Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 5 Ramadan 1446 | Na: 1446/22 |
M. Jumatano, 05 Machi 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano wa Cairo Unathibitisha Usaliti wa Watawala wa Kiarabu kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina
(Imetafsiriwa)
Mkutano huo wa dharura wa Waarabu ulifanyika jijini Cairo katikati ya mazingira machungu ambayo Umma wa Kiislamu unapitia, hasa hujuma za Kiyahudi mjini Gaza, na shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusu kadhia ya Palestina. Kama ilivyotarajiwa, mkutano huo ulitoa taarifa ya mwisho ambayo ilikuwa na maneno ya kulaani na kukashifu, na kutaka masuluhisho ya viraka ambayo hayashughulikii mizizi ya mgogoro huo. Je, tunautazamaje mkutano huu? Na ni upi msimamo juu ya matokeo yake?
Viongozi wa Kiarabu wamezoea kufanya mikutano ya dharura wakati wowote migogoro inapoongezeka, lakini haileti mabadiliko msingi katika uhalisia wa kisiasa au kijeshi.
Badala yake, inakuja kama kipimo rasmi cha kuonyesha "hatua ya Kiarabu" kwa watu wenye hasira, bila kudhuru maslahi ya dola za Magharibi ambazo zinadhibiti hatima ya kanda hiyo, watawala na tawala zake. Mkutano wa mwisho wa kilele hautofautiani na sheria hii, kwani ulifungika tu na kutoa taarifa ya wito wa "kukataa kuhamishwa kwa lazima kwa Wapalestina" na "kutabanni mpango wa ujenzi mpya wa Gaza", huku Mayahudi wakiendelea na uvamizi wao kwa msaada wa Magharibi, bila washiriki wa kongamano hilo kuchukua hatua yoyote ya kweli kukomesha.
Mojawapo ya mambo hatari zaidi ya matokeo ya mkutano huo ni kutilia mkazo suluhisho la kisiasa linalotokana na maazimio ya Umoja wa Mataifa, jambo ambalo linagongana na uhalisia, kwani shirika hili halijawahi kuwa upande wa Umma, bali ni chombo mikononi mwa nchi za Magharibi kulazimisha miradi yake ya kikoloni. Kuendelea kupigiwa debe kwa suluhusho la dola mbili na watawala wa Kiarabu kama njia ya kujiondoa katika mgogoro huo ni udanganyifu wa kisiasa unaowahadaa watu kuamini kuwa kuna suluhisho la kisiasa ambalo linaweza kupatikana, huku uvamizi huo ukiendelea na mradi wake wa uwekaji makaazi bila kukoma, huku ukitoacha nafasi ya kuanzishwa kwa dola hiyo inayodaiwa.
Mkutano huo wa kilele ulipuuza kabisa suluhisho msingi la kadhia ya Palestina, ambalo ni kuikomboa kutokana na Mayahudi kwa njia ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Khilafah inayounganisha Umma na kuyaelekeza majeshi yake katika kupambana na Mayahudi wanyakuzi, badala ya kujihusisha na miradi ya Magharibi ambayo inalenga kuendeleza uvamizi huo.
Palestina sio tu ni kadhia ya kibinadamu au ya kisiasa, bali ni kadhia la kiitikadi ambayo inahusiana na hukmu za kisheria zinazopaswa kutekelezwa mara moja, na kushindwa kufanya hivyo ni dhambi. Ukombozi wa Palestina yote ni kadhia ya Ummah ambayo majeshi yake lazima yasonge mara moja hadi ipatikane, yakiongozwa na nchi zinazoizunguka, kwanza kabisa Misri.
Moja ya mada kuu ambayo mkutano huo ulizingatia zaidi ni "kuijenga upya Gaza", karata inayotumiwa kuzuia hasira za watu wengi na kuwahadaa Wapalestina kwamba suluhisho lipo katika kusukuma fedha, badala ya kuhamasisha majeshi kukomesha uvamizi huo. Ujenzi upya wakati uvamizi inaendelea ni kuitakasa hali ilivyo, kwa sababu kila kitu kitakachojengwa kitaharibiwa tena. Suluhisho si kuomba msaada, bali ni kuukusanya Umma na majeshi yake ili kuikomboa Palestina, ambayo ni wajibu halisi wa Umma na majeshi yake, hususan Misri na jeshi lake.
Ujenzi upya ni uregelezaji wa mgogoro, hivyo Gaza inasalia kuzingirwa na chini ya tishio la mara kwa mara, wakati makampuni na nchi zinafaidika na kandarasi na pesa zinazotolewa kwa jina la ujenzi upya. Makampuni ya kimataifa na ya Kiarabu yanaingia katika miradi hiyo, na kupata kandarasi zenye thamani ya mabilioni ya dolari, na umbile la Kiyahudi linadhibiti uingiaji wa vifaa vya ujenzi, na wakati mwingine huagizwa kutoka kwa makampuni yake, ambapo ina maana kwamba linafaidika kutokana na ujenzi mpya uliokuja kutokana na uhalifu wake. Mbali na nchi za Kiarabu, zikiongozwa na Misri, mshirika mkuu wa umbile hilo nyakuzi, na mdhibiti halisi wa kila kitu kinachoingia Ukanda wa Gaza.
Licha ya kuendelea jinai za uvamizi huo dhidi ya watu wa Gaza, matokeo ya mkutano huo wa kilele hayakujumuisha hatua zozote za kivitendo za kukomesha uvamizi huo, hata kama ni mara moja kukomesha umwagaji damu wao, kama vile kukata mahusiano ya kidiplomasia, au kusimamisha ushirikiano wa kijeshi na uratibu wa usalama nao. Au hata kutumia rasilimali za kiuchumi kushinikiza nchi zinazoliunga mkono. Kinyume chake, baadhi ya nchi za Kiarabu bado zinacheza dori ya mpatanishi kati ya upinzani nalo, badala ya kuwa upande wake. Utawala wa Misri bado ni ule ule, unawazingira watu wa Gaza kwa shinikizo la mara kwa mara ili wakubali kile ambacho nchi za Magharibi inawaamuru.
Matokeo ya mkutano huo yanaakisi ukweli kwamba watawala wa Kiarabu sio sehemu ya suluhisho, bali ni sehemu muhimu ya tatizo, kwani ni ala za utendaji zinazotekeleza miradi ya nchi za Magharibi katika eneo hilo. Lau wangekuwa na nia ya kweli hata kidogo ya kuikomboa Palestina, majeshi ya Waislamu yasingebakia katika ngome zao, huku umbile la Kiyahudi likiendelea na uvamizi wake bila ya kuzuiwa.
Mkutano huu wa kilele haukutoa lolote jipya, bali ulikuja kama nyongeza ya msururu mrefu wa mikutano ya kilele iliyofeli ambayo haikufanikisha lolote kwa Ummah, bali ilichangia kuendeleza mateso yake. Ni fursa mpya ya kufichua ukweli kuhusu tawala hizi kwa watu wao, ili watambue kwamba hatima yao haitabadilika kwa mipango ya uhaini, bali kwa mapinduzi ya kifikra na kisiasa ambayo yanaurudisha Uislamu madarakani na kuuongoza Umma kuelekea utukufu wake ulioibiwa.
Enyi Wanajeshi wa Kinana: Nyinyi ni kizazi cha Al-Nasir Salah Al-Din aliyeikomboa Al-Qudsi kutoka kwa Wapiganaji wa Kimsalaba, na Al-Muzaffar Qutuz na Al-Zahir Baybars ambao walizuia kusonga mbele kwa Wamongolia. Mlikuwa ngao kwa Ummah na ushindi kwa ajili yake, basi timize kazi yako na mufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha juu yenu, kwani nyinyi munaweza kuwasaidia watu wetu wa Palestina na mukomboe ardhi yao katika masaa machache ya siku, basi fanyeni hivyo kwa ajili ya Mola wenu Mlezi na muwafukuze kutoka kwenu watawala wa madhara wanaokuzuieni na jukumu hili kubwa na heshima, kwa hivyo wamefukuzeni watawala hawa na maamuzi yote batili na matokeo mabovu waliyohitimisha, na muwe ushindi kwa Ummah kwa kusimamisha dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, dola inayokuhamasisheni kuunusuru Uislamu na watu wake na kuhifadhi matukufu yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awe pamoja nanyi na ndani yenu enyi wanajeshi wa Kinana.
[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa 4:75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |