Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 16 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 087 |
M. Jumamosi, 15 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Msiikubali Marekani kama Mpatanishi,
Kwa Maana sio tu kuwa ina Upendeleo; bali, ni Sehemu ya Mzozo!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Januari 15, makubaliano yalifikiwa kusitisha vita dhidi ya Gaza kati ya umbile la Kiyahudi na harakati ya Hamas. Makubaliano hayo yalianza kutekelezwa mnamo Januari 19 mwezi huo huo na yalisimamiwa na nchi tatu: Amerika, Misri na Qatar. Tangu wakati huo hadi leo, umbile la Kiyahudi limetekeleza ukiukaji mwingi wa makubaliano haya na limeshindwa kutimiza wajibu wake mwingi, kama ilivyo kawaida kwa Mayahudi katika khiyana na uvunjaji ahadi na makubaliano.
Hili lilisababisha Hamas na pande zinazopigana pamoja nayo kutishia kutowasalimisha wafungwa wa Kiyahudi waliokubali kuachiliwa huru mnamo siku ya Jumamosi, Februari 16, isipokuwa umbile la Kiyahudi litii kikamilifu masharti yote yaliyokubaliwa. Tishio hili lilitolewa siku tano kabla ya tarehe iliyopangwa ya kuachiliwa huru ili kuwapa wapatanishi fursa ya kushinikiza umbile la Kiyahudi kutimiza ahadi zake. Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump alijibu kwa kutishia kuwasha moto Gaza na watu wake ikiwa Hamas haitawaachilia huru wafungwa wote ifikapo saa sita mchana Jumamosi. Tishio hili lilitolewa na Trump mwenyewe na maafisa kadhaa wa Amerika, licha ya ukweli kwamba walipaswa kuwa wapatanishi katika makubaliano. Maafisa kadhaa kutoka umbile la Kiyahudi pia walikubali tishio hili.
Sasa, swali linazuka: Je, inakubalika kwa mpatanishi kutoa vitisho kwa mmoja wa wahusika katika makubaliano hayo, na hivyo kupitiliza katika dori yake ya kuwa mpatanishi asiyeegemea upande wowote na badala yake kuwa mshiriki katika mzozo huo?
Ukweli usiopingika ni kwamba Marekani ni sehemu ya mzozo, sio mpatanishi. Ni mshirika mkubwa wa umbile la Kiyahudi, ndiye aliyeipatia silaha na risasi zilizotumiwa kuharibu Gaza na kuwaangamiza watu wake. Imetoa hifadhi ya kisiasa kwa uhalifu wake na inaendelea kufanya hivyo. Amerika ndiyo inayopigia debe kuhamishwa kwa wakaazi wa Gaza kwenda Misri, Jordan, na maeneo mengine, ikitangaza wazi nia yake ya kuchukua udhibiti wa Gaza baada ya kuwaondoa watu wake ili kuanzisha miradi yake ya kiuchumi. Pia Amerika ndiyo iliyopeleka manuari na vikosi vya jeshi la wanamaji kwenye eneo hilo, ikihofia kutokea kwa harakati yoyote ya dhati kutoka kwa majeshi ya Waislamu.
Haya yote yameidhihirisha Marekani kama adui msingi na mkubwa zaidi wa Umma wa Kiislamu, huku umbile la Kiyahudi likitumika tu kama mojawapo ya ala zake katika uadui huu, wenye lengo la kuzuia umoja wa Umma na kusimamishwa kwa Khilafah.
Baada ya yote haya, je, Waislamu bado wanaweza kuikubali Marekani kama mpatanishi katika mapatano yoyote kati yao na maadui zao? Je, wanaweza kutarajia adui yao mkubwa zaidi, Amerika, kuwa mpatanishi asiye na upendeleo anayelinda haki zao?
Tahadharini enyi Waislamu! Kuweni waangalifu enyi Mujahidina! Msiruhusu Marekani, mkuu wa Ukafiri kuwa mpatanishi kati yenu na maadui zenu. Badala yake, itambueni kama adui na jihadharini nayo. Msiifanye kuwa mdhamini wa haki zenu, kwani ndiyo nguvu ile ile iliyo nyuma ya kugawanya nchi zenu, kuwaunga mkono watawala wenu wasaliti, na kupora mali zenu, na kulitumia umbile la Kiyahudi kama mkuki ndani ya moyo wa ardhi zenu—ikilipa njia zote za uhai, nguvu, na utawala juu yenu.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |