Tawakkul (Kumtegemea) Mwenyezi Mungu: Sababu nyuma ya Mafanikio Makubwa ya Umma wa Kiislamu
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ukisoma historia ya Umma wa Kiislamu, mtu ataona ufunguzi mkubwa ambao ulipitia, ambao hakuna taifa jengine lililowahi kuupata. Waislamu walitoka Bara ya Arabu na kupigana na dola kubwa duniani kwa wakati mmoja, Dola ya Kirumi, Himaya ya Byzantine na Himaya ya Kifursi. Anapoangalia hili mwanzoni mtu atasema: watu hawa wenye kichaa ni kina nani?