Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 18 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 089 |
M. Jumatatu, 17 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala wa India Wanatumia Sheria ya (Kuzuia) Shughuli zisizo halali ya 1967 kupiga Vita Uislamu na Waislamu, wakimwemo Mashababu wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Katika kampeni yake inayoendelea dhidi ya Hizb ut Tahrir, Shirika la Kitaifa la Upelelezi la India lilimkamata Bava Bahrudeenand Kabeer Ahmed Aliyar mnamo 3 Februari 2025, baada ya miezi kadhaa ya unyanyasaji. Vyombo vya habari vya India viliripoti kwamba "walikula njama na wengine kueneza fikra ya Hizb ut Tahrir huko Tamil Nadu, ambalo ni shirika lililopigwa marufuku." Kisha mamlaka zikanasibisha kesi yao na kesi inayoendelea ya Dkt. Hameed Hussain chini ya Sheria ya (Kuzuia) Shughuli Zisizo Halali (UAPA) ya 1967!
Kuhusu Dkt. Hameed Hussain, ana Shahada ya Uzamivu katika Uhandisi wa Mitambo na ni mwanajamii anayeheshimika. Alikamatwa Mei 2024 kwa kutoa maoni yake juu ya Uislamu kukataa demokrasia, utawala bora wa Khilafah katika kuwajali raia wake bila kujali rangi au dini, na suluhisho la Kiislamu kwa ukandamizaji unaowakabili watu walio wachache na tabaka la chini kabisa la Dalit. Licha ya maoni yake chanya na yenye kujenga, yeye ndiye mshukiwa mkuu katika kesi chini ya Sheria ya (Kuzuia) Shughuli zisizo halali ya 1967!
Sheria hii ni ala ya dhulma inayotumiwa na watawala wa India kuzuia kuhesabiwa. Ni sheria kandamizi ambapo mchakato wa kuwekwa kizuizini na kesi yenyewe hutumika kama adhabu. Ukweli huu ni dhahiri kutokana na kiwango chake cha chini cha kutisha cha 2%. Kati ya 2016 na 2020, kesi 5,027 zilisajiliwa chini ya sheria hii dhidi ya watu 24,134. Kati yao, ni 212 tu waliopatikana na hatia, huku 386 wakiachiliwa huru. Hii ina maana kwamba kuanzia 2016 hadi 2020, 97.5% ya waliokamatwa chini ya sheria hii walibaki gerezani wakisubiri kesi zao! Je, rekodi hii haitoshi kuitishwa kufutwa kwa sheria hii kandamizi?
Licha ya rekodi yake ya kutisha, mnamo Julai 2019, watawala wa India walianzisha marekebisho ya UAPA, na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Sheria iliyorekebishwa inaruhusu mamlaka kuainisha watu binafsi kama "magaidi" bila utaratibu wa kisheria. Uteuzi huu husababisha kutengwa kwa jamii na upotezaji wa kazi. Marekebisho hayo wala sheria asili hayatoi ufafanuzi kamili wa ugaidi. Hivyo, sheria iliyofanyiwa marekebisho ni leseni ya wazi kwa serikali kukandamiza na kutisha watu kwa kisingizio cha kudumisha utulivu wa umma. Ni dhuluma ambayo inapingana na sheria kandamizi zilizowekwa na wakoloni wa Uingereza wakati wa utawala wao dhalimu juu ya India.
Watawala wa kimadhehebu wa India wametumia Marekebisho ya UAPA ya 2019 kueneza hofu kati ya mamia ya mamilioni ya Waislamu nchini India. Waislamu walipopaza sauti zao kupinga Sheria kibaguzi ya Marekebisho ya Uraia ya 2019, serikali ililipiza kisasi kwa kuwaweka kizuizini wanafunzi wa Kiislamu na wanaharakati, akiwemo mwanamke mjamzito, chini ya UAPA. Waislamu wengi wanabaki kizuizini bila kufunguliwa mashtaka. Kisha, mnamo Oktoba 2024, Serikali ya India ilitoa taarifa katika gazeti rasmi la serikali kupiga marufuku Hizb ut Tahrir, chini ya Sheria ya Kuzuia Shughuli zilizo Kinyume cha Sheria, 1967.
Kwa Watu wa India kwa jumla, na kwa Ndugu zenu kutoka kwa Wataalam wa Sheria na Mashirika ya Haki za Kibinadamu haswa!
Watawala wa India wamekuleteeni uharibifu, umaskini, ukosefu wa usalama, ubaguzi, na migawanyiko ya kijamii. Yeyote kati yenu akipaza sauti kwa ajili ya haki yake, watawala wanakuadhibuni. Je, hivi ndivyo babu zenu walivyofikiria walipopigania uhuru kutoka kwa ukandamizaji wa wakoloni? Je, huu ndio mfano munaotaka kuwasilisha mbele ya macho ya ulimwengu? Hakuna sheria, ya kimungu au iliyoundwa na wanadamu, ambayo inaweza kukubali ukandamizaji huu.
Enyi Watu wa India: Kumfumbia macho dhalimu kunamshajiisha kuendelea na dhulma yake, ilhali kusimama dhidi yake ni mwanzo wa mwisho wa dhuluma.
Kwa Waislamu wa India kwa jumla, na kwa Wanachuoni wenu hasa!
Tazameni mateso, umaskini, na taabu za watu wanaokuzungukeni. Je, nyinyi hamna jukumu kwao kwa mujibu wa Dini yenu? Mwenyezi Mungu (swt) alimtuma Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama rehma kwa walimwengu. Babu zenu waliitawala India kwa uadilifu wa Uislamu kwa karne nyingi, wakitoa usalama na ustawi ambao haukuwahi kuonekana kabla ya Uislamu na hawajawahi kuona kitu kama hicho tangu wakati huo. Leo, ni Dini ya Uislamu pekee ndiyo inayoweza kuwakomboa watu wa India kutokana na ukandamizaji wa mfumo ulioundwa na mwanadamu.
Je, ni sawa kuweka kikomo maono yenu ya kushiriki katika mfumo huu dhalimu kwa matumaini ya kupata afueni fulani kwa ajili yenu?! Je, ni sawa kukimbizana na viti vichache vya ubunge badala ya kujitahidi kurudisha uongozi wa Uislamu nchini India?! Je, ni sawa kwa madhalimu kufanya kazi ya kuzima ulinganizi wa Uislamu, na nyinyi mukae kimya?
Nyinyi sio madhaifu wala si wachache kiidadi, nyinyi ni wengi na wenye nguvu ikiwa mtashikamana na Dini yenu na kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt). Ulinganizi kwa dini ya haki ya Uislamu pekee ndio utakaokuunganisheni kuwa nguvu madhubuti ya mabadiliko yanayohitajika sana nchini India. Inukeni, enyi Waislamu wa India, kwani Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi.
[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [Surat At-Tawba:32]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |