Marekani Yausukuma Ushawishi wa Urusi nje ya Armenia
- Imepeperushwa katika Siasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Nancy Pelosi anazuru Armenia kuhusiana na kuadhimisha mapatano ya Azerbaijan, kituo cha televisheni cha Qatari cha Al Jazeera kinaripoti.
Nancy Pelosi anazuru Armenia kuhusiana na kuadhimisha mapatano ya Azerbaijan, kituo cha televisheni cha Qatari cha Al Jazeera kinaripoti.
Mnamo 2008 vita vilivyokuwa vikiendelea kati ya Ethiopia na Eritrea vilimalizika rasmi. Hata hivyo, kuyumba kwa eneo hilo kunakochochewa na fikra za utaifa kumesababisha serikali ya Ethiopia kuingia katika mienendo ya mizozo na taifa jirani la Tigray.
Zifuatazo ni baadhi ya nukta muhimu kuhusiana na matukio ya hivi sasa nchini Iran kufuatia kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 ambaye inasemekana aliuawa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi la utawala huo, kutokana na kutovaa Hijabu ipasavyo.
Kifo cha Malkia Elizabeth II kimeifanya Uingereza kuingia katika kipindi cha maombolezi ya pamoja. Upeperushaji mpana wa mazishi na utawala wa malkia wa miongo saba umeshughulisha watu. Kumekuwa na mihemko na rambirambi kutoka kote ulimwenguni huku wengi wakimuona Malkia Elizabeth II kama mtu thabiti katika siasa za Uingereza.
Mnamo tarehe 5 Septemba 2022, Seneta wa Pakistan Mushtaq Ahmad aliwasilisha mswada wa marekebisho katika Sheria ya Kuwalinda Wanaobadili Jinsia, 2018, kwa Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Haki za Kibinadamu. Katika mkutano huo, Seneta Mushtaq Ahmad, alisema kuwa, "Transgender ni neno la Kimarekani, halina nafasi katika Uislamu, na sheria kuhusu jamii ya watu waliobadili jinsia ni kinyume na Qur'an na Sunnah na itakuza ushoga."
Waislamu lazima waibuke kutoka katika mporomoko. Hili angalau linakubalika kwa wote, waliberali na wanaharakati wa Kiislamu. Hata hivyo, tafauti inakuja katika fikra zinazopelekea katika uoni huu. Msukumo kwa msimamo wa waliberali ni maendeleo ya ajabu ya kisayansi na ya vitu ya Wamagharibi, ambayo yanaweka kipimo kwa waliberali.
“Tunasikitishwa sana na jinsi vita vya Putin nchini Ukraine vimekatiza pakubwa silsila za usambazaji za kimataifa za chakula na kilimo, na tishio vinavyoleta kwa usalama wa chakula duniani. Tunatambua kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikitegemea chakula na pembejeo za mbolea kutoka Ukraine na Urusi, huku uchokozi wa Putin ukivuruga biashara hiyo.” (Taarifa ya Pamoja ya Ikulu ya White House ya Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen)
Shirika la Anadolu katika makala, "Mamlaka ya Uturuki katika uwanja wa kimataifa yanaongezeka," linatoa mukhtasari wa hotuba ya Rais wa Uturuki Erdogan kwa wawakilishi wa chama tawala cha Haki na Maendeleo.
Baada ya miaka 19 na miezi 9 na kwa gharama ya zaidi ya dolari trilioni 2, serikali inayoungwa mkono na Marekani nchini Afghanistan ilianguka baada ya Taliban kuuzingira mji mkuu, Kabul mnamo Agosti 2021.
Mdahalo wa nchi nzima kuhusu Siku ya Uhuru wa Pakistan, 14 Agosti, umepanuka hadi kuhoji muundo wa katiba na siasa zinazotekelezwa. Ni mjadala wa kimsingi, ambao utafafanua mwelekeo wa juhudi za Waislamu wa Pakistan wanaoteseka kwa muda mrefu, kwa ajili ya mabadiliko.