Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Machozi ya Wanawake wa Kiislamu wa Eritrea Hayatakauka bila ya Khilafah!

(Imetafsiriwa)

Mnamo 2008 vita vilivyokuwa vikiendelea kati ya Ethiopia na Eritrea vilimalizika rasmi. Hata hivyo, kuyumba kwa eneo hilo kunakochochewa na fikra za utaifa kumesababisha serikali ya Ethiopia kuingia katika mienendo ya mizozo na taifa jirani la Tigray. Maelfu wameuawa huku wengi wakikimbia makaazi yao kama wakimbizi katika mizozo ya hivi majuzi. Huku ukame ukikumba eneo zima la Pembe ya Afrika, hakuna dalili za misaada kwa watu ambao tayari wako hatarini wanaokabiliwa na vifo kutokana na vita, baa la njaa na maradhi.

Juu ya maafa yanayowakabili Waislamu wa eneo hilo, majeshi ya Eritrea yanayoingia katika eneo la vita yametuhumiwa kwa ukiukaji wa kutisha wa haki za binadamu. Wanawake wengi wamekiukwa katika mazingira ya uvunjaji sheria bila ya kuwa na njia ya kutafuta haki.

Wengi katika mji mkuu, Asmara, walipewa ilani mnamo Alhamisi, 15 Septemba 2022 na kuhamishwa hadi kwenye mpaka wa eneo la Tigray nchini Ethiopia ndani ya saa chache.

Askari wa akiba hadi wa umri wa miaka 55 wameitwa, na mashuhuda waliripoti kuwa kulikuwa na kina mama, watoto na wake waliokuwa wakilia wakati wa kuwaaga watoto wao, baba, kaka na waume zao.

Matukio haya hayawezi kulinganishwa na njia tukufu ya Jihad ambapo Ummah unapigana kuitetea Quran na Sunnah. Huu ni mpangilio usio na haja wa mateso na kifo unaochochewa na maslahi ya mataifa ya kikoloni yanayopigania eneo la kimkakati la pembe ya Afrika.

Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha mtu yeyote kuwa upande wa njia haramu za utaifa.

(إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ اللَّهُ سَكِينَتَهُ عَلَى رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ)

Pale walio kufuru walipo tia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini ...” [Al-Qur'an 48:26]. Mtume sallallahu 'alayhi wa sallam amesema:

«مَنْ خَرَجَ مِنْ الطَّاعَةِ وَفَارَقَ الْجَمَاعَةَ فَمَاتَ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً، وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً فَقُتِلَ فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ»

Yeyote anayejiondoa katika utiifu (twa’a) na akajitenga na Jama’ah kisha akafa, amekufa kifo cha kijahiliya. Na yeyote anayepigana chini ya bendera ya upofu, akakasirika kwa ajili ya ‘asabiyyah (ukabila, uzalendo, utaifa) au akalingania ‘asabiyyah au akainusuru ‘asabiyyah kisha akauwawa, amekufa kifo cha kijahiliya.” [Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (6/21), kutoka kwa Abu Hurayrah radhiallahu 'anhu].

Ummah wa Muhammad (saw) hauwezi kuchukulia kuwaua kaka na dada zao kuwa ni kitendo chema au kama kitendo kitakacho wapeleka Jannah. Ni lazima tukatae miito hiyo ya kukiuka Quran na Sunnah. Ni pale tu Khalifah anapotoa wito kwa Ummah kwenye Jihad, ndipo tunapopaswa kuitikia. Hadi wakati huo mahamasisho mengine yote ya viongozi haramu yanakataliwa na lazima yazungumzwe kama yasiyoruhusiwa na Sharia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu