Jumanne, 24 Shawwal 1446 | 2025/04/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  19 Ramadan 1446 Na: H 1446 / 095
M.  Jumatano, 19 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yaanzisha Mashambulizi ya Kikatili kwa Yemen Huku Majeshi Yetu Yakitulia tuli, Yakishindwa Kuinusuru Yemen na Gaza!
(Imetafsiriwa)

Kwa siku nyingi sasa, Amerika imekuwa ikianzisha mashambulizi ya kikatili kwa watu wetu nchini Yemen, kwa kutumia kile Rais wa Marekani Trump alichoeleza kuwa "nguvu kuu mbaya." Alikuwa amewatisha hapo awali, akichapisha, “JAHANAM ITANYESHA JUU YENU KWA NAMNA AMBAYO KWAME HAMJAWAHI KUONA KABLA!!”

Hivi ndivyo Marekani inavyotenda kwa kiburi na majivuno dhidi ya Waislamu na ardhi zao, wakiwatishia moto wa Jahannam na vita vya kuangamiza pasi na kujali kabisa kwa watawala wa Waislamu, majeshi yao, na uwezo wao. Wanalipua mabomu ardhi zetu, wanaua watu wetu, na kukiuka matukufu yetu kwa urahisi, bila kuzingatia majibu yetu au kujali majibu yetu!

Ama viongozi wa Iran, ambao kwa muda mrefu wamejigamba kuunga mkono upinzani na kuitangaza Marekani kuwa ni “Shetani Mkuu,” sasa wanawakana washirika wao wa Kihouthi kana kwamba hawajawahi kuwepo, na kuwaacha kuwa mawindo rahisi kwa Mayahudi na Marekani!

Wakati huo huo, Amerika inatafuta kulazimisha muundo wa usaliti na kutochukua hatua, hata kwa wale wanaoitwa watetezi wa "upinzani". Baada ya kuwalazimisha Hizb ya Iran nchini Lebanon kuachana na makabiliano yao na Mayahudi na kuilazimisha Iran iondoe uungaji mkono wake kwa Gaza na makundi yenye upinzani - licha ya miaka mingi ya kudai kuwaunga mkono - sasa inalenga kuwalazimisha Mahouthi kuachana na makabiliano yao na Mayahudi na vitisho vyao kwa maslahi ya kiuchumi katika Bahari Nyekundu, na kuiacha Gaza ikiwa imetengwa kukabiliana na ukatili wa Mayahudi na Trump pekee yake.

Uhalisia ambao Amerika inatafuta kuuanzisha chini ya uongozi mpya wa Trump ni rahisi: kujisalimisha au kifo. Ikiwa Waislamu na majeshi yao hawataamka kutoka katika usingizi wao wa muda mrefu, hatima mbaya inawangoja. Trump atahamia nchi zao moja baada ya nyingine, mradi tu hakuna atakayesimama kumzuia na kumlazimisha kurudi nyuma - jambo ambalo analitangaza waziwazi bila kuficha chochote.

Hivyo basi, wenye ikhlasi miongoni mwa majeshi ya Waislamu hawana budi kuinuka haraka kuunusuru Uislamu na Waislamu, kukabiliana na Mayahudi, Marekani, na nguvu zote za ukafiri kabla hazijaangamiza ardhi zetu, na kutuacha tukiomboleza katika wakati ambapo hakuna njia ya kutoroka!

Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu