Jumamosi, 23 Sha'aban 1446 | 2025/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  13 Sha'aban 1360 Na: 1446 / 29
M.  Jumatano, 12 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuanguka kwa Khilafah Kunaashiria Wito wa Kuhuishwa Kwake

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 3 Machi 1924, sawia na 28 Rajab 1342 H, kikundi kidogo cha wasaliti wa Kituruki, wakiongozwa na Mustafa Kemal, walivunja urithi wa zaidi ya karne 13 za umoja wa Waislamu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, Waislamu walipoteza paa lao juu ya vichwa vyao na wakawa mayatima. Leo, miaka 104 ya hijria imepita tangu tukio hili la kusikitisha. Baada ya kuanguka kwa Khilafah, makafiri waligawanya ulimwengu wa Kiislamu katika maeneo madogo yaliyojitenga. Waliweka vikwazo vya usafiri kati ya maeneo haya, yakihitaji pasipoti na visa, na kuharibu majeshi yetu, silaha, rasilimali, ardhi, uwezo wa binadamu, na teknolojia-kila kitu. Kwa ufupi, tukawa uwanja wa uwindaji wa makafiri. Sasa hakuna jeshi la Waislamu la kuwatetea Waislamu wa Gaza au Burma. Vikosi vya jeshi la Pakistan havihamasishwi kukomboa Masjid Al-Aqsa, wala vikosi vya jeshi la Uturuki havihamasishwi kuikomboa Kashmir. Ni kana kwamba mwili umevunjwa vunjwa, kichwa, kiwiliwili, mikono, na miguu vyote vimekatwa!

Ili kuhifadhi Khilafah, Waislamu wa India walianzisha kampeni kubwa zaidi ya kisiasa katika historia ya nchi hiyo, inayojulikana kama Harakati ya Khilafah. “Kamati za Khilafah” zilianzishwa katika kila mtaa na kila kitongoji. Hata Gandhi alitambua kwamba mustakabali wa Mabaniani nchini India ungekuwa wenye giza bila kuunga mkono harakati hii. Waislamu wa India hapo awali walipeleka misaada kusaidia Khilafah wakati wa Vita vya Balkan, na askari wengi wa Kiislamu wa India walichagua kukabiliwa na hukumu ya kifo mikononi mwa Waingereza badala ya kupigana dhidi ya Khilafah ya Uthmani. Ilhali leo, vikosi vyetu vinatumika kama mamluki katika vita vya Amerika. Maluteni wetu vijana, manahodha, na wakuu wanakuwa majeruhi katika migogoro inayowanufaisha wakoloni kila siku. Tunashuhudia kwa macho yetu ukatili unaofanywa na makafiri dhidi ya watu wetu huko Palestina. Mateso ya ndugu na dada zetu katika Turkestan Mashariki, Kashmir, Myanmar, Asia ya Kati, Sudan, Yemen, Syria, na nchi nyinginezo za Kiislamu yanajulikana sana. Wanastahamili dhulma, umwagaji damu, na maangamivu bila ya Imam (Khalifa), ngao yao, waliyemtegemea kwa ulinzi, na ambaye walitazamia kwake uongozi katika vita.

Enyi Waislamu! Kuanguka kwa Khilafah kunaashiria wito wa kuhuishwa kwake. Khilafah ni dola na chombo cha kisiasa cha Uislamu. Ni njia ya Shariah ya kutekeleza Uislamu. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) alimuamuru Mtume wake (saw) kuhukumu baina ya Waislamu kwa mujibu wa Sharia iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema, [فَٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلْحَقِّ] “Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Surah Al-Maidah, 5:48]. Na akasema (swt):

[وَأَنِ ٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ وَٱحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَنۢ بَعْضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Maidah, 5:49]. Kanuni ya Shariah ni kwamba, خِطَابُ الرَّسُولِ ﷺ خِطَابٌ لِأُمَّتِه “Khitaab (Hotuba) kwa Mtume (saw) ni hotuba kwa Ummah Wake.” Ingawa hotuba kwa Mtume (saw) inaelekezwa kwake na yeye amejumuishwa ndani ya hotuba hiyo, hotuba inaelekezwa kwake kama Mtume sio tu yeye kama mtu binafsi. Kwa hivyo hotuba ni hotuba kwa Mtume wa Ummah. Vile vile, dalili ya kuwa hotuba kwa Mtume ni hotuba kwa Ummah wake ni kwamba hotuba iliyoainishwa kwa ajili ya Mtume (saw) pekee hubainishwa kuwa ni kwa ajili yake (saw) pekee. Hivyo faradhi ya kutawala kwa Uislamu ni juu ya Umma wa Muhammad (saw).

Ama Sunnah, Imam Muslim amepokea kutoka kwa Nafi’ kwamba alisema: Ibn Umar (ra) aliniambia kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»

 “Mwenye kuuondoa mkono wake katika utiifu atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama bila ya hoja yoyote juu yake, na atakayekufa bila ya kuwa na Ba’yah shingoni mwake atakufa kifo cha kijahiliya.” Kwa hiyo, Mtume (saw) alimlazimu kila Muislamu kuwa na Ba’yah shingoni mwake. Akamtaja mwenye kufa bila ya kuwa na Ba’yah shingoni kana kwamba amekufa kifo cha Jahiliyyah. Ba’yah sio sahihi isipokuwa Bayah aliyopewa Khalifa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliweka ufaradhi kwamba kila Muislamu awe na Ba’yah shingoni mwake kwa ajili ya Khalifa. Hata hivyo, yeye (saw) hakumlazimu kila Muislamu kutoa Ba’yah kwa Khalifa. Kwa hiyo, ufaradhi ni kuwepo kwa Ba’yah kwenye shingo ya kila Muislamu.

Imaam al-Mawardi amesema katika kitabu chake Ahkam al-Sultaniyyah, الإمامة موضوعة لخلافة النبوة في حراسة الدين وسياسة الدنيا، وعقدها لمن يقوم بها في الأمة واجب بالإجماع “Imamah (Khilafah) imewekwa kama mrithi wa Utume katika kulinda Dini na siasa za dunia, na uteuzi wa mwenye kuitekeleza katika Ummah ni faradhi ya Shariah kwa Makubaliano ya pamoja ya Maswahabah.” Imaam al-Nawawi amesema katika Sharh Muslim, أجمعوا على أنه يجب على المسلمين نصب خليفة “Wamekubaliwa kwamba ni wajibu wa Shariah kwa Waislamu kumchagua  Khalifah.” Khilafah ya Kiislamu na kuunganishwa kwa Ummah chini ya mtawala ambaye atawatawala kwa mujibu wa Sharia ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa namna ya Mtume (saw), ndilo lengo kuu la maisha ya Muislamu leo. Ni moja ya malengo muhimu ya Uislamu. Inawakilisha aina ya juu kabisa ya umoja na mshikamano ambao Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) wameamrisha. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَٱعْتَصِمُوا۟ بِحَبْلِ ٱللَّهِ جَمِيعًۭا وَلَا تَفَرَّقُوا۟] “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Surah Aali Imran, 3:103]. Kwa hiyo, mgawanyiko ndani ya Ummah unasababisha machafuko na udhalilifu.

Enyi Waislamu! Hakika kusimamisha Khilafah ni faradhi kutoka kwa Mola wenu Mlezi (swt) na ni bishara njema kutoka kwa Mtume wenu (saw). Ni chanzo cha heshima kwenu na njia ya kuwatiisha adui zenu. Ni njia ya kueneza haki na uadilifu kote ulimwenguni, kwa hivyo fanyeni kazi kwa uaminifu kuelekea kuanzishwa kwake. Je! nyoyo zenu hazitamani Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt)? Mbele ya uoga wa watawala wenu, na kwa hakika khiyana yao kwenu, wako wapi wale watakaoitikia wa-mu‘tasimah?

Dawah ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi kwa bidii, inavuka mipaka ya kirongo ya kitaifa ambayo ukoloni umeiweka baina ya ardhi za Waislamu baada ya kuanguka kwa Khilafah ya Uthmani. Ni Dawah ya kimataifa kwa Waislamu wote kwani Khilafah ni uongozi wao wa pamoja. Hizb imetayarisha rasimu ya katiba kwa ajili ya Khilafah, inayotokana na Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume, ambayo inajumuisha hukmu za Shariah kuhusu uchumi, mambo ya nje, vita, mahusiano ya kijamii, elimu, afya, fedha, na kila kitu muhimu kwa ajili ya utekelezaji wake kivitendo kuanzia siku ya kwanza, in shaa Allah. Dalili za kuhuishwa kwake tayari zinaonekana, na Waislamu wanaitamani.

Kwa hivyo enyi Waislamu! Tunakulinganieni mushirikiane nasi katika kufanya kazi kwa umakini na ikhlasi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida, na tunakuombeni muzingatie amri hii ya Mwenyezi Mungu (swt),

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَقَلْبِهِۦ وَأَنَّهُۥٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Suran Al-Anfaal, 8:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu