Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 4 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 081 |
M. Jumatatu, 03 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maamuzi ya Mikutano ya Mawaziri wa Kiarabu ni Matupu na Hayatapita zaidi ya Maandishi kwenye Karatasi
(Imetafsiriwa)
Mkutano wa Mawaziri wa Pande Sita wa Kiarabu jijini Cairo mnamo Jumamosi, 1 Februari 2025, kuhusu Gaza na Kadhia ya Palestina ambayo ni pamoja na Jordan, Imarati, Saudi Arabia, Qatar, na Misri, pamoja na Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu - walithibitisha katika taarifa yao kile walichokiita "uungaji mkono wao kamili wa watu wa Palestina juu ya ardhi yao na kuzingatia haki zao halali kwa mujibu wa sheria ya kimataifa." Pia walionyesha kupinga kwao "ukiukwaji wowote wa haki hizo zisizoweza kutenganishwa, iwe kupitia shughuli za makaazi, kufukuzwa na kubomolewa kwa nyumba, unyakuzi wa ardhi, au kwa kuwaondoa wamiliki kwenye ardhi yao kwa njia ya kuwahamisha, kuhimiza uhamisho au kung'olewa kwa Wapalestina kutoka kwa ardhi yao kwa namna yoyote, kwa dhurufu zozote au hoja zozote."
Yeyote anayechunguza maamuzi ya mkutano huu anaweza kuona kwa uwazi kwamba ni matupu na yana wino tu kwenye karatasi, hayana mpango wowote wa utekelezaji au programu ya utendaji. Waliohudhuria walithibitisha uungaji mkono wao kamili kwa watu wa Palestina na haki zao, lakini walifanya maregeleo ya haki hizi kuwa sheria ya kimataifa ambayo kila mtu anajua inatawaliwa na Marekani na dola za kikoloni ambazo iliwawezesha Mayahudi kuinyakua Palestina na kuweka udhibiti juu yake. Zaidi ya hayo, hawakuonyesha jinsi wanavyokusudia kutekeleza uungaji mkono wao kamili kwa Palestina na watu wake, ikithibitisha kwamba kauli zao si chochote zaidi ya maneno ya kulaani, kupinga na kutokubali.
Palestina inakabiliwa na uvamizi wa kikatili na vita vya kinyama, na njia ya kuinusuru na kuilinda ni kwa kuhamasisha majeshi, kung'oa uvamizi huo na kuikomboa. Kukabiliana na njama chafu za Trump, ambazo zinatishia eneo hilo kwa uharibifu ikiwa halitalingana na mipango na programu zake, haziwezi kupatikana kwa kauli tu za kulaani, kupinga, na kuthibitisha upya, wala kupitia matamko matupu ya mawaziri.
Kama kawaida, waliohudhuria hawakusahau kuthibitisha tena idhini na uungaji mkono wao kwa mradi wa kujisalimisha na makubaliano, unaojulikana kama suluhisho la dola mbili, na kupendekeza kuanzishwa kwa dola ya Palestina ndani ya mipaka ya Juni 4, 1967. Hii inaweka wazi kwa kila mtu kwamba matarajio yao ya juu ni kuomba ufumbuzi wa kujisalimisha kutoka kwa mpiganaji wa kimsalaba mhalifu Amerika.
Watawala hawa wataendelea kusalimu amri kwa matakwa ya wakoloni, na hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuwategemea wao au nyadhifa zao dhaifu. Tangu wakoloni walipowaweka juu yetu, wamekuwa na sifa ya udhalilifu na unyenyekevu kwa gharama ya maslahi na sababu za Ummah. Kwa hiyo, watu wote wenye ikhlasi katika Ummah, hasa ndani ya majeshi yake, lazima washirikiane nasi ili kuregesha mamlaka ya Ummah na kusimamisha Khilafah yake, ambayo itaikomboa Palestina na kukabiliana na dola zote za kikoloni. Hapo ndipo tutakaporegea kuwa Ummah wenye hadhi na heshima, usiotawaliwa tena na viongozi wasio na umuhimu na wasiostahili.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[إِنَّ الأَرْضَ لِلّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ]
“Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho mwema ni kwa wachamngu.” [Al-A'raf:128].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |