Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 10 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 084 |
M. Jumapili, 09 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Urusi Yajaribu Kubandika Shtaka la Ugaidi kwa Chama Kinachoheshimika zaidi cha Kisiasa ili Kuhalalisha Ukandamizaji na Kufilisika kwake!
(Imetafsiriwa)
Chini ya kichwa cha habari: "Huduma ya Usalama ya Urusi yakamata seli ya kigaidi yenye uhusiano na Hizb ut Tahrir," Russia Today ilichapisha ripoti mnamo 5 Februari 2025, ikisema kwamba "Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi ilisambaratisha seli ya kigaidi yenye uhusiano na Hizb ut Tahrir huko Crimea na kuwakamata watu watano ambao walikuwa wakisajili wafuasi wa chama hicho, ambacho kimepigwa marufuku nchini Urusi." Video ilionyeshwa inayoonyesha operesheni ya ukamataji na uvamizi wa nyumba.
Ilikuwa wazi katika video hiyo kwamba kilichopatikana katika nyumba za Mashababu ni nakala za Quran Tukufu, vitabu, na vijitabu vya kifikra na kisiasa vya Kiislamu—machapisho ya Hizb ut Tahrir ambayo yanasambazwa duniani kote na kujulikana sana kwa maudhui yake. Picha za ukamataji pia zilionyesha kuwa nyumba za hawa mashababu zilikuwa za kawaida, zisizo madhubuti, na zisizo na tashwishi. Wakaazi wake walifungua milango yao wakiwa wamevalia nguo za kiraia zenye staha, wengine hata wakiwa wamevalia nguo za kulalia, bila kuonyesha upinzani au vurugu. Baada ya msako huo, hakuna silaha wala zana zozote za vurugu au ugaidi zilizopatikana, jambo ambalo lilitarajiwa na kujulikana.
Hizb ut Tahrir, katika maeneo yake yote ya utendaji katika nchi mbalimbali, inabakia kuwa Hizb ile ile katika fikra na njia yake, ambayo haijaibadilisha wala kuigeuza. Inafuata njia ile ile ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu—mwelekeo wa kifikra wa hali ya juu na wa kisiasa, ambao ndani yake hakuna nafasi ya vurugu au ugaidi. Huu ni ukweli unaojulikana vyema kuhusu Hizb, unaotambuliwa na watafiti, tafiti, na wachunguzi sawia, na haijawahi kuthibitishwa kwamba Hizb ilijihusisha na vitendo kama hivyo.
Jaribio la utawala wa Urusi la kuituhumu Hizb na wanachama wake kwa ugaidi ni juhudi ya kutapatapa inayoendeshwa na kufilisika kwake kifikra na lenye lengo la kuhalalisha ukandamizaji wake dhidi ya Hizb huku ikitamausha jamii kutokana na kuiunga mkono—hasa inapoona hadhi na heshima waliyo nayo Waislamu huko kwa Hizb na wanachama wake. Hata hivyo, ni kwa jinsi gani utawala wa Urusi unaweza kupotosha sura ya Hizb au kuharibu sifa yake wakati inabaki bila doa na safi, bila dosari yoyote?
Mashababu wa Hizb watabaki imara katika ahadi zao kwa yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu, na kwa Msaada Wake, Hizb itaendeleza kazi yake ya kifikra na kisiasa hadi Mwenyezi Mungu atakapoijaalia ushindi na kuiwezesha kuregea maisha kamili ya Kiislamu chini ya Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume, ikieneza Uislamu kama dini ya rehema, uadilifu, na utulivu, ili mataifa yasilimu makundi kwa makundi, wakikimbia ukandamizaji wa urasilimali na dhulma ya watawala, na ili watu wapambanue haki na batili.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللهِ شَهِيداً]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.” [Al-Fath 48:28].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |