Jumatano, 18 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Safar 1447 Na: 06 / 1447
M.  Alhamisi, 21 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hali Baada ya Mvua na Mafuriko kwa Mara Nyingine Tena Imeweka Wazi Kuwa Waislamu Wanahitaji Mchungaji Khalifah

(Imetafsiriwa)

Tangu Juni 26, mafuriko katika maeneo mbalimbali ya Khyber Pakhtunkhwa, Punjab, na Karachi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 650 na kujeruhi zaidi ya elfu moja. Maelfu ya nyumba zimesombwa na maji, pamoja na akiba za maisha yote za watu, mali za nyumbani, na magari. Dada na mabinti zetu—ishara za staha na heshima—wamenyimwa nyumba na faragha zao, wakilazimishwa kuishi chini ya anga wazi.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inashiriki kwa usawa katika majonzi ya ndugu na dada zetu wote Waislamu. Tunavumilia taabu hii kwa subira na tunawataka Waislamu wengine kufanya vivyo hivyo kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyosema:

«مَا يُصِيبُ الْمُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ وَلَا وَصَبٍ وَلَا هَمٍّ وَلَا حُزْنٍ وَلَا أَذًى وَلَا غَمٍّ حَتَّى الشَّوْكَةِ يُشَاكُهَا إِلَّا كَفَّرَ اللَّهُ بِهَا مِنْ خَطَايَاهُ»

Haitomfikii Muislamu uchovu, wala maradhi, wala huzuni, wala udhia, wala dhiki, wala mchomo wa miiba, isipokuwa Mwenyezi Mungu humfutia miongoni mwa dhambi zake.” (Bukhari na Muslim)

Hata hivyo katika wakati huu huu, uzembe, mapuuza, na kutojali kwa watawala wetu kumefichuliwa. Hii si mara ya kwanza kwa Pakistan kukumbwa na maafa ya mafuriko. Mafuriko ya uharibifu ya 2010 na 2022 yangalipo katika kumbukumbu. Katika mafuriko ya 2022 pekee, theluthi moja ya nchi iliathiriwa, na watu milioni 33 waliachwa katika hali ngumu. Pakistan ni miongoni mwa nchi kumi zilizoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi. Ina zaidi ya barafu 9,000—idadi kubwa zaidi ulimwenguni nje ya Ncha ya Kaskazini na Kusini. Kuyeyuka kwake haraka kumeongeza hatari ya mafuriko. Walakini, kama kawaida, watawala wetu wanaonekana tu kuwa hai kwa siku chache za uangaziaji wa vyombo vya habari, baada ya hapo kila kitu kinasahaulika. Kwa mfano, serikali ya Khyber Pakhtunkhwa ilitenga rupia milioni 800 tu kwa mkoa mzima, na rupia milioni 500 tu kwa wilaya ya Buner, ambazo hazitoshi kwa kujenga upya miundombinu wala kutoa msaada wa kimsingi kwa watu walioathirika. Siasa za watawala hawa wa kidemokrasia zimafungika kwenye maonyesho ya vyombo vya habari badala ya utumishi wa kweli wa umma.

Kinyume chake, chini ya Khilafah, Khalifa anawajibika kwa uchungaji wa Ummah mzima. atahisabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na yuko chini ya uchunguzi wa Umma. Kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu kundi lake. Imam (Khalifa) ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.” (Bukhari na Muslim)

Lau Khilafah ingesimamishwa leo, isingeficha mapungufu yake nyuma ya maneno kama “cloudburst.” Badala yake, ingejenga miundombinu ya kitaasisi na ya kimfumo, kushiriki katika upangaji wa muda mrefu, na kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hasara. Lakini serikali mtawalia za Pakistan zimepuuza jambo hili kwa zaidi ya miongo saba, kwani vipaumbele vyao daima vimejikita katika kulinda maslahi ya dola za kikoloni. Matatizo ya watu huchukuliwa kwa uzito kwa kiasi tu kinachoathiri uhai wa serikali zao.

Ndani ya Khilafah ya Kiislamu, maisha ya Muislamu ni matukufu, na fidia (diyah) hulipwa kwa hasara ya maisha, inayosababishwa na sababu za kibinadamu, ikiwemo uzembe na ulegevu. Kinyume chake, katika mfumo wa kidemokrasia, thamani ya binadamu inadunishwa hadi kwenye ushawishi wa kisiasa na uwezo wa kuathiri mapambano ya madaraka. Mfumo huu wa kidemokrasia wa kibepari mara kwa mara haujaleta chochote kwa Waislamu isipokuwa udhalilifu, unyimwaji, na unyonge. Wakati umefika sasa wa kuuzika mfumo huu na kusimamisha Khilafah. Waislamu wa Pakistan, pamoja na vikosi vyetu vya jeshi, lazima wakomeshe mfumo huu uliopitwa na wakati na watangaze kuasisiwa kwa Khilafah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu