Jumamosi, 23 Sha'aban 1446 | 2025/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  13 Sha'aban 1446 Na: H 1446 / 085
M.  Jumatano, 12 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kushutumu kwa Watawala wa Waislamu Mradi wa Kuwahamisha Watu wa Gaza hakufuti Upeo wa Aibu wa Usaliti wao
(Imetafsiriwa)

Usaliti wa watawala wa Waislamu, na majeshi yao, kwa watu wa Gaza, na Palestina yote, kwa zaidi ya miaka 78 ya kukaliwa kwa mabavu Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na umbile la Kiyahudi, ni fedheha kubwa. Haiwezi kufutwa kwa shutuma tu za kuhamishwa. Watawala hawa wameficha usaliti wao mkubwa katika kipindi cha miezi kumi na tano iliyopita. Nchi kadhaa zimeelezea kukataa mipango ya kuwahamisha watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kutoka Ukanda wa Gaza, hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alisema mnamo Jumatatu, 10 Februari, "Hakuna mtu anayeweza kuwasukuma watu wa Palestina kuelekea Nakba mpya ya uhamisho." Erdogan alisisitiza kwamba "ukaliaji kimabavu wa 'Israel' lazima ubebe gharama ya ujenzi mpya wa Gaza peke yake," akionya dhidi ya "jaribio lolote la kuwalazimisha watu wa Palestina Nakba mpya ya uhamisho."

Watawala wengine wa Waislamu walimtangulia Erdogan katika kukataa, wakiwemo watawala wa madhara wa nchi za Kiislamu, karibu na mbali. Wa kwanza kati ya hawa, walikuwa watawala wa Jordan na Misri, kufuatia ombi la Trump la kuwapokea Waislamu waliohamishwa kutoka Gaza. Hii ilifuatiwa na wengine kama vile bin Salman, Waziri Mkuu wa Pakistan, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Muhammad Ishaq Dar, ambao wamelaani vikali kauli ya Waziri Mkuu wa umbile la Kizayuni kuhusu kuwahamishia Wapalestina Saudi Arabia kama "zisizo na msingi, uchochezi na kutokuwa na mawazo," akisisitiza kwamba "pendekezo lolote linalotaka kuwaondoa au kuwahamisha watu wa Palestine kutoka nchi ya mababu zao halikubaliki."

Haikutarajiwa kamwe kutoka kwa watawala hawa vibaraka kuwa wangefanya zaidi ya yale ambayo kwa kawaida hufaulu kufanya, ambayo ni kulaani, au kuitisha mikutano na makongamano, ambapo hufuja mamilioni ya dolari ya utajiri wa Ummah kwa anasa na starehe zao, na kuibuka tu na matokeo ambayo yanadhuru Uislamu, Waislamu, na malengo ya Ummah. Je, Erdogan, mtawala wa Uturuki, kwa mfano, anawezaje kutarajiwa kuwanusuru watu wa Gaza, baada ya kuwasaliti kwa muda wa miezi 15 kamili? Anawezaje kutarajiwa, wakati Uturuki ndio nchi pekee ya Waislamu katika muungano wa NATO? Erdogan ametia saini mikataba sitini kati ya Uturuki na umbile la Kiyahudi la Kizayuni wakati wa utawala wake. Zaidi ya hayo, kuna kambi mbili za kijeshi za umbile la Kiyahudi la Kizayuni nchini Uturuki, mjini Konya na Izmir. Ubadilishanaji wa biashara kati ya umbile la Kizayuni na Uturuki yalizidi dolari bilioni 9 mwaka 2022, huku zaidi ya watalii nusu milioni kutoka umbile la Kiyahudi wakizuru Uturuki kila mwaka. Uturuki inawaruhusu watalii kutoka umbile la Kiyahudi kuingia bila viza, huku ikiweka masharti magumu ya kabla ya visa kwa watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Zaidi ya hayo, Uturuki ni mwenyeji wa kiwanda cha pili kwa ukubwa cha kijeshi cha "Israel" duniani. Mtu yeyote mwenye akili timamu anawezaje kuamini kwamba shutuma za Erdogan ni ushindi kwa, Gaza au ni ukataaji wa dhati wa njama za Trump?

Mfano mwingine wa kufedhehesha ni Pakistan, nchi pekee ya Kiislamu inayomiliki silaha za nyuklia, na makombora ya balestiki yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia. Pakistan inaweza kuangamiza umbile la Kizayuni kwa makombora machache. Hakika kombora moja tu lingetosha kuondoa minong'ono ya Shetani! Je, mtu yeyote anawezaje kuamini kwamba kulaani kwa Waziri Mkuu wa Pakistan, au ghadhabu tu, juu ya kuhamishwa makaazi yao ni ya dhati, wakati hajainua hata kidole kukomesha mauaji ya makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia huko Gaza, au kubonyeza kitufe kufyatua hata kombora moja? Hali ya watawala wengine wa Waarabu na Waislamu haina tofauti na wale wa Uturuki na Pakistan. Wote ni waongo wanafiki, wanatamka yale tu aliyoyaruhusu bwana wao Ikuluni White House.

Wajibu wa Shariah kwa nchi za Kiislamu na majeshi yao kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina sio kukemea uhamishaji peke yake. Wajibu wa Shariah ni kukusanya vikosi vyao vya majeshi ili kuikomboa Palestina, kulipiza kisasi kwa watu wake ambao wameuawa, kuteswa, na kufungwa. Hili linaweza kupatikana tu kwa kuwang'oa hawa watawala vibaraka waliopandikizwa na Magharibi kwa Ummah. Watawala hawa ndio wanaolikinga umbile la Kiyahudi kutokana na ghadhabu ya Ummah. Ukombozi unaweza kupatikana tu kwa kusimamisha Khilafah Rashida, inaotawala kwa sharia ya Mwenyezi Mungu na kuyakusanya majeshi ya Waislamu kuikomboa Ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na Al-Masjid Al-Aqsa, kwa ajili ya Umma wa Kiislamu. Kwa hiyo, maafisa wanyoofu wa majeshi ya Ummah lazima waipe Nusrah Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume. Kwa kufanya hivyo, watatekeleza wajibu wao wa Shariah, na kujikinga na udhalilifu duniani, na adhabu kesho Akhera. Iwapo watasitasita na kushindwa, Mwenyezi Mungu (swt) hatashindwa katika ahadi yake ya kuupa ushindi Uislamu, Waislamu, na ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa:

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ * يَوْمَ لَا يَنْفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi, Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makaazi mabaya kabisa.” (Surah Ghafir 51-52)

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu