Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 13 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 25 |
M. Ijumaa, 05 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Matendo ya Watawala wa Sudan na Misri Kuhusu Bwawa la An-Nahdha
Upotevu wa Usalama wa Maji kwa Watu wa Bonde la Nile
(Imetafsiriwa)
Utaratibu wa mashauriano baina ya nchi mbili unaojulikana kama 2+2, unaojumuisha mawaziri wa mambo ya nje na unyunyiziaji maji wa Misri na Sudan, walifanya mkutano katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri mnamo Jumatano, 3/9/2025, kujadili maendeleo katika faili la Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD). Mkutano huo ulisababisha taarifa ya pamoja ambapo pande hizo mbili zilieleza makubaliano yao kamili kuhusu hatari ya hatua za upande mmoja zinazochukuliwa na Ethiopia kuhusu ujazaji na uendeshaji wa bwawa la GERD. Taarifa hiyo iliashiria hatari kadhaa zinazohusishwa na bwawa hilo, ikiwa ni pamoja na dhamana dhaifu ya usalama, mtiririko wa maji usio wa kawaida, na athari zinazoweza kutokea wakati wa ukame.
Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, tulionya kabla ya bwawa kujengwa juu ya hatari zake, na kwamba watawala wa Misri na Sudan lazima wafanye kazi kwa bidii ili kusitisha ujenzi wake. Hata hivyo, hakuna yeyote akiyesikiliza hadi bwawa hilo kukamilika na kuwa uhalisia.
Kwa kuzingatia uhalisia huu, tunasisitiza ukweli ufuatao:
Kwanza: Watawala wa Misri na Sudan ndio walioiacha haki ya maji ya watu wa Sudan na Misri kwa kutia saini kile kilichoitwa Azimio la Kanuni mnamo Machi 2015, ambalo liliipa Ethiopia haki ya kujenga bwawa hilo, na hivyo kuziacha haki za kihistoria na mgawo wa maji wa Misri pamoja na Sudan.
Pili: Utaratibu huu unaozungumzia hatari zinazotokea hivi sasa, baada ya ujenzi wa bwawa kukamilika, ni aina ya udanganyifu, unaowapotosha watu wa Sudan na Misri, na kuwahadaa kuwa wana serikali zinazotetea maslahi yao.
Hizb ut Tahrir ilipozungumza kuhusu hatari hizi, ikizitaja katika vikao na mihadhara yake, na kisha katika kijitabu, “Bwawa la An-Nahdha (Grand Renaissance) na Matishio ya Vita vya Maji; Uzembe wa Watawala na Wajibu wa Ummah,” kilichotolewa mnamo Septemba 2017, ambacho, kiliungwa mkono wajuzi na wataalamu, wakati huo, waandishi na wasemaji wa serikali ya Sudan walijibu, wakikanusha hatari hizo na kudai kwamba bwawa hilo linatumikia maslahi ya watu wa Sudan! Inashangaza kwamba leo wao wenyewe wanazungumza juu ya hatari zile zile!
Tatu: Baada ya watawala wa Misri na Sudan kusalimu amri na kuruhusu Ethiopia kujenga bwawa hilo, waliwashughulisha watu kuzungumzia kuhusu usimamizi na uendeshaji wa bwawa hilo, ili kuwafanya waamini kuwa hilo ndilo tatizo. Hata hili, Ethiopia haikuwaruhusu kujadiliana, ili kuwadhalilisha zaidi, na kwa sababu inajua kwamba watawala wa Misri na Sudan hawana utashi kukabiliana na Amerika, ambayo Rais wake Trump alifichua kwamba ilikuwa nyuma ya bwawa hilo na ufadhili wake, aliposema katika Ikulu ya White mnamo 15/7/2025: “Nadhani Marekani ilifadhili bwawa hilo,” kabla hajatujalia kwamba alituachia maji katika Mto Nile, akiongeza: “Sijua kwa nini hawakutatua tatizo kabla ya kujenga bwawa hilo. Lakini ni vuzuri ikiwa Mto Nile una maji.
Nne: Ethiopia, ikiungwa mkono na Marekani na umbile la Kiyahudi, haitapumzika hadi Mto Nile utakapokauka kabisa na wawe na udhibiti kamili wa usalama wa maji wa nchi hizo mbili. Mkurugenzi Mtendaji wa Afisi ya Uratibu wa Bwawa laAn-Nahdha, Aregawi Berhe, alisema kwa vyombo vya habari mnamo Jumatano, 23/7/2025, akisema: “Bwawa la An-Nahdha sio mwisho wa barabara. Ethiopia haitatosheka na bwawa moja,” na hivyo kuashiria kuwa nchi yake inaendelea na ujenzi wa mabwawa mapya, ambayo ni Karadobi, Beko Abo na Mandaya, ambayo yanakadiriwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo bilioni 200 za maji, ikishajiishwa na msimamo dhaifu ya watawala wa Sudan na Misri.
Tano: Serikali hizi, iwe nchini Sudan, Misri, au Ethiopia, ni serikali za kiutendaji ambazo dhamira yake ni kutekeleza matakwa ya bwana wao katika Ikulu ya White House. Hivyo basi kupelekea misimamo ya dhaifu iliyochukuliwa na watawala wa Misri na Sudan kuhusu ujenzi wa bwawa hilo, licha ya hatari yake kwa watu wa Sudan na Misri na kupoteza haki zao za maji.
Hatimaye: Hebu watu wa Sudan na wajue kwamba serikali hizi za kiutendaji zinatumikia miradi ya Wakoloni makafiri wa Magharibi. Uvurugaji huu wa nchi yetu, rasilimali zake, na usalama wake wa maji utasitishwa tu na Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah hii itang'oa ushawishi wa wakoloni makafiri kutoka katika nchi yetu, itahifadhi usalama wa nchi na watu wake, na itasitisha uvamizi wa dola zisizo na umuhimu juu ya umma mtukufu ambao historia yake imeupamba ulimwengu.
Kwa hivyo, enyi watu wa Sudan fanyeni kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kumridhisha Mola wenu Mlezi, kwa ajili ya izza yenu, na kwa ajili ya kuishi kwenu kwa staha chini ya mfumo unaochunga mambo yenu na unaoangalia maslahi yenu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |