Jumatatu, 16 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  14 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 26
M.  Jumamosi, 06 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Wakutana na Mkuu wa Chama cha Adalah nchini Sudan
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Al-Nadir Muhammad Hussein, mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Mhandisi Banqa Hamid, na Ustadh Issam al-Din Abdul Qadir, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelea Ustadh Al-Tijani Abdul Wahab, mkuu wa Chama cha Adalah nchini Sudan, nyumbani kwake katika mji wa Al-Obeid, mnamo Ijumaa tarehe 05/09/2025, kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ili kutibua mpango wa kuitenganisha Darfur.

Mwanzoni mwa kikao, mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Al-Nadir, alisema kuwa umoja wa Umma na Dola ni suala muhimu, ambalo Uislamu ulituamrisha kuchukua hatua ya uhai au kifo, na dalili za hilo katika Qur’an na Sunnah ni nyingi. Inajulikana kuwa Amerika inataka kuigawanya Sudan katika vidola vitano vidogo, na ilifanikiwa kutenganisha Kusini, na sasa inataka kutenganisha Darfur kwa zana zile zile, kwa kumfanya mtoto wake anayebembelezwa, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), harakati yenye nguvu zaidi ya kijeshi mjini Darfur, ili kutenganisha Darfur na watu wake yenyewe, sio na watu wa Ulaya kama ilivyofanya mbeleni, kwa kumfanya kibaraka wake John Garang na vuguvugu lake mkuu wa makundi ya waasi. Kisha ikatumia fikra ya kugawanya madaraka na mali kwa misingi ya kikanda na ya ubaguzi wa rangi, na fikra ya mapambano ya katikati na pembezoni, kisha kuiondoa RSF kutoka Sudan ya kati na kutoka mji mkuu, na kuwekwa mjini Darfur, kisha kuunda serikali sambamba huko Nyala. Vitendo hivi vyote vinaonyesha njama chafu.

Kwa hiyo, Hizb ut Tahrir imezindua kampeni ya kufichua na kutibua njama hii, kwa kufanya kazi pamoja na nguvu muhimu na Ummah, na ziara hii kwenu ilikuwa ni sehemu ya hilo. Kwa upande wake, Ustadh Al-Tijani alisema: “Nimefurahishwa kwamba mumenijumuisha katika ziara hii, na kunifanya niwe sehemu ya kazi hii kubwa, na daima mnabeba hamu ya Umma na nchi, na mimi niko pamoja nanyi kutibua njama hii ambayo inaungwa mkono na dola za kikoloni, na kwa mujibu wa ufuatiliaji wangu wa matukio nilikuwa nafahamu kwamba vita hivi vingewaka moto.”

Mwishoni, tulimshukuru kwa mapokezi yake mazuri na ukarimu wake.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu