Ijumaa, 20 Shawwal 1446 | 2025/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kufeli kwa Ruwaza ya Burundi 2025

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kufuatia Makubaliano ya Amani ya Arusha mwaka 2000, Ruwaza ya Burundi 2025 ambayo ililenga kuwapatia Warundi maendeleo endelevu ilianzishwa mwaka 2003. Hata hivyo, huku ikiwa katika mwaka wake wa mwisho wa utekelezaji hakuna malengo yake yoyote ambayo yamefikiwa.

Maoni:

Burundi, ambayo ilipata uhuru wake wa bendera mwaka 1962 kutoka kwa Ubelgiji, ilipitia migogoro mingi ya kikabila iliyoegemezwa kwenye ukabila ambayo hatimaye ilisababisha vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miaka 12 kuanzia 1993. Hatimaye katika mwaka wa 2000 baada ya msururu wa mazungumzo ya mchakato mrefu wa mpito wa kisiasa nchini Tanzania, Makubaliano ya Arusha yalipitishwa ambayo yalikuja na Ruwaza ya 2025.

Ruwaza hiyo imeweka mambo muhimu katika malengo matatu ambayo ni: kuweka utawala bora, maendeleo ya uchumi imara na shindani na uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi wa Burundi.

Kuhusu uwekaji wa utawala bora, serikali ililenga kupiga vita ufisadi na kuunda serikali shirikishi kwa wote. Hali iliyopo uwanjani ni kinyume na hili. Kulingana na Ripoti ya ‘Freedom House 2024’, ufisadi umeongezeka nchini Burundi ambayo ilipata pointi 4 mwaka wa 2024 kutoka pointi 3 mwaka wa 2000. Burundi mara kwa mara inaorodheshwa miongoni mwa nchi fisadi zaidi duniani.

Pia, kuna uwepo wa mgawanyiko mkubwa wa kijamii katika jamii ya Burundi unaoegemezwa kwenye misingi ya kikabila hasa miongoni mwa makabila mawili makuu: Wahutu na Watutsi. Kwa mfano, upinzani hasa Watutsi na wafuasi wao wanakabiliwa na unyanyasaji, vitisho na hata mauaji na kuwalazimisha wengi wao kufanya shughuli zao uhamishoni.

Suala la kuendeleza uchumi imara na shindani pia limeonekana kutofanikiwa. Serikali ililenga kurekebisha mwelekeo hasi wa Pato la Taifa kwa kila mtu ambalo nchi imekuwa nalo kwa kipindi kirefu cha zaidi ya muongo mmoja, na kuhakikisha linapanda kutoka USD 137 hadi USD 720 mwaka 2025, ili kupunguza kasi ya umaskini na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hadi wastani wa 10%.

Pato la Taifa kwa mtaji lilikuwa USD 362 mwaka 2023, USD 320 mwaka 2024 na USD 156 mwaka 2025. Hii inaonyesha kuwa kufikia Pato la Taifa la USD 720 kwa mtaji ni jambo lisilowezekana mwaka 2025. Kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa asilimia 4.6 mwaka 2024 na ukuaji wa asilimia 5.9 mwaka 2025 haujafikiwa. Burundi bado ni miongoni mwa nchi maskini duniani ikimaanisha kuwa serikali imeshindwa kuboresha hali ya maisha ya watu kama ilivyopangwa katika Ruwaza yao ya 2025.

Kwa kweli, viongozi ndani ya chama tawala CNDD–FDD na maafisa wengi wa serikali wametanguliza udhibiti wa rasilimali za kiuchumi ili kuendeleza utawala wao na kutimiza matarajio yao ya kiuchumi badala ya kuwatumikia wananchi.

Kuhusu uboreshaji wa hali ya maisha, mambo hayajaboreka. Raia wengi wa Burundi wanakabiliwa na ukosefu wa ajira, huku kilimo kikisalia kuwa shughuli yao kuu ya kiuchumi inayoajiri 90% ya watu kwenye kilimo cha kujikimu.

Upatikanaji wa huduma za afya uko mashakani, kwa kuwa serikali bado inatumia bajeti ndogo, wakati imekuwa vigumu zaidi kwa Warundi walio wengi kufuatia hali ya kupitishwa kwa mfumo wa kuregesha gharama mwezi Februari 2002. Wagonjwa bila kujali uwezo wao lazima walipie ushauri wote wa matibabu, vipimo, madawa, kukaa hospitalini, nk. (Chanzo: The British Journal of Practice).

Fauka ya hayo, Burundi inakabiliwa na ukosefu wa wafanyikazi wa matibabu wenye mafunzo, wengi wao wanafanya kazi katika taasisi za kibinafsi au kuruka hadi nchi jirani ya Rwanda kutafuta pato zuri (Chanzo: Human Right Watch). Sehemu kubwa ya wakaazi wanaishi chini ya mstari wa umaskini, jambo ambalo ni vigumu kwao kumudu makaazi bora.

Kulingana na Ripoti ya World Happiness 2018, Burundi iliorodheshwa miongoni mwa mataifa yenye furaha ndogo. Bila kusahau kwamba Burundi ilikuwa na lengo la kuendeleza mtaji wa watu ambao ni rasilimali tajiri zaidi ya taifa, lakini kwa kutabanni mtazamo wa kibepari inaachana na mipango hiyo, badala yake inapunguza ongezeko la watu kutoka 2.5% hadi 2% kwa mwaka.

Kama nchi nyingine nyingi zinazoendelea, Burundi ni tajiri yenye wakaazi wapatao milioni 14, ardhi ya ukulima ambayo inazalisha aina bora zaidi ya kahawa duniani (arabica), misitu ya asili inayokadiriwa kuwa hekta 172,000 yenye zaidi ya spishi 2,500 za mimea na miti migumu, aina mbalimbali za rasilimali za wanyamapori, rasilimali za maji kama Ziwa Tanganyika, Ziwa Rweru na Ziwa Cyohoha, hifadhi ya nickel inayokadiriwa kufikia tani milioni 180, hifadhi ya dhahabu, nk.

Licha ya hayo yote hapo juu, cha kushangaza Burundi inajulikana sana kuwa moja ya mataifa masikini zaidi yasiyo na matumaini. Kufeli kwa Burundi na nchi zote zinazoendelea kunachangiwa sana na mfumo wa ubepari wa kikoloni ambapo nchi za kikoloni za Magharibi zinanyonya na kuzikoloni nchi maskini kupitia ukoloni mamboleo.

Burundi imelazimishwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kikabila na Amerika kwa upande mmoja, na Wazungu chini ya Uingereza kwa upande mwingine, ikilazimisha uongozi kupitia mapinduzi ya kijeshi na mauaji yanayopendelea wakoloni hao wawili kwa gharama ya Warundi.

Mfumo wa ubepari kutoka katika ilokuwa koloni ya kikatili ya Ubelgiji na ukoloni mamboleo wa sasa wa Marekani na Ulaya umefeli Burundi, na usingeweza kamwe kupona chini ya kauli mbiu tupu ya Ruwaza ya 2025. Kile ambacho kitaikomboa Burundi na mataifa mengine yanayoendelea ni kuondokana na mfumo wa kishenzi wa kinyoyaji wa ubepari, kisha kutabanni mfumo wa haki na uadilifu wa Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah kama badali.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu