt) amekupeni ushawishi, basi ipambanueni haki na batili mbele ya Ummah, ili Umma uweze kuwatambue wasaliti. Jihadharini na watawala hawa na wafuasi wao wasije wakakuongozeni kuficha haki. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَدُّوۡا لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُوۡنَ] “Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.” [Surah Al-Qalam 68:9].
Msimamo wa umoja wa pamoja juu ya suala hili wa Waislamu wote wanaounga mkono Uislamu na wanaotamani kuona utekelezwaji wa Sharia ya Mwenyezi Mungu (swt) utawalazimisha watawala kurudi nyuma na kupiga magoti. Iwapo watasusia bidhaa za Kiyahudi na za Magharibi na kutaka kupelekwa kwa majeshi ya Waislamu huko Gaza kama hatua za pamoja, hii itawafichua watawala wabaya na kuharibu sifa zao. Msimamo huo wa wazi kuhusu kadhia ya Kashmir pia utakuwa mwanzo wa kuwazika watawala hao pamoja na tawala zao. Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan inakupongezeni kwa kufanya kongamano hili, na inatumai kwamba kongamano hili litatoa tangazo la msimamo huu wa pamoja kwa Waislamu wa Kashmir na Palestina.
[وَمَا عَلَيْنَا إِلا الْبَلاغُ الْمُبِينُ]
“Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.” [Surah Yasin: 17]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |