Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 6 Ramadan 1446 | Na: H 1446 / 094 |
M. Alhamisi, 06 Machi 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano wa Cairo, kama Watangulizi wake, Unadhihirisha Usaliti wa Watawala wa Kiarabu na Kuitelekeza kwao Gaza na Watu wake!
(Imetafsiriwa)
Mwishoni mwa mkutano wa dharura wa kilele wa Waarabu uliofanyika mnamo Jumanne, 4 Machi 2025, jijini Cairo, Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi alitangaza kutabanniwa kwa Mpango wa Mkutano wa Waarabu "Mpango wa Kujenga Upya Ukanda wa Gaza, ambao unaruhusu watu wa Palestina kubaki kwenye ardhi yao bila kuhamishwa makaazi yao." Taarifa ya mwisho ilisisitiza "umuhimu wa 'Israel' kuzingatia maazimio husika ya uhalali wa kimataifa ambayo yanakataa majaribio ya kubadilisha muundo wa idadi ya watu wa maeneo ya Palestina." Taarifa hiyo pia imelaani uamuzi wa kusitisha uingiaji wa misaada ya kibinadamu Gaza na kufungwa kwa vivuko. Kama kawaida, waliohudhuria hawakusahau kusisitiza tena "msimamo thabiti wa Waarabu kuhusu kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina kwenye mipaka ya Juni 4, 1967, huku Jerusalem Mashariki ikiwa kama mji mkuu wake, kama njia pekee ya kufikia amani ya kudumu katika eneo hilo."
Kwa hivyo, mkutano huo ulifanyika na kuhitimishwa bila kuchukua hatua yoyote ya maana kuhusu mauaji, njaa, na adhabu jumla iliyotolewa kwa watu wetu huko Gaza. Ilipuuza kabisa, au tuseme ilifumbia macho, vitisho vya Mayahudi na Amerika vya kusababisha jehanamu juu yao, badala yake ilijikita kwenye mijadala kuhusu siku baada ya vita dhidi ya Gaza—kana kwamba vita tayari vimekwisha na uvamizi umekoma!
Msimamo huu wa watawala wa Kiarabu unatokana na ukweli kwamba wazo la kuinusuru Gaza au kukabiliana na uvamizi wa Kiyahudi haliko mezani kwao kabisa. Mkutano wao ulikuwa ni jaribio la kubuni tu mpango badali ya mpango wa Trump wa kuwahamisha watu wa Gaza – baada ya kuwapa kibali cha kupendekeza mpango unaokidhi masharti yake kwa kuwaondoa Hamas katika utawala na kuiondoa kabisa katika ulingo wa kisiasa ili kuhakikisha usalama wa Mayahudi na kuzuia kurudiwa kwa matukio ya Oktoba 7, 2023. Hili lilithibitishwa waziwazi katika mkutano wao, ambapo mpango wa Misri ulifafanua uundwaji wa kamati ya kusimamia masuala ya Gaza katika kipindi cha mpito cha miezi sita. Kamati hii itakuwa huru na itajumuisha watu wasioegemea upande wowote (wajuzi) wanaofanya kazi chini ya mwavuli wa serikali ya Palestina, kwa lengo kuu la kuikabidhi Gaza kwa Mamlaka ya Palestina.
Zaidi ya usaliti na njama zao zilizotarajiwa, walisisitiza zaidi, kama kawaida, kujitolea kwao bila kuyumbayumba kwa mradi wa makubaliano na kujisalimisha unaojulikana kama "mchakato wa amani" na suluhisho la dola mbili. Kwa kufanya hivyo, wanajishuhudia dhidi yao wenyewe katika siku hizi zilizobarikiwa za mwezi mtukufu, wakithibitisha kwamba Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri nyoyo na masikio yao ili wasiweze kufahamu, kutimiza maneno yake:
[خَتَمَ اللهُ عَلَى قُلُوبِهمْ وَعَلَى سَمْعِهِمْ وَعَلَى أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ عظِيمٌ]
“Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa.” [Al-Baqara:7].
Kwa hivyo, watawala hawa wanathibitisha kwamba wao si chochote zaidi ya ala duni za kutekeleza njama za Amerika, Magharibi, na Mayahudi. Hawafikirii hata kujadili mambo ambayo hawajapewa ruhusa kuyashughulikia. Kwa hiyo, haikushangaza pindi uvujaji habari ulipofichua kwamba wapatanishi walikuwa wameingilia kati pamoja na Mayahudi, wakiwataka waepuke hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Gaza kabla ya mkutano huo—ili tu kuwasaidia watawala hao kuokoa kipande kidogo cha adhama yao!
Gaza haihitaji mipango zaidi inayoiweka chini ya ukaliwaji kimabavu na udhibiti wa Mayahudi. Kinachohitaji kwa hakika ni hatua ya dhati kutoka kwa Ummah na majeshi yake ili kuinusuru na kuikomboa kutokana na mitego ya Mayahudi na Marekani. Bila haya, tutaendelea kuwahesabu mashahidi na majeruhi, tukishuhudia unajisi na kiburi cha Mayahudi—wakati wote huku watawala wa Waislamu wakiendelea kuusaliti Umma na utumwa wao kwa Amerika.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |