Ijumaa, 27 Shawwal 1446 | 2025/04/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Ramadan 1446 Na: H 1446 / 101
M.  Jumamosi, 29 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tangazo la Matokeo ya Kuutafuta Mwezi Muandamo wa Shawwal 1446 H

Pongezi kwa Idd Al-Fitr Iliyobarikiwa

(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Alhamd

Bismillahi Ar-Rahman Ar-Raheem. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehma na amani zimshukie mbora wa Mitume, bwana wetu Muhammad, na jamaa zake na maswahaba zake wote.

Amepokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba alisema, Nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema: kwamba Mtume (saw) amesema, au alisema: Abu Al-Qasim (saw) amesema: «صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ» “Fungeni kwa kuuona (mwezi muandamo) na fungueni kwa kuuona. Lakini ikiwa (kwa sababu ya mawingu) utafichika, basi timizeni siku thelathini.”

Baada ya kuutafuta muandamo wa mwezi wa Shawwal katika usiku huu uliobarikiwa wa Jumapili, muandamo wa mwezi mpya umethibitishwa kulingana na mahitaji ya Shariah. Kwa hivyo, kesho, Jumapili, itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd ul-Fitr iliyobarikiwa.

Kwa mnasaba huu, Hizb ut Tahrir inatoa pongezi zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu kwa mnasaba wa Idd ul-Fitr iliyobarikiwa, na kumuomba Mwenyezi Mungu airegeshe mwakani huku dola yake ikiwa imeasisiwa, Dini yake imepewa tamkini, na Uislamu wake mtukufu umetukuzwa. Vile vile natoa pongezi maalum, kwa niaba yangu na Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amhifadhi). Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amjaalie mafanikio katika kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume mikononi mwake.

Huku tukiwa na uchungu wa janga la miongo mingi la vita ambavyo vimekumba Ummah wetu wa Kiislamu, huku vita vimoja vinapomalizika vyengine vinazuka, na kuwaangamiza watu wake na kuchukua uhai wao—sio kwa udogo ni vita vya kikatili ambavyo vimekuwa vikiendelea dhidi ya watu wetu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi tangu Oktoba 7, 2023—hata hivyo tunatazamia kutokea kwa mabadiliko ambayo yanaanza kujitokeza, na kubadilisha hali ya Umma wa Kiislamu kutoka ile ya mauaji na kudhalilishwa hadi ile ya ushindi na izza, na, Mwenyezi Mungu akipenda, kumaliza mikasa ya Umma.

Tangu mapinduzi ya Kiarabu, kisha Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na kuanguka kwa mhalifu Bashar al-Assad, Umma wa Kiislamu umekuwa katika hali ya msukosuko na mgongano na uhalisia uliowekwa juu yake na Magharibi. Umekuwa ukifahamu zaidi ubaya wa uhalisia huu na kuwa na hamu zaidi ya kujikomboa kutokana nao. Umekua karibu na Uislamu, na kuwa na nguvu zaidi na dhamira zaidi kukabiliana na watawala wake katika jaribio la kurudisha mamlaka yake kutoka kwao.

Ummah umepitia mateso ya kubaki chini ya nira ya tawala za vibaraka. Umeshuhudia kwa macho yake wenyewe watawala wakifuja mali zake kwa makafiri, wakoloni wa Magharibi, kuzitelekeza kwao na sababu zake, kuzuia kwao majeshi kusonga ili kuinusuru Palestina kutoka kwenye makucha ya Mayahudi wahalifu, uingiliaji wa wazi wa Magharibi katika dini yake na uadilifu wake, na jaribio la kuulazimisha kulishuhudia  umbile la Kiyahudi, na kuuacha na chaguo kati ya uhalalalishaji mahusiano au kifo. Mandhari na matukio haya yote yameufanya utambue kwamba bila ya utawala wa Uislamu, utabakia kukoloniwa, kulengwa, na kudhalilishwa. Kukinaika kwake kwa haja ya dola ya Khilafah kumeimarishwa, na kwa hakika, Khilafah imekuwa ni kiu yake.

Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, Umma umeanza kutafuta njia na haukubali tena kuakhirisha utabikishwaji wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Una chuki ya wazi na dhahiri kwa usekula. Katika Ash-Sham, unataka kwamba watawala wake wapya waitangaze kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, na katika ardhi zote, unawafuatilia, ukimuomba Mwenyezi Mungu Awajaalie mafanikio na uongofu.

Nchi za Magharibi ziko katika hatua yake dhaifu katika kuudhibiti Ummah, na kwa hivyo ziko katika ukali wake zaidi, zikijaribu kukazanisha mshiko wake kwa Waislamu na nchi zao. Ndio maana tumeona vita vyake vya moja kwa moja na vya wakala, lava ikimiminika juu ya Umma wa Kiislamu na nchi zake, ikiua na kuangamiza nchi nzima. Pia tunaiona ina hamu ya kuiba mali zao, na yote hayo ni kwa sababu tu inatambua kwamba hii ni ngoma yake ya mwisho kabla ya kupoteza ushawishi na vibaraka wake katika nchi za Kiislamu, milele.

Ni kweli kwamba mtu anaweza kusema kwamba nchi za Magharibi zina mashini kubwa ya kuua na zina vibaraka wanaowadhibiti Waislamu. Zinadhibiti vifaa muhimu vya ulimwengu, zinafuatilia nchi za Kiislamu, zinazipeleleza, na kuhesabu pumzi zao. Walakini, Magharibi ni wanadamu kama sisi. Kama tunavyoshuhudia, Mwenyezi Mungu ameishughulisha Magharibi na nafsi yake, na nyoyo zao zimegawanyika. Sisi ni wenyeji wa ardhi hizi, wao ni wageni kwao, kwa hiyo sisi ndio wenye nguvu zaidi ndani yazo. Fauka ya hayo, Ummah wa Kiislamu umeingia katika migogoro ya moja kwa moja na nchi za Magharibi nchini Iraq, Afghanistan, Palestina, Syria na kwengineko, na imedhihirika kuwa popote pale ambapo juhudi zilikuwa za dhati na za pamoja, Magharibi ilishindwa na kujiondoa. Kurudi kwake katika ardhi hizi ni kwa sababu tu watawala walikula njama dhidi yake kwa mara nyengine tena, na kuwafunulia migongo yao ili iweze kuwadunga mgongoni. Hii inatuleta kwenye ukweli usioepukika: Magharibi haiwezi kukabiliana na Umma wa Kiislamu isipokuwa kwa msaada wa watawala wasaliti. Haya yamekuwa ni mazoea yake tangu kuvunjwa kwa Khilafah hadi leo. Kwa hiyo, Umma wa Kiislamu lazima uwaondoe watawala vibaraka na kumlisha adui katika juhudi ya pamoja chini ya uongozi wa kweli kama Hizb ut Tahrir ili kufikia lengo hili na kuregesha nguvu zake. Kuna uzi mwembamba tu baina ya Ummah na ushindi.

Enyi Waislamu: Ukombozi unaweza kupatikana wakati wowote. Mmeona jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyokuteremshieni ushindi katika sehemu nyingi. Mlikuwa washindi mulipofanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. [Muhammad: 7].

Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na azma ya vijana wa Kiislamu, muliweza kulazimisha uhalisia mpya kwa Magharibi huko Ash-Sham, Afghanistan, na Palestina. Kafiri Magharibi ni dhaifu kuliko inavyoonekana.

Kwa wale wanaofanya kazi uwanjani ya kuunda rai jumla: Msiushughulishe Ummah wenu kwa fikra finyo na purukushani zinazopoteza juhudi. Badala yake, elekezeni juhudi zenu kuelekea katika kuuongoza kwenye kutekeleza sheria ya Kiislamu kama mfumo kamili wa maisha usiobadilika. Uungeni mkono ili uweze kujikomboa kutoka katika ukandamizaji wa Sykes-Picot na urudi kwenye fikra na utendaji kama Ummah mmoja, ili Magharibi isiweze kuukabili.

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi: Hii ni fursa yenu kuushika mkono Ummah kuelekea kwenye utukufu na tamkini, na kuukomboa kutokana na watawala wahalifu, na kutoka kwenye utawala wa wakoloni makafiri juu yake. Sasa munaweza kuona kiburi cha Magharibi na jinai zake dhidi ya Ummah wenu, ardhi zenu na mali yenu. Basi kuweni kama Saad, As’ad na Usaid, kuandika kurasa za mustakabali kwa wino wa nuru kama walivyo andika watangulizi wenu wema, answari wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Basi fanyeni hima, enyi maafisa na wanajeshi wa majeshi ya Waislamu, wala msiogope yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ni Al Qahir (Mtii) juu ya waja Wake na ni Muweza wa kila kitu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِن يَنصُرْكُمُ اللهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. [Aali-Imran: 160].

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La illaha illa Allah… Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahil Hamd

Mwenyezi Mungu azikubali amali zenu njema, Idd Mubarak

Usiku wa Jumapili ndio siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal wa mwaka wa Hijria wa 1446 sawia na 30 Machi 2025 M.

Mhandisi Salah Eddine Adadah

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu