Jumatatu, 16 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  26 Safar 1447 Na: 1447 H / 01
M.  Jumatano, 20 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

“Maslahi Makuu ya Serikali” Yanakula Watoto Wake Yenyewe!
(Imetafsiriwa)

Chansela wa Ujerumani yuko chini ya shinikizo kutoka kwa kanuni ile ile ya kisiasa ambayo hivi majuzi aliitangaza kuwa “kiini cha uwepo wa Wajerumani.” Licha ya matamshi yake ya mara kwa mara ya kujitolea kikamilifu kwa kanuni ya maslahi makuu ya dola (ambayo ina maana ya uungaji mkono kamili kwa umbile la Kiyahudi), majeshi ya Kizayuni katika siasa na vyombo vya habari yanahamasisha juhudi za kuhujumu uamuzi wake wa hivi karibuni wa kuzuia usafirishaji nje wa silaha kwa umbile hilo kupitia mashambulizi yaliyoratibiwa!

Chansela Friedrich Merz, mwanzoni mwa kushika wadhifa wa uchansela, alitangaza bila shaka dhamira yake kamili kwa umbile la Kiyahudi na usalama wake, na alihoji waziwazi ulazima wa kutekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya Benjamin Netanyahu. Wakati huo, kila kitu kilionekana sawa katika anga ya kisiasa ya Berlin. Lakini hilo lilibadilika ghafla na taarifa iliyochapishwa na Chansela kwenye jukwaa la X mnamo Agosti 8: “Serikali ya Ujerumani, hadi itakapotoa maelezo zaidi, haitaruhusu usafirishaji wa zana zozote za kijeshi ambazo zinaweza kutumika katika Ukanda wa Gaza.” Ingawa Chansela alianza sentensi hii kwa kusema: “Kuachiliwa huru kwa mateka [...] ni jambo la kipaumbele kabisa na kwamba (Israel) ina haki ya kujilinda dhidi ya ugaidi wa Hamas,” dhoruba ya hasira ilizuka ndani ya dakika chache. Magazeti na vyombo vya habari—hasa miongoni mwao vile vilivyohusishwa na shirika la uchapishaji la Kizayuni Axel Springer—vilizungumza kuhusu “kufutwa kwa kanuni ya maslahi makuu ya serikali,” “kupoteza udhibiti wa kisiasa,” na “uhaini”! Baraza Kuu la Mayahudi nchini Ujerumani lilikwenda mbali zaidi kwa kufananisha uamuzi huo na kitendo cha uhasama moja kwa moja: “‘Israel’ inashambuliwa kila siku na maadui katika Mashariki ya Kati na inapigwa kwa makombora [...]. Kuinyima ‘Israel’ uwezo wa kujilinda dhidi ya vitisho hivyo kunaweka uhai wake hatarini.” Kulingana na Baraza Kuu la Mayahudi, serikali ya Ujerumani lazima “isahihishe njia ambayo imechukua haraka iwezekanavyo.”

Hata hivyo, hatari zaidi, ilikuwa ni mashambulizi kutoka ndani ya duara ya kisiasa ya Chansela mwenyewe... vyanzo vilivyoarifiwa vilionyesha “kuwa na wasiwasi” katika kambi yake ya bunge, katika baraza la mawaziri, na miongoni mwa “watu wenye ushawishi mkubwa” katika chama chake cha Christian Union. Mshirika wa karibu wa Chansela huyo, ambaye hakutajwa jina, alithibitisha kuwa “CDU iko motoni.” Markus Söder, kiongozi wa Christian Social Union (chama ndugu cha CDU huko Bavaria), alikataa kutoa uungaji mkono unaohitajika kwa Chansela. Badala yake, aliwatuma Alexander Hoffmann, kiongozi wa kundi lake la kieneo, Klaus Holetschek, kiongozi wa kundi la wabunge wa Bavaria, na Stefan Mayer, mtaalam wa sera za kigeni wa CSU, wakitaka kuhakikiwa kwa uamuzi huo na kufanyika kwa “mazungumzo ya ndani.” Roderich Kiesewetter, mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje ya CDU, aliutaja uamuzi huo kama “kosa kubwa la kisiasa na kimkakati.” Mbunge wa CDU Carsten Müller aliandika kwenye X kwamba “analaani vikali” uamuzi wa serikali ya Ujerumani. Huku kimya cha Katibu Mkuu wa CDU, Carsten Linnemann, kikiendelea, kiongozi wa kundi la wabunge wa chama hicho, Jens Spahn, hakutoa tamko lolote hadi siku chache baadaye, alipoeleza katika ujumbe wa video kwenye Instagram kwamba uamuzi huo, kwa maoni yake, “ulikuwa wa haki.”

Kulingana na mchanganuzi mmoja, kauli hii ilikuwa “njia ya chini zaidi ya uungaji mkono, na wakati huo huo namna ya juu zaidi ya kupinga ambayo kiongozi wa kundi la wabunge anaweza kuonyesha kwa chansela wake.”

Mashambulizi haya yalifuatana na taarifa kutoka kwa balozi wa umbile hilo, Ron Prosor: “Badala ya kuwapokonya silaha Hamas, sasa kuna mjadala wa kuipokonya silaha Israel; hii ni sherehe kwa Hamas.” Aliongeza: “Msimamo wa Berlin hauchangii mjadala halali juu ya mwelekeo mjini Gaza, lakini unalenga kuifanya 'Israel' kutokuwa na uwezo wa kujilinda.” Hatimaye, mnamo Agosti 10, Netanyahu mwenyewe alitoa taarifa kuhusu suala hilo, akimuonyesha Chansela dhaifu wa Ujerumani ambaye “alianguka chini ya mashinikizo ya vyombo vya habari ya kupotosha na mashinikizo ya ndani kutoka kwa makundi mbalimbali.” Kwa kuongezea, vyombo tofauti tofauti vya habari vilivyo na uhusiano na umbile la Kiyahudi vilianzisha mashambulizi yao wenyewe, vikichapisha tena, katika muktadha wa mjadala huo, matamshi dhidi ya Ujerumani ya Waziri wa Usalama wa Kitaifa Itamar Ben-Gvir: “Miaka themanini baada ya mauaji ya halaiki ya Mayahudi, Ujerumani kwa mara nyengine tena inaunga mkono Unazi.”

Kwa hivyo, kanuni ya “maslahi makuu ya serikali” inajitokeza sio tu kama fahamu “kinyume na misingi ya sheria” na “fahamu ya kiimla” (kama Kai Ambos anavyoelezea), lakini pia inatumika kama “chombo cha kudhibiti kitambulisho cha kisiasa” na athari yake inaenea “mbali zaidi ya Christian Union” (kulingana na Robin Alexander). Ingawa kura za maoni za hivi sasa zinaonyesha kuwa 83% ya Wajerumani wanaunga mkono kusitisha uuzaji wa silaha nje ya nchi na 76% wanakataa matendo yanayofanywa mjini Gaza, uhamasishaji mkubwa wa vyombo vya habari vya Kizayuni na wanasiasa wake unashambulia uamuzi wa Chansela wa Ujerumani na kutaka uhakiki wake! Katika muktadha huu, fahamu ya “maslahi makuu ya serikali” inatumiwa kama silaha madhubuti ya kisiasa ambayo inaweza kuelekezwa dhidi ya afisi ya juu zaidi ya kisiasa na mwakilishi wake – hata ikiwa wanatangaza waziwazi kuwa ndani yake na utiifu kamili kwa mradi wa Kizayuni!

Mkengeuko mdogo kutoka kwa mstari uliochorwa, ambao ni uungaji mkono kamili kwa umbile, moja kwa moja husababisha kampeni iliyoratibiwa kikamilifu inayoongozwa na mawakala wa ushawishi, wahalifu waliofunzwa kutenda kulingana na imani zao potovu zilizopandikizwa, na wadandiaji wanaotafuta mamlaka na ushawishi. Uhalisia huu unathibitishwa na utafiti kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Kupambana na Ugaidi na Usalama jijini The Hague, aliyesema hivi: “‘Israel’ hutekeleza kampeni za kimakusudi za kupotosha habari na kujaribu kuishawishi Uholanzi kisiasa.” Kiuhalisia, ufanisi wa kampeni kama hizo, kama shirika la Uholanzi lilivyozungumzia, unaongezeka nchini Ujerumani, na athari zao za kisiasa zinazidi kuwa za kina zaidi, kwa sababu wazo la maslahi makuu ya serikali – katika kazi yake ya utambulisho – limefungamanishwa na mchakato wa kuoanisha tena Ujerumani baada ya Vita Vikuu vya II na kuiunganisha kwa nguvu na Magharibi.

Hizb ut Tahrir kwa mara nyengine tena inaitaka serikali ya Ujerumani kutafakari upya kwa kina msimamo wake na kujinasua kutoka katika kushikamana kwake na umbile la Kiyahudi. Kilio cha kimataifa juu ya mauaji ya halaiki mjini Gaza, pamoja na rai jumla ya umma ya Ujerumani kupinga mauaji haya ya halaiki, yanaunda kwa pamoja fursa ya kihistoria ya kukombolewa kutoka kwa “tatizo la hatia ya milele” ambalo limefunga pingu maamuzi ya kisiasa ya Ujerumani kwa miongo kadhaa, na kuunda mabadiliko ya kweli katika sera ya Ujerumani kuelekea Mashariki ya Kati. Kwa msingi huu itaamuliwa iwapo Ujerumani itaweza kuungana tena na uhusiano wake wa kihistoria na ardhi za Kiislamu, au iwapo itaainishwa kama mtekeleza adui, aliyebeba mzigo wa kushiriki kwake katika mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina, na kuwajibishwa kwa hilo na Dola ya Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

[قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ]

“Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.” [Az-Zumar: 9]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Nchi Zinazozungumza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Ujerumani Yapoteza Fursa ya Kihistoria

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu