Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 22 Ramadan 1446 | Na: H 1446 / 098 |
M. Jumamosi, 22 Machi 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yatoa Tahadhari kuhusu Alfajiri ya Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume
(Imetafsiriwa)
Kila wakati Umma unapopiga hatua kuelekea ukombozi kutoka kwenye nira ya ukoloni unaolemea sana kifua chake, na kutaka kujikomboa kutoka kwenye himaya ya Magharibi, dola za Magharibi hutoa tahadhari, zikihofia kwamba juhudi za waumini wa kweli wa Ummah zitafikia kilele kwa kuasisiwa Khilafah Rashida, kama ilivyotolewa bishara njema na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kwa hivyo, Amerika na muungano wake wa Makruseda walijipanga, baada ya kukimbia kwa dhalimu wa Syria, Bashar al-Assad, na kuingia kwa wanamapinduzi jijini Damascus. Walituma mjumbe baada ya mjumbe, wakuu pamoja na wa vyeo vya chini, wanaowakilisha serikali zao, ili kudhibiti tukio ambalo Amerika na muungano wake wa Makruseda walikadiria kuwa muhimu. Endapo maji yatazidi unga, matokeo hayatakuwa mazuri kwa makafiri.
Kwa upande wa Mashariki mwa Ulimwengu wa Kiislamu, nchini Bangladesh, Marekani na kibaraka wake India wamekuwa wakifuatilia kwa makini hali ya huko, kwa wasiwasi mkubwa, baada ya kutoroka dhalimu Hasina, wakihofia kwamba hali ya huko ingegeuka na kuupendelea Uislamu na wafuasi wake. Wanajua kuwa Uislamu ndio chaguo pekee ambalo nyoyo za Waislamu duniani kote, ikiwemo Bangladesh, zingeweza kuugeukia, iwapo wangeachwa wafanye mambo yao wenyewe, bila ya kuingiliwa na watawala wa Waislamu, vibaraka wa nchi za Magharibi. Kwa hiyo, Amerika ilimtuma mtu wake, Muhammad Yunus, kutoka uhamishoni ili kudhibiti uasi wa wanafunzi ambao ulilazimisha jeshi la Bangladeshi kumpindua dhalimu Hasina, na kumsafirisha kisiri hadi India.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha India NDTV, Tulsi Gabbard, Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani, alidai kuwa mateso na mauaji ya watu wa dini za walio wachache nchini Bangladesh na "tishio la magaidi wa Kiislamu" nchini humo "vinatokamana na fikra na lengo moja - ambalo ni kuhukumu au kutawala kwa Khilafah ya Kiislamu." Sasa, kauli hizi zilikuja baada ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh kuandaa "Matembezi ya Khilafah" mnamo siku ya Ijumaa, Machi 7, 2025, ili kuwakumbusha watu juu ya kuvunjwa kwa Khilafah, na kuwalingania kufanya kazi kuelekea kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Matembezi hayo pia yalikuwa ni barua ya wazi kwa watu wenye mamlaka na ulinzi wa nchi hiyo, ikiwataka kutoa Nusrah (msaada wa kimada) kwa Hizb katika juhudi zake za kusimamisha Khilafah, katika kumbukumbu ya kuvunjwa kwake. Licha ya serikali ya mpito kukandamiza matembezi hayo kikatili, hili halikumsaidia mtu wa Marekani, rais wa mpito wa Bangladesh, Muhammad Yunus, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, na rafiki mwaminifu wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton kwa miaka arubaini. Serikali yake ya muda ilifurahia baraka za serikali ya Marekani, baada ya kukutana na Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden jijini New York.
Vibaraka wa wakoloni hujitahidi kuishi kulingana na matarajio ya mabwana zao. Kwa hivyo majibu ya serikali ya mpito ya Bangladesh kwa taarifa za Tulsi Gabbard yalikwenda mbali zaidi kuliko ilivyotarajiwa, ikisema kwamba "Taarifa hii inapotosha na inaharibu sura na sifa ya Bangladesh, taifa ambalo mila yake ya jadi ya Uislamu imekuwa maarufu na yenye amani na ambayo imepiga hatua za ajabu katika mapambano yake dhidi ya itikadi kali na ugaidi." Serikali ya mpito ya Bangladesh na watu wake wenye ushawishi wa kina imejitolea kikamilifu katika vita dhidi ya Uislamu, na kuzuia kurudi kwa Khilafah nchini humo. Ahadi hii si mpya. Ahadi hii imejikita katika njia ya kisiasa ya Bangladesh, ambayo haijabadilika kwa kukimbia kwa dhalimu Hasina. Badala yake, watu wenye ushawishi wa kina katika serikali wamedumisha uaminifu wao wa zamani kwa Magharibi, kuwasiliana na balozi za Magharibi na dola za kikoloni na kupokea mwongozo kutoka kwao, kama ilivyokuwa wakati wa Hasina. Kwa hiyo, jibu lake lilikuwa ni kukanusha kauli za Gabbard, ambazo ziliwashutumu kwa uzembe, wakati wao walikuwa wakifanya kila wawezalo kuupiga vita Uislamu na kukandamiza Da’wah kwa ajili ya Khilafah.
Kile ambacho watawala wa Waislamu, wakiwemo wale wa Bangladesh na dola washawishi wake wa kina, wanashindwa kuelewa, ni kwamba Marekani inatishwa na kutajwa tu Uislamu katika nchi za Waislamu. Wakati Marekani mara nyingi huwaamini watawala, na mara chache hutangaza waziwazi, inaichukulia Dawah ya kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu nchini Bangladesh na nchi nyingine za Kiislamu kwa umakini, si kama mzaha. Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani na nchi yake wanajua vyema kwamba Uislamu ni njia bora, iliyostaarabika badali ya hadhari yao ya Kimagharibi yenye ulafi na upotovu. Lau watetezi wa Khilafah wangeachwa peke yao na Umma wa Kiislamu, ungeikumbatia Dawah, ungeichagua hukmu ya Kiislamu, na kuweka kiapo cha Bayah kwa Khalifa wake kutawala kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw).
Hivyo basi, sera ya Marekani na muungano wake wa Makruseda ilikuwa ni sera duni, iliyojengwa juu ya msingi wa kutaka kwamba vibaraka na wafuasi wao katika nchi za Waislamu waitenge zaidi Da’wah na Ummah wa Kiislamu, kupitia kupigwa marufuku, mateso, kufungwa jela, na ukandamizaji, kwa nguvu zao zote, kama vile Maquraish walivyofanya kwa bwana wa wanadamu, Muhammad (saw) walipomsusia yeye (saw) na maswahaba zake (ra), wakawatesa, wakawapiga marufuku, na wakaeneza uongo katika makabila kuhusu as-Sadiq al-Amin (mkweli, mwaminifu) na kuhusu Da’wah yake. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) aliipa nguvu Dini yake na kuifanya ishinde dini zote. Na mambo hivi karibuni yatakuwa vilevile, in shaaAllah, kwa wabebaji Da’wah ya Khilafah ingawa Marekani na mkuu wake wa ujasusi wanachukia hilo. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[يُرِيدُونَ أَنْ يُطْفِئُوا نُورَ اللهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللهُ إِلَّا أَنْ يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [Surah At-Tawbah 32].
Inabakia kuzingatiwa kuwa watu wetu nchini Bangladesh, na wenye ikhlasi katika Jeshi la Bangladesh, wanalengwa na vikosi vya Magharibi kafiri. Vikosi hivi haviwatakii kheri, jambo ambalo linadhihirika kwa kuregea Uislamu na kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hiyo, wanajitahidi kuzuia ukaribu wao na wabebaji Da’wah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah. Hivyo basi, ni lazima waelewe nyuzi za njama hii, na wajitahidi kuizuia kwa kufanya kazi kwa umakini na Hizb ut Tahrir. Kadhalika, watu wenye ikhlasi katika Jeshi la Bangladesh lazima waharakishe kutoa Nusrah kwa Hizb kabla ya Amerika kufanikiwa kuwapanga nguvu vibaraka wake nchini Bangladesh, na labda hata kumrudisha dhalimu Hasina madarakani, kwa mara nyingine tena. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَاللهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ]
“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.” [Surah Al-Baqarah 2:105].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |